Kidume mzima unaanzaje kufanya birthday party?

Kidume mzima unaanzaje kufanya birthday party?

Aiseee! Nimeshangazwa na rafiki yangu ni mtu mwenye familia yake kunialika kwenye birthday part yake khaaa! Hivi vidume tumekuwaje sikuhizi? Kidume mzima unaanzaje kuimbiwa happy birthday tu yuuu na wewe umekaa tu unakenua meno? Yani na wewe uvae taji eti kisa birthday!

Haya mambo ebu tuwaachie wavulana wa vyuoni high school na wanawake yani sikuhuzi ungangali wa wanaume wenzangu unapungua ebu tuache utoto wa kusherekea birthday kijinga hivyo. Pia kumekuwa na kamchezo ka mtu kumwagiwa maji hivi izo akili za hivo mnatoa wapi?
Mkuu samahani muhusika anakaa Dar?
 
Katika ujinga ambao siwezi kufanya nihuo maana hivi vitu vimekuja gafra
 
Mimi nafanyaga, waalikwa 65% wanawake, 35% familia, majirani na marafiki wa kiume,
Nimegundua wanawake wanapenda mambo haya ya kusocialise ,
Sasa na mimi napenda mapenzi, ndio hapo natafuta wapenzi wapya
 
kuna masharo nawaona kutaa huku yaani wanakamuana michango kisa birthday,wanakodi gari then wanaenda kufanyia huko fukwen yaani hawana hata muda wa kutafuta helA ;kinachonisikisha zaidi wengine cku ya tukio wanakuja kuazima nguo...
 
Halafu wanakushangilia au kukuimbia How old are you now?? Hahahaahah nawapenda sana sana mabinti zangu wawili, wana akili na huwa hawa-entertain huo ujinga
Yani mkuu, sipati picha kabisa tena unakuta kabana mpaka makalio ili mishumaa izimike vizuri. Teheheh. Vitu vingine tunaiga ila sijui kama tunajua maana yake.
 
Hata mimi hiyo kitu imenishinda kabisa...Ila sababu Bi mkubwa huwa yuko makini sana...Unakuta mimi sijui hata ndiyo Birthday yangu nikifika hme nakuta ameninunulia zawadi kama Saa ama nguo za ndani anafanya surprise fulani kimya kimya then siku imepita hiyo...
Bora unatambua na kuheshim na kuthamini alichokifanya hongera sana
 
Kunakipindi mtoto wangu alitaka kuambukizwa hako kaugojwa na majilin nakaanza kuambiwa o bhd ya mtoto unakalibia nikamwambia huo ujinga sitaki kuuskia paka leo sijasikia habar bhd
 
well huwez fanya bday hupendi au unaamini sio uanaume??? sasa unachokipenda mwingine aanakichukulia ni dhambi kabisa si uanamke wala si utoto . izi likes n dislikes hazijadiliki ni binafsi saaana
 
Ni ujinga uliopitiliza mwanaume kukariri na kuandaa sherehe et ya kuzaliwa............hizi tabia ziko sana wa wanaume wa Dar
 
Si pesa zake kwani alikuomba mchango wa hiyo Birthday kama umekuwa ni wewe wengine bado wanaakili za kitoto
kutoa ushauri n kuomba maoni ya wenzie ni ruksa katiba inamruhusu,acha udikteta kama unakereka nenda kachungulie shimo la choo dk 45 thn unywe juisi ya majani ya mchunga
 
Jana nimemuona Obama CNN akiomba udhuru situation room Pentagon, kwamba asiulizwe maswali mengi ili awahi birthday (yake) dinner na familia.

Hii mnaizungumziaje vidume wa nguvu wa JF?

Mimi kwa maoni yangu nafikiri ni life style tu. Nikiwa peke yangu huwa sifanyi ila tukiwa hom nakumbuka baba alikuwa anatoa hela ya champaign na mama alikuwa anakupikia ur favorite food tunakula familia nzima dinner

Nakaribia kuoa natarajia kuendeleza hii tradition
Yap, ur right!

1470395396679.jpg
 
Back
Top Bottom