Kidato cha nne kutumia kikokotoo (calculator) kwenye mtihani wao wa mwisho ina mpango gani kwa taifa la baadae?

Viva JF

Nikiwa sijui kinachoendelea kwenye kwenye mitihani ya kidato cha nne iliyoanza hii wiki, nikawa nawasiliana na dogo mmoja finalist ananiambia wametangaziwa kuruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na calculator hivyo wamefurahi sana.

Nilijikuta nashangaa na kuchukia ghafla, kwamba watu wazima wanaosimamia Wizara na NECTA wamefikiria nini kuruhusu hili?

Hivi ni kweli nchi nzima Form Four sasa ndio wanaanza kutumia calculator? Ni kama bado siamini.

Hivi ndio ufaulu utaongezeka au ni kuwafanya tu wanafunzi sasa waache kujibidisha?

Hizo calculators watakuwa wanazikagua au ndio bora yoyote, maana kuna scientific one zinatunza mpaka data, nyingine zinaonesha mpaka njia (solution) and many other operations.

Kuna faida gani kuwa na vijana wengi walio na vyeti vizuri mtaani wakati uwezo wao kiakili ku-solve mambo ni mdogo? Maana hizi devices zinadumaza akili hasa kwa vijana wadogo kama Form 4.

Kadri miaka inavyozidi kwenda, mfumo wa elimu nchini unazidi kuwa mbovu na rahisi kwa watoto kufaulu. Walianza na lile la multiple choices kwenye hesabu wakaona haitoshi sasa ni mteremko tu, sielewe lengo ni nini hasa kama sio kuandaa taifa la wavivu kufanya kazi na wavivu kufikiri.

God Bless America

Mkuu, ni kwanini watanzania wengi tunadhania kuwa kupata Elimu kwa nji ya mihangaiko, ndio kukomaa kiakili?

Kuitumia hiyo calculator yenyewe inahitaji uwe na akili tosha! tusikomae na mambo ya matumizi ya nguvu nyingi katika ulimwengu wa science! ulimwengu tulio nao ni wa science! matumizi ya vyombo ya kidigitali ndio zama zake!

Naona watu wengi hatujali kabsa muda wetu, huwa tunaona muda upo tu as if umesimama kutusubiri! na hii ndio inapelekea kuwa na mentality za ajab katika inchi yetu.

Tunahitaji kutoka hapa tulipo, kifikra na kiuchumi na hata kimaendeleo!!

Machine au technologia ipo kwa ajili ya kurahisisha mambo mbalimbali kulingana na muda mchache tulio nao!

Ndio mana hata juzi kuna member amekuja kukosoa matumizi ya OREX katika Chuo Kukuu Huria, huku akiwa hana utetezi wa hoja yake kikamilifu

Wenzetu wanazidi kurahisisha maisha ili kuendana na muda mchache walio nao, sisi tunazidi kufanya mambo yawe magumu kwanini!

Tibadilike!
 
Back
Top Bottom