Kidato cha nne kutumia kikokotoo (calculator) kwenye mtihani wao wa mwisho ina mpango gani kwa taifa la baadae?

Nasisitiza tumechelewa sana ,tena serikali inatakiwa kuongeza wigo na teknolojia zaidia katika elimu. Twende na wakati pamoja na zama zake 2020 haitokuwa sawa na 2000

Kutumia kikokotozi hakufanyi mtu kuwa mjinga
Safi sana mkuu,tatizo la sisi tunafikiri kwa kutumia tumbo, wenzetu wanafanya mitihani ya paper less, yaani ni kutumia teknolojia na mambo ya codes ambayo ndio future sisi tumesimama kwenye miaka ya 47 lengo la chama tawala ni kuwa na taifa la wajinga ili utawala wao uendelee.
 
ISLETS, Unasumbuliwa na roho ya kwanini. Watu dizaini yako ni wale wanaoamini maisha ni kuteseka, bila kuteseka wanaona sio maisha. Calculator inasaidia kupunguza muda wa kufikiria maana yake mwanafunzi ataongeza ufanisi kwenye calculations.
 
Graph,
Hakuna mtu anayejua saikolojia na sayansi ya ukuaji wa watoto atatoa hoja kama yako. Hata hivyo sawa najua hatuwezi kurudi nyuma maana na ni kawaida kuiga mambo tena kwa wazungu pasipo kujua misingi yao tangu utotoni.

Mtu mwengine anatoa hoja ya kumaliza maswali, kwani waliokuwa wanamaliza yote wao vichwa vyao vikoje? Au ulishindikana ndio mbadala ya kulinganisha wingi wa maswali na muda wanaopewa?

Leo hii kuna form four wana miaka 16, 15, mpaka 14, huyu bado yupo kwenye hatua ya ukuaji, bado ana nafasi ya kuuboresha ubongo wake tofauti na mtu wa miaka 18, 19 au 20.
 
ISLETS,
Hao wa kuacha mikasi tumboni ni hao wa zamani ambao walikuwa hawatumii calculator. Halafu sidhani Kama ni suala zito kivile maana madarasani sidhani kama wanatumia calculator isipokuwa kwenye mtihani tu.
 
Toka nilivyoanza kutumia calculator advance uwezo wangu wa ku-calculate vitu vikubwa vikubwa kwa kichwa kiukweli umepungua sana.
 
kifusi boy, Imetumika kwenye Basic Maths pia, wala haina tatizo maana matumizi yake ni kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzidisha tu.
 
KENZY,
Mambo huanza taratibu, kutoka kutumia kwenye mitihani wataanza darasani kwa vigezo kuwa mbona masomo ya tech na advanced level wanatumia.
 
Unasumbuliwa na roho ya kwanini

Watu dizaini yako ni wale wanaoamini maisha ni kuteseka, bila kuteseka wanaona sio maisha.

Calculator inasaidia kupunguza muda wa kufikiria maana yake mwanafunzi ataongeza ufanisi kwenye calculations

Sawa, endeeni kupunguza muda wa kifikiria, sijui mnataka ubongo ufanye kazi gani baada ya kuupunguzia majukumu ya kufikiria.
 
ISLETS,
Baada ya miaka mingine kadhaa watafanya OPEN BOOK EXAMINATION; Ufaulu utategemea uwezo wa kujua swali linatoka "topic" gani
 
Ila mtaala wa Tanzania ni vichekesho. Mitaala mengine tulianza kutumia non scientific calculator tangu standard 7.
 
ISLETS,
Mtu wa Form four unamuita mtoto?
We psychology umesomea wapi? Kama ya wazungu huyataki acha kutumia JF, tupa simu kule na usitumie electronic devices zozote maana zote hizo wamezileta wao, tusiige wakatii wao kisayansi na elimu wamefika mbali kutuzidi? Kutumia calculator sio kuiga, tatizo unaleta chuki zako kwa wazungu kwenye mambo ya elimu ambayo ni ya msingi.

Elimu inabadilika, ubongo wa binadamu unabadilika, leo hii Form four sio sawa na ya miaka ya 80, Form four sio muda wa kukaa unatumia kalamu ku-calculate, maswali yanazidi kuwa magumu yanayohitaij mtu ajue concept nyingi sio kukaa anapoteza muda kucalculate namba ndogo ndogo.

Wewe unampa mtoto swali kucalculate umbali wa sayari kutokana na red au blue shift, formula zina exponents, kuna namba ndogo ndogo kibao unataka akae atumie kichwa huku dunia nzima inatumia computer kucalculate vitu kama hivyo?

Matatizo yako:

1. Una chuki binafsi na wazungu
2. Hujui kuwa elimu inakua
3. Umebaki nyuma na beliefs zako za kizamani unataka kila mtu azifate hizohizo, naomba nikuulize zimetufikisha wapi? Elimu ya zamani imetufikisha wapi kama nchi? Hadi leo mtu anagraduate chuoni hawezi tengeneza hata baiskeli alafu unataka tupoteze muda na hesabu za kujumlisha badala ya kukaa tukafikiria concept za kurusha rocket nje ya sayari? Wewe utarusha rocket kwenda Mars utapanda alafu utumie kalamu na karatasi kucalculate speed ya fuel ejection? Acha utani
 
Mleta mada, ungetafuta taarifa za ukweli juu ya ulichokisikia ndipo ujenge hoja badala ya kulalamikia jambo usililolijua kiundani.
Kuna wadau wamekutajia aina za calculators.

Kuna barua imeandikwa kutoka NECTA ikionesha aina za calculators na model yake.
 
ISLETS,
Kwani dunia ya sasa kuna mtu anapiga hesabuu kichwani? Maana hata jiwe namba zikiwa mingi anauliza wasaidizi wake.
Halafu sisi tuliotumia vichwa tumelipeleka wapi Taifa mpaka wanaotumia calculator tuwaone wanakosea.
 
ISLETS, Hawa jamaa hawalijui hili, kufaulu mtihani wenye calculation inaonyesha kuwa mtu huyu ni makini. Kama pia wanatumia scientific calculator hadi kwenye Basic Maths,basi hili ni kosa, maana kuna maswali mtu unaweza kuyafeed kwenye calculator na ukapata majibu.

Kwa kulitazama hili kwenye angle ya ukuaji wa akili halijakaa sawa, watoto wasolve kwa kichwa
 
Graph, Kwa O-level kutumia calculator ni kudumaza tu akili. Akili inabidi iwe sharp, baada ya kuwa sharp wakifaulu wakienda A-level ndio wanatumia calculator maana ni complex level.
 
Graph,
Huyu muanzisha mada inaonyesha ni jinsi gani alivyokuwa mgumu kubadilika kutokana na wakati, hajui hata hao magenius anaowaona huko uUaya miaka hii wengi wao wamekuwa wakifanya mitihani yao kwa kutumia calculator pale inapobidi.
 
Back
Top Bottom