Kidato cha nne kutumia kikokotoo (calculator) kwenye mtihani wao wa mwisho ina mpango gani kwa taifa la baadae?

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,192
Points
2,000

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,192 2,000
Viva JF

Nikiwa sijui kinachoendelea kwenye kwenye mitihani ya kidato cha nne iliyoanza hii wiki, nikawa nawasiliana na dogo mmoja finalist ananiambia wametangaziwa kuruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na calculator hivyo wamefurahi sana.

Nilijikuta nashangaa na kuchukia ghafla, kwamba watu wazima wanaosimamia Wizara na NECTA wamefikiria nini kuruhusu hili?

Hivi ni kweli nchi nzima Form Four sasa ndio wanaanza kutumia calculator? Ni kama bado siamini.

Hivi ndio ufaulu utaongezeka au ni kuwafanya tu wanafunzi sasa waache kujibidisha?

Hizo calculators watakuwa wanazikagua au ndio bora yoyote, maana kuna scientific one zinatunza mpaka data, nyingine zinaonesha mpaka njia (solution) and many other operations.

Kuna faida gani kuwa na vijana wengi walio na vyeti vizuri mtaani wakati uwezo wao kiakili ku-solve mambo ni mdogo? Maana hizi devices zinadumaza akili hasa kwa vijana wadogo kama Form 4.

Kadri miaka inavyozidi kwenda, mfumo wa elimu nchini unazidi kuwa mbovu na rahisi kwa watoto kufaulu. Walianza na lile la multiple choices kwenye hesabu wakaona haitoshi sasa ni mteremko tu, sielewe lengo ni nini hasa kama sio kuandaa taifa la wavivu kufanya kazi na wavivu kufikiri.

God Bless America
 

kifusi boy

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
968
Points
1,000

kifusi boy

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
968 1,000
Calculator inatumika katika mitihani miwili tuuya Chemistry na Physics, basi. Halafu sio dhambi Mkuu, kingine kama wachangiaji wengine walivyosema juu hapo kila zama na watu wake. Wao wakitumia calculator wewe inakuuma nin? Au utapungukiwa nini?

Nadhani unajua shughuli ya kutomaliza maswali kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha 4 hususani kwenye Chemistry na Physics ambapo kunakuwa na mambo mengi.

Acha vijana wasome.
 

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
8,385
Points
2,000

KENZY

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
8,385 2,000
Hebu fikiria hivi mtu anajua njia ya namna ya kusolve swali ila anakosea kwenye kuzidisha namba moja tu, hapo inamaanisha kakosa. Sasa huyu kwa kukosea sehemu moja tu anajua au hajui?

Mimi nafikiri calculator ni kwa ajili ya kupunguza muda hivyo inamrahisishia mwanafunzi kufanya maswali mengi zaidi. Tena, ikibidi waongeze na dictionary maana kuna baadhi ya maswali mwanafunzi anakosa kisa hajui msamiati mmoja tu. Ila kama angekuwa anaujua ina maana swali husika lisingemchenga. Mkuu mbona hata four figure huwa zipo na wachache ndiyo hutumia wengine hawajui.
 

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Messages
1,466
Points
2,000

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2013
1,466 2,000
kifusi boy, Si hayo tu, bali ni pamoja na Geography, Basic Mathematics, Engineering, Book Keeping, Survey, Agriculture, Electrical Installation.

Halafu sio dhambi Mkuu, kingine kama wachangiaji wengine walivyosema juu hapo kila zama na watu wake... wao wakitumia calculator wewe inakuuma nin!? au utapungukiwa nin?
Mimi mwenyewe nawaunga mkono NECTA kwa kupitisha uamuzi wa kutumia calculators kwa sababu kama vile:
1. Wanafunzi wengi walikuwa hawamalizi maswali ya calculations.
2. Kukosea kuzidisha au kugawanya wakati njia ni sahihi, hivyo kukosa marks kwa sababu ya kukosea kidogo kwenye kugawanya, kuzidisha, kujumlisha au kutoa.

Lakini kubwa zaidi, mleta mada atambue kwamba calculators zilizoruhusiwa ni zile non programmable calculators ambazo sidhani kama zinadumaza akili ya mwanafunzi.
 

Avriel

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2017
Messages
2,651
Points
2,000

Avriel

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2017
2,651 2,000
Imekuwa kama advanced level sasa, hatua kubwa. Itapunguza pia matumizi ya four figure.
Maboresho.
 

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,192
Points
2,000

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,192 2,000
kifusi boy,
Bado na Mathematics na Geography pia. Kwa hiyo mnapenda tu kusikia ufaulu umeongezeka wakati watoto hata hesabu za kujumlisha atategemea calculator!
 

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,192
Points
2,000

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,192 2,000
KENZY
Mtihani unapima vitu vingi, sio kukariri tu ni pamoja na umakini wa mwanafunzi. Mwanafunzi anayekosea namba moja maana yake kakosa umakini hivyo ni hahali yake kukosa hilo swali.

Leo hii ukisikia mtu anaendesha gari anaparamia ukuta, au daktari anasahau mikasi ndani ya tumbo la mgonjwa, shida si kwamba hawajui kazi zao ila ni kwamba wamekosa umakini kwenye kazi.

Hili ni jambo la kuanza kujifunza tangu wakiwa watoto shuleni.
 

Graph

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Messages
2,206
Points
2,000

Graph

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2016
2,206 2,000
Kuruhusiwa calculator ni kitu kizuri, tatizo mnakariri, huwezi sema devices zinatumika kudumaza akili. Calculator inadumaza akili? Wewe unapima mtu uwezo wa kujumlisha na kugawanywa kwa haraka au unapima uwezo wake wa kufikiri na kusolve matatizo?

Calculator inatumika kwenye kila kitu duniani siku hizi, hata simu unayotumia ni calculations zinafanyika billions ot times kila sekunde, kila mwanafunzi wa Form 4 tayari anajua hesabu za kutoa na kuzidisha, au hata vitu kama matrices hakuna haja ya kufanya kwa kutumia karatasi kabisa, hata nchi za nje hatatumii kichwa kufanya mambo haya.

Ya nini utumie kichwa huku technology ipo? Unadhani calculator kesho yake zitakufa zote dunia nzima alafu tushindwe kucalculate? Kutumia ile Four figure kutafuta cosine na sine ni upuuzi mtupu, hakuna mtu anatumia ule upuuzi duniani.

Siku hizi tunasolve matatizo makubwa makubwa yanayohitaji very precise calculations, trust me hakuna scientist duniani anacalculate kwa kutumia kichwa hata moja.

There's more to Maths than kujumlisha na kutoa, ushamba ndio unasumbua watanzania wengi.
 

Forum statistics

Threads 1,379,308
Members 525,377
Posts 33,742,157
Top