Kidato cha nne kutumia kikokotoo (calculator) kwenye mtihani wao wa mwisho ina mpango gani kwa taifa la baadae?

Nkanini,
Tunaifanya elimu yetu kuwa ngumu tukiamini ndio uelewa. Unakuta mzungu kasoma course chache za ujenzi ila anaweza simamia ujenzi hata ghorofa likaanguka ,sisi tumekariri injinia lazima akeshe na mavitabu wakati kazi inahitaji expert katika field. Nina mfano kuna jamaa kitambo tulisoma naye tukamaliza form 4 yeye akaenda nje baada ya miaka mitatu na nusu tayari na kazi yake.
 
Darmian,
Akili inakuaje sharp? Hivi unadhani kucalculate 3444.22323^2 / 8483.2233344 * 32.333 inafanya akili iwe sharp au inapoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi ambayo hakuna anayefanya kwa ubongo siku hizi?

Form four wanajua vizuri hesabu basic hizi kujumlisha na kutoa, hakuna sababu yoyote ya wao kufanyia kichwa tena namba ndefu ambazo hakuna mtu anatumia kichwa kucalculate, ubongo sharp inamaana dunia nzima wanakosea bongo tu ndo mnajua kukuza ubongo wa watu uwe sharp? miaka ya nyuma ambapo walikuwa hawatumii calculator na ubongo wao sharp wamefanya nini hadi leo?

Wanaotumia calculator wamekuletea computer, simu, wamefika mwezini, leo wanatengeneza rocket kuruka kwenda mars, sisi ambao miaka yote tulikua hatutumii huo ubongo sharp umetuletea nini? tumetengeneza hata jembe la kulima kweli? au hata majembe tuna-weld kwa kutumia machine walizotutengenezea watumia calculator?

Nimejua kwa nini elimu ya bongo haibadiliki, sababu ni wengi hampendi mabadiliko mmekariri ila hamkusoma mkajua challenges zilizopo Tanzania, tunapoteza muda kwenye mambo ya kijinga badala ya kufocus kwenye uelewa ambacho ndio kitu cha muhimu.

Unavyojifunza kutengeneza daraja litakaloweza kusimama urefu flani na kupitisha magari ya tani kadhaa, huendi kujifunza kujumlisha na kutoa, hayo yote utatumia calculator, unaenda kujifunza utumie material ipi, uliweke daraja katika angle ipi, utahandle vipi upepo, pressure ya maji etc. Hivyo ndio vya muhimu vya kujifunza 99.99999%. hiyo 0.00001% ya calculation inafanywa kwa computer siku hizi kwa kua binadamu kawaida hua tunafanya makosa kucalculate namba ndogo.

Embu jaribu kukubali mabadiliko sio mmekaa na njia zenu za kizamani ambazo hazijawafikisha popote pale.
 
Wick,
Tuliko sasa sio tulikokuwa jana japo hatujafika tunapotakiwa kuwa. Kama viungo vyote vya mwili vinavyohitaji mazoezi, ubongo nao unahitaji kuwa sharpened, na njia zinazotumika ndio kama hizo za kushughulisha kwa ku-solve calculations, kusoma vitabu, kupractice kwa mambo vya vitendo nk.

Leo hii vyote hivyo tunaviondoa kwa watoto unategemea nini? Maana kusoma vitabu hakuna wanapenda kusikia na kuona, calculations hakuna wanapenda calculators hata kujumlisha, practices hakuna tunakomaa na theories. Hapa hakuna kuendelea bob.
 
stephot,
"Pale inapobidi". Ndio kuna levels na complex calculations, kama ilivyo kwa wanaosoma masomo ya uhandisi, advanced level na vyuo. Maana anachoshughulika nacho pale sio basics of calcutations bali anatumia maths tricks kwenye kusolve kitu kingine.

Mfano mtu wa O-level kwenye Maths bado anajifunza kusolve Log, hiyo ni basics maana akifika advance kwa mfano kwenye Physics atatumia ile basic knowledge ya Log kusolve other calculations, sasa hapo ndio anapoweza kutumia calculator maana hahangaikii kale la Log tena ila anakatumia kuhangaikia kitu kingine.
 
ISLETS,
Uchaguzi ukikariba huku Amerika Kusini lazima utasikia elimu imeyumba, mara GPA, mara merit, mara credit na ukishapita tu utaanza kuona division. So, calculator wala hiyo multiple choice haina miaka miwili, itakwisha tu.
 
ISLETS,
Samahani kwa nitakachokiandika. Lakini mawazo yako haya yalikuwa sahihi miaka angalau 25 iliyopita. Naomba pitia websites za international education halafu uangalie sample exams zao. Wanatoa hadi formulae na jinsi ya kujibu maswali (kwa mfano: when you are asked to describe you should..)

Nitakuelewa ukiniambia kuwa basis ya objection yako ni kuwa hakuwezi kuwa na even playing field maana baadhi ya watahiniwa hawana uwezo wa kuwa na calculator lakini watapimwa kwa namna ile ile.
 
Graph,
Umeandika vingi lakini ni imani yako ndio inakutuma hivyo. Mimi wala siko hivyo. Ninachotetea ni ubora wa elimu na kuona watu wakifaulu kwa akili zao tena wakiwa vichwa kweli kweli, sipendi uzembe uzembe, ujanja ujanja na ukanjanja kwenye maswala ya elimu.

Mnaweza kuona ni kawaida ila siku zitakuja ambako wanafunzi wanaoharibiwa sasa na haya mambo wataishia kuamini kuwa wazungu wanaakili kuliko waafrika, wataamini kuna vitu haviwekekani bila msaada wa calculator, watashindwa kuhoji vitu vidogo vidogo, wataamini constant values zote haziwezekani kuwa zi-derive kwa kichwa kama walivyofanya waliozi-invent, itafikia mahali wataamini hata kusolve 68+(78x35)/22 ni kitu kisichowekekana kwa kichwa cha mwanadamu.
 
Mfiaukweli,
Watakuwa wamefanya la maana kama walingebadili na mfumo wa utungaji wa maswali na mtaala uendane na hiki wanachofanya. Sasa leo hii unampa mtoto swali la magazijuto, unampima nini wakati anaweza akali-feed lote kama lilivyo kwenye calculator na akapata jibu. Kama wakiamua kubadili na mitaala na formats za mitihani hapo hapo sawa.
 
NTABO wa NTABO,
Huyo ni mhafidhina (conservative). Anacholalamikia ni sawa mtu kulalamika hizi pikipiki au magari yanawadekeza watu, anataka watu watembee kwa miguu toka Mwanza hadi Dar kwa siku kadhaa kama sio majuma (weeks).

Calculator ni kuokoa muda na kuendana na wakati kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Watu kama huyu jamaa ni shida kwa watoto wake au kwa wafanyakazi wenzie akiwa kiongozi.
 
ISLETS,
Hao waliogundua calculator ambao unataka tushindane nao ndio waliogundua Four Figure na wameachana nayo kutumia kwenye mitihani ya elimu ya sekondari. Ungekuwa kwenye field ya ICT ungedai watu waendelee na mfumo wa punching cards na batching sytems.

Unataka watu waendelee kulima kwa jembe la mkono kwa madai trekta linadekeza watu, unalima mwezi sehemu ya kulima dakika 10. Unajitetea unajiandaa siku ukikosa trekta usishindwe kulima. Unataka watu waende uUaya kwa majahazi ili wasijidekeze, siku wakikosa ndege wasishindwe kwenda Ulaya.

Unataka watu lazima wafanyiwe upasuaji kwa kuwekwa jeraha kwa kisu wakati inawezekana kutumia mionzi au njia nyingine bila kuchana mwili.
 
Unataka watu waendelee kukomaa na kutwanga nafaka kwenye kinu badala ya kutumia mashine kisa usijidekeze?
Ni matumizi mabaya ya akili na rasilimali watu na muda.
 
ISLETS,
Swali la magazijuto linaweza lisiwekwe mabano, mwanafunzi asipojua tendo (operation) gani linatangulia kulingana na order of operation lazima atakosa hata akipewa calculator.

Mfano anaweza kuulizwa aonyeshe hatua gani zilifanyika ndani ya calculator kupata jibu fulani kwa kuzingatia kanuni za magazijuto (BODMAS).

Labda utuambie wewe umeona hayo maswali ya mtihani kutetea hii hoja/tuhuma zako?
 
ISLETS
Wewe jamaa una matatizo ya kuexaggerate vitu, tatizo unakaa unafikiria alafu unakuja na conclusion zako unataka dunia nzima tufuate, huna research yoyote kuprove wala nini, sio kila unachofikiri kuwa sahihi ni sahihi, tunaenda na data, hakuna mtu atakaa kuja kusema hesabu za kujumlisha haziwezekani kwa kichwa sababu tu wamempa calculator.

Anyway hii ndio message ya mwisho naongelea hili suala because nimeshaona limit ya akili yako, sina muda wa kupoteza kudiscuss hili suala tena, my last advice to you, jaribu kufungua akili sio umekaa unajifunga kwenye your little bubble ukafikiri ndio mwisho wa kila kitu.
 
Hata kama ukipewa laptop kama hesabu hujui hujui tu, calculator haishushi majibu ambayo huyajui inakurahisishia tu kile unachojua.
 
Hata hivyo wameruhusiwa kitumia calculator za kawaida za kuuzia madukani na siyo scientific!!!
 
Viva JF

Nikiwa sijui kinachoendelea kwenye kwenye mitihani ya kidato cha nne iliyoanza hii wiki, nikawa nawasiliana na dogo mmoja finalist ananiambia wametangaziwa kuruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na calculator hivyo wamefurahi sana.

Nilijikuta nashangaa na kuchukia ghafla, kwamba watu wazima wanaosimamia Wizara na NECTA wamefikiria nini kuruhusu hili?

Hivi ni kweli nchi nzima Form Four sasa ndio wanaanza kutumia calculator? Ni kama bado siamini.

Hivi ndio ufaulu utaongezeka au ni kuwafanya tu wanafunzi sasa waache kujibidisha?

Hizo calculators watakuwa wanazikagua au ndio bora yoyote, maana kuna scientific one zinatunza mpaka data, nyingine zinaonesha mpaka njia (solution) and many other operations.

Kuna faida gani kuwa na vijana wengi walio na vyeti vizuri mtaani wakati uwezo wao kiakili ku-solve mambo ni mdogo? Maana hizi devices zinadumaza akili hasa kwa vijana wadogo kama Form 4.

Kadri miaka inavyozidi kwenda, mfumo wa elimu nchini unazidi kuwa mbovu na rahisi kwa watoto kufaulu. Walianza na lile la multiple choices kwenye hesabu wakaona haitoshi sasa ni mteremko tu, sielewe lengo ni nini hasa kama sio kuandaa taifa la wavivu kufanya kazi na wavivu kufikiri.

God Bless America


Hoja haina mashiko, tena kwa taarifa yako tumechelewa mno kuanza kutumia calculators.

Mfano, unakuta swali ambalo outcome yake ni kama hivi; 36789× 234, hapo kwanini usitumie calculator kuokoa muda??!!, hizi sio zama za slide rule na four figure, mambo yamekuwa rahisi, mambo ya SGR na Rapid transport.
 
Sio kwel maana hata katika mtihani huu wa mwaka jana instructions zilisema kuingia na calculator ila kwa shule zingne walizuiliwa

@Walteronthechair
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom