Kichefuchefu cha CUF/Prof. Lipumba Jangwani leo

Hon.MP

Senior Member
Jul 15, 2012
153
86
Mchano juu ya Mkutano wa CUF & Speech Prof. Lipumba

1.Mkutano wa CUF leo Jangwani ulihudhuriawa na watu wengi na Prof. Lipumba alitoa hotuba.

2. Makamu wa Mwenyekiti CUF alisema kuwa kwa vile CCM & CHADEMA wanasema kuwa CUF ni chama cha Waislam basi Waislam wote Tanzania jiungeni na CUF. Pamoja na kwamba usemi huu unaweza kuwa ulitolewa as sarcasm hauna mashiko kwani ingetosha kusema nyote Wakristo kwa Waislam mnakaribishwa CUF. Kiongozi kakosa hekima kwa ku- reinforce kinatuhumiwa. Hii ni kama vile mtu aseme "kwa vile huwa nasingiziwa kuwa natembea na mke wa Fulani, sasa nasema nafanya kweli, Mrs. Fulani tuonane!

3. Prof. Lipumba kaongea issue za maana za kumpunguzia umaskini Mtz lakini ukweli hajatumia fursa ya sasa ya mabadiliko ya Katiba katika kuhamasisha wanachama chake juu ya mambo mengi muhimu yatakayo leta mabadiliko. Kaongea moja tu kuhusu kuwepo kipengelele kinachotamka Wananchi kufaidika moja kwa moja na rasilimali za nchi. Aidha haitoshi kuiombea roho ya marehemu Mwandishi wa habari na kisha mwishoni unamaliza kwa kusema tu kuwa Polisi mmeona sisi CUF tunapokutana hatuna fujo na tunakwenda Arusha kupeleka sera sio fujo / magomvi wala matusi.

Hii kauli imeshusha shule yake babu kubwa ya Uprofesa wa kweli katika uchumi aliyokuwa ameitoa katika kunyanyua uchumi wa nchi maana by implication alikuwa anasema tafuatayo: " SISI CUF SI KAMA CHADEMA WALETA FUJO WANAOSABABISHA POLISI KUTUMIA NGUVU HADI MAUAJI"

Mark my words!

Nimalizie kwa kusema kuwa VYAMA VYA UPINZANI VINAPOPATA NAFASI MBELE YA WANANCHI NA WAKAJIKITA KATIKA KUPIGANA VIJEMBE WAO KWA WAO, hakika mimi binafsi siwachukulii serious, ni kichefuchefu na mnaonekana vichekesho. Na ukweli ni kwamba unless mkubali kuunganisha nguvu au Katiba ibadilike na kukataa a simple majority Government; CCM itaendelea kuwatawala kwa muda mrefu ujao.
​Historia inabainisha kuwa ukombozi wa Taifa letu ulianzia Dar-es-salaam na ukamalizikia Dar-es-salaam

Mitandao na maongezi ya watu mitaani yalikuwa yanabainisha na kututaka tuamini kuwa CUF haiko tena hai Tanzania bara.

Mkutano wa leo Jang'wani umetoa kitendawili kipya katika jamii na hasa watu wanaofuatilia siasa za Tanzania. katika hali ya kawaida kwa sasa ni vigumu kukitengua.

Ninadiriki kusema, wafuasi na wapenzi wengi wa vyama vingine vya kisiasa hasa CHADEMA kabla ya mkutano wa leo jang'wani waliamini kama CUF haiko tena Tanzania bara. Mkutano wa leo umewapa taswira mpya na wengi wao mpaka muda huu hawaamini wanachokiona katika television na picha mpaka wanadiriki kusema picha zimechakachuliwa.


Marumbano kwa sasa ni kati ya wapenzi na wanachama wa CUF na CHADEMA kutaka kuiaminisha jamii kipi ni chama chenye wafuasi wengi nchini.

CCM wanafurahia sana haya marumbano na ninaamini wanapenda yaendelee milele kwa vile kwao ni mtaji wa kisiasa. Kwa sasa wako kimya wakiangalia kwa mbali.

Waswahili walisema, vita vya panzi, furaha ya Kunguru na siasa za Tanzania siyo kama tuzijuavyo.

Kwa watu tusiowapenzi na wafuasi wa chama chochote cha kisiasa Tanzania tunazifurahia changamoto kama hizi kwa sababu ni kichocheo chanya cha maendeleo nchini.

Haya ni maoni yangu.
Leo Profesa katamka vitu sikutegemea kabisa, hizo ni kauli za watu kama Mtatiro, Kambaya na wengine. Hivi anaamini kabisa kwamba CDM, na siyo polisi ndiyo husababisha vifo kwenye mikutano? Au hii anasema kwa CDM tu na si chama chake?

Anasahau kijiji cha Shumba Mjini huko Zanzibar mwaka 1993 wakati polisi walipomuuwa mwanaCUF aliyekuwa akipandisha bendera ya chama chake katika ufunguzi wa tawi?

Anasahau January 2001 pale makumi ya wanaCUF walipouawa na risasi za polisi huko Pemba katika maandamano ya amani?

Kufuatana na kauli ya Prof leo -- ina maana matukio hayo yote mawili yalitokana na CUF kufanya fujo?

Anasahau alivyovunjwa mkono na polisi wakati anaresist kukamatwa katika kampeni za mwaka 2000? Bahati hakukutokea maafa, lakini ni CUF ndiyo walifanya fujo?

Inakuwaje leo hii Profesa anawaona polisi hawana hatia wakati vifo vinatokea mikutanoni, hatia ni vyama?

Nilikuwa naona kwamba Prof ni only a reasonable person amebakia katika CUF, kumbe sasa nina mashaka sana, naye ameanza kusombwa na siasa za kihovyo hovyo tu.
 
Nakuunga mkono 100%. The Prof is tired. By the way will he run in 2015?


Ni wakati wa kumwacha hata mwingine ajaribu. Anafaa sana kuwa Waziri wa Uchumi au Mshauri wa rais katika uchumi lakini kuwa Rais I have my doubts!
 
He's been trying for four times and being bitten,naona hakutumia busara kusema kuwa CDM ni wa fujo huyu haelewi.source ya fujo ni nini.
Binafsi najua source ya fujo kwenye mikutano ya CDM ni Viongozi wa serikali ambao hutoa amri kuvunjwa kwa mikutano,kuanza kurusha mabomu
 
Nimemsikia huyo Naibu ya M'Kiti wa CUF akitamka hayo Jangwani leo, sikuamini masikio yangu!! kama ni utani, basi huu umewaharibia sana CUF maana sijui watayacontrol vipi magazeti etc watakavyoripoti.

Mkutano ulikuwa mzuri umeharibiwa na kuropoka hovyo!
 
ndo malengo ya cuf........... Kwenye hili propaganda za ccm za cuf chama cha udini nakubaliana nao, hukumbuki hata kwenye uchaguz znz jussa alisema walishindwa kwa sababu ya wakristu wengi kwenye hilo jimbo?

Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia.....
 
Wakuu naona CUF leo wamenzindua operation wanayoiita MCHAKAMCHAKA MPAKA IKULU 2015. Hii imekaaje na mnadadavuaje kuzinduliwa kwa operation hii hasa wakati huu ambapo M4C inatafutiwa kila sababu ya kuzuiwa kuendelea kwa nguvu zote na matokeo yake ndo hayo ambayo tunayashuhudia ikiwemo kifo cha kikatili kabisa cha mwandishi wa habari.


Hebu tulijadili hili kwa mapana wana JF!
 
.............. Hoja zake za UISLAMU na CUF hazikumzuia kuanguka mara 4 kwenye kugombea Uraisi, bado anazirudia tena?!!
 
Balaghashia ndo zilopigania uhuru nchi hii massaun hajakosea kwa sbb wapigania uhuru wa nchi hii wengi walikua waislam ni jambo la kawayda waislam ndo wamepigania uhuru sasa hv mnawaona wajnga? wapigania uhuru kama 1-Abdulwahid sykes 2-Dosa Aziz 3-Suleiman Takadir 4-Hassan bin amir 5-Jumbe Tambaza 6-Hamza mwapachu 7-Zubeir mtemvu hao ndo waasis wa TAA hayumo baba yenu...
 
Prof Lipumba amesema katibu wake amefuata nini Marekani?
 
Hii operesheni inaonekana kuwa ni mbinu mahususi ya CCM. Kwanza sio desturi kwa TBC kurusha live mikutano ya wapinzani !!!
 
3. Prof. Lipumba kaongea issue za maana za kumpunguzia umaskini Mtz lakini ukweli hajatumia fursa ya sasa ya mabadiliko ya Katiba katika kuhamasisha wanachama chake juu ya mambo mengi muhimu yatakayo leta mabadiliko.

We hujasikia kuwa jaji warioba amepiga marufuku viongozi wa vyama vya siasa kuinfluence maoni ya wanachama wao?
 
Wewe jamaa naona unalialia bila hoja umegeuka mshauri wa vyama vya siasa, washauri Chadema kwa nini wamejichaguwa wenyewe bungeni kama wanajuwa kuwa kuna wapinzani wengine kwa nini wamejitenga, hivi ni vita kila chama kinakuja na njia yake, wewe unataka CUF, NCCR Mageuzi, UDP, waisifie Chadema, wakati hao hao Chadema wanasema Tanzania hakuna chama cha upinzani zaidi ya Chadema tu...endelea na kichefuchefu chako mkuu.
 
Back
Top Bottom