Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
​Historia inabainisha kuwa ukombozi wa Taifa letu ulianzia Dar-es-salaam na ukamalizikia Dar-es-salaam
Mitandao na maongezi ya watu mitaani yalikuwa yanabainisha na kututaka tuamini kuwa CUF haiko tena hai Tanzania bara.
Mkutano wa leo Jang'wani umetoa kitendawili kipya katika jamii na hasa watu wanaofuatilia siasa za Tanzania. katika hali ya kawaida kwa sasa ni vigumu kukitengua.
Ninadiriki kusema, wafuasi na wapenzi wengi wa vyama vingine vya kisiasa hasa CHADEMA kabla ya mkutano wa leo jang'wani waliamini kama CUF haiko tena Tanzania bara. Mkutano wa leo umewapa taswira mpya na wengi wao mpaka muda huu hawaamini wanachokiona katika television na picha mpaka wanadiriki kusema picha zimechakachuliwa.
Marumbano kwa sasa ni kati ya wapenzi na wanachama wa CUF na CHADEMA kutaka kuiaminisha jamii kipi ni chama chenye wafuasi wengi nchini.
CCM wanafurahia sana haya marumbano na ninaamini wanapenda yaendelee milele kwa vile kwao ni mtaji wa kisiasa. Kwa sasa wako kimya wakiangalia kwa mbali.
Waswahili walisema, vita vya panzi, furaha ya Kunguru na siasa za Tanzania siyo kama tuzijuavyo.
Kwa watu tusiowapenzi na wafuasi wa chama chochote cha kisiasa Tanzania tunazifurahia changamoto kama hizi kwa sababu ni kichocheo chanya cha maendeleo nchini.
Haya ni maoni yangu.