Kichefuchefu cha CUF/Prof. Lipumba Jangwani leo

Leo Profesa katamka vitu sikutegemea kabisa, hizo ni kauli za watu kama Mtatiro, Kambaya na wengine. Hivi anaamini kabisa kwamba CDM, na siyo polisi ndiyo husababisha vifo kwenye mikutano? Au hii anasema kwa CDM tu na si chama chake?

Anasahau kijiji cha Shumba Mjini huko Zanzibar mwaka 1993 wakati polisi walipomuuwa mwanaCUF aliyekuwa akipandisha bendera ya chama chake katika ufunguzi wa tawi?

Anasahau January 2001 pale makumi ya wanaCUF walipouawa na risasi za polisi huko Pemba katika maandamano ya amani?

Kufuatana na kauli ya Prof leo -- ina maana matukio hayo yote mawili yalitokana na CUF kufanya fujo?

Anasahau alivyovunjwa mkono na polisi wakati anaresist kukamatwa katika kampeni za mwaka 2000? Bahati hakukutokea maafa, lakini ni CUF ndiyo walifanya fujo?

Inakuwaje leo hii Profesa anawaona polisi hawana hatia wakati vifo vinatokea mikutanoni, hatia ni vyama?

Nilikuwa naona kwamba Prof ni only a reasonable person amebakia katika CUF, kumbe sasa nina mashaka sana, naye ameanza kusombwa na siasa za kihovyo hovyo tu.

Mbona unajiuliza maswali yenye majibu. Kwani ujui kuwa cuf ni ccm B, Na leo wengi ni magwanda wamevaa majoho za cuf ili kuwadanganya watanganyika.
 
Kwa yeyote aliutazama mkutano wa CUF, na kusikia hotuba za viongozi wa CUF, atakubaliana nami kwamba CUF ina ombwe kubwa la viongozi weledi wa siasa za sasa bila ya Ibrahim Lipumba! Ibrahim Lipumba alizungumzia vema matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya watanzania na alijaribu kweli kweli kutoa dira! Ila viongozi wengine wote (ila labda Mtatiro) wamebaki kwenye siasa za chuki na udini! Lipumba anapoteza ueledi wake wa siasa za kiuchumi CUF!
 
Bado mambo siyo shwari ndani ya CUF ukiangalia walivyokuwa wanajenga hoja bado kuna kazi kubwa, nakubaliana nawe mti mmoja hata uwe mkubwa vipi haufanyi msitu!
 
Kwa yeyote aliutazama mkutano wa CUF, na kusikia hotuba za viongozi wa CUF, atakubaliana nami kwamba CUF ina ombwe kubwa la viongozi weledi wa siasa za sasa bila ya Ibrahim Lipumba! Ibrahim Lipumba alizungumzia vema matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya watanzania na alijaribu kweli kweli kutoa dira! Ila viongozi wengine wote (ila labda Mtatiro) wamebaki kwenye siasa za chuki na udini! Lipumba anapoteza ueledi wake wa siasa za kiuchumi CUF!
Ipo siku huko huko itaota miti mingine. Kwani CDM mwenyekiti wao si alikuwa mvaa heleni? lakini haukuwa mti bahati nzuri ikaja kuota miti mingine ambayo imefanya CDM kuwa msitu wa kutumainiwa.
 
He's been trying for four times and being bitten,naona hakutumia busara kusema kuwa CDM ni wa fujo huyu haelewi.source ya fujo ni nini.
Binafsi najua source ya fujo kwenye mikutano ya CDM ni Viongozi wa serikali ambao hutoa amri kuvunjwa kwa mikutano,kuanza kurusha mabomu

Ni kama maigizo vile. Ni hivi karibuni wakimbizi wa Zanzibar wamerudi tangu walipokimbia mwaka 2000. Inamaana tumekuwa ni wepesi wa kusahau?
Mwaka 2008 wakati wa kampeni Kenya kiongozi wetu alisema kwa nini uwe na wasiwasi wakati wewe "Kibaki" umeshikilia dola! Nilichojufunza ni kwamba kwa Africa chama kilichopo madarakani kina haki kutumia mbinu zozote zile ili kiendelee kutawala.
 
Kwa yeyote aliutazama mkutano wa CUF, na kusikia hotuba za viongozi wa CUF, atakubaliana nami kwamba CUF ina ombwe kubwa la viongozi weledi wa siasa za sasa bila ya Ibrahim Lipumba! Ibrahim Lipumba alizungumzia vema matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya watanzania na alijaribu kweli kweli kutoa dira! Ila viongozi wengine wote (ila labda Mtatiro) wamebaki kwenye siasa za chuki na udini! Lipumba anapoteza ueledi wake wa siasa za kiuchumi CUF!

Dada Zed, huo uchumi anaoufahamu lipumba si ungejidhihirisha zanzibar ambako cuf inatawala huku yeye akiwa mwenyekiti wa chama tawala?
Lipumba zilongwa mbali zitendwa mbali.
Mnapoteza muda kwa lipumba, mpeni usheikh mkuu wa tanzania.
 
Last edited by a moderator:
cuf na chadema can you guyz give us a break in that kind of politics ur doing?cum on guyz we don't need to hear that,we need to know your plans na kwanini mnadhani nyie mtakua borakwetu kuliko ccm,thats it.
 
Hasemi hayo kwa bahati mbaya,baada ya mwenzake kuukwa umakamu wa Rais yeye ameahidiwa kuwa mgombea mwenza wa CCM 2015. CCM dhaifu +CUF hovyo=dhaifuhovyo
 
Wote mmeona leo udini waziwazi, na ubaguzi wa kauli zinazoelekea kusukwa na watawala wa nchi hii. JK hajajifunza bado kuwa udini haujawahi kuwa suluhisho la utawala mahala popote duniani. Kuibuka kwa vyama na ndoa ya mkeka ya CCM na kipenzi CUF itaishia kwa Lipumba kuwa mshindi wa nane uchaguzi wa 2015. Vidumu Vyama Vizuri!

VIDUMU!
 
Mjengwablog Itaripoti Live Mkutano Wa CUF Jangwani



Julius Mtatiro
Leo kwenye viwanja vya jangwani,Dar es salaam


CUF Buguruni Hakuna Mtu, Majeshi Yameelekezwa Jangwani



Walinzi wa CUF wakielekea jangwani
Nimepitia ofisi za CUF makao makuu,tayari viongozi wameenda Jangwani.Punde zitawajia taswira moja kwa moja toka viwanja vya jangwani
[h=3]Mchakamchaka Mpaka Ikulu 2015

Bwana Katani Ahmadi,mwenyekiti wa vijana wa CUF akisoma risala ya vijana kwa mwenyekiti
CUF Yaifunika CHADEMA Na CCM Jangwani

[/h]

[h=3]Kuna Waliorejesha Kadi Pia[/h]

Julius Mtatiro

h





 
Walianza na maandamano makubwa Ijumaa na leo wamehitisha Jangwani............

tuvyama twingine bana!
 
Ni wakati wa kumwacha hata mwingine ajaribu. Anafaa sana kuwa Waziri wa Uchumi au Mshauri wa rais katika uchumi lakini kuwa Rais I have my doubts!
Mie naona bora tuwaache wote waliowahi kugombea nafasi ya uraisi miaka yote ya nyuma. Hivi hakuna watu wengine katika vyama wenye sifa za kugombea? Kurudiarudia sio siri wanatuboa. Nahisi ndiyo inawafanya wajihisi kama nafasi ya uraisi na vyama ni mali yao
 
Balaghashia ndo zilopigania uhuru nchi hii massaun hajakosea kwa sbb wapigania uhuru wa nchi hii wengi walikua waislam ni jambo la kawayda waislam ndo wamepigania uhuru sasa hv mnawaona wajnga? wapigania uhuru kama 1-Abdulwahid sykes 2-Dosa Aziz 3-Suleiman Takadir 4-Hassan bin amir 5-Jumbe Tambaza 6-Hamza mwapachu 7-Zubeir mtemvu hao ndo waasis wa TAA hayumo baba yenu...
uelewa wako ni wa kiwango cha chini kabisa,soma kijana,achana na stori za vijiwe vya kahawa!
 
Sio siri Prof.Lipumba ndie amekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha cuf kwa kila chaguzi kuu zinapofanyika.Kinachoshangaza ni kwani huyu msomi hapati kura za kutosha ?

Wapiga kura wanataka viongozi wa aina ipi?
Kama una jibu basi ndio tunaishia kuchagua "chaguo la mungu" na mambo yetu yanakwenda "kimungu mungu".

Siku tukiona / tukiamua tunataka mtu msomi wa kada ya Atta Mills tutachagua mtu wa aina hiyo.

Mungu ibariki Tz na uwabariki na watu wake!
 
Back
Top Bottom