Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Kibosile wa TBC1 leo asubuhi alikuwa na wakati mgumu wa kutetea utafiti wao ambao alidai ni wa kitalaamu lakini alishindwa kujibu hoja za kimsingi kutoka kwa mwanahabarishaji wa TBC1 Bw. Gabriel Zacharia.
katika uchunguzi wangu, maeneo yafuatayo si REDET au SYNOVATE ambao wanaweza kutupa majibu ya kuridhisha na hivyo kufanya tafiti zao kutokuwa na sifa za kuitwa za kisayansi:-
1) Vigezo walivyovitumia katika kuchagua ukubwa wa sampuli na majumuisho ya kimatabaka ya jamii ya sampuli hiyo ya utafiti wao hasa ukizingatia tafiti zao hawazifanyi kila wiki kama nchi zilizoendelea. Vile vile ifahamike hakuna takwimu za kuyabainisha makundi ya kijamii yalivyogawanyika kimapato, kitikadi n.k zaidi ya kutegemea taarifa za wahojiwa ambazo zaweza kuwa ni za kweli au la na hakuna namna ya kuzikagua.
2) Kwa nini wao na REDET wanatofautiana sana katika matokeo ya tafiti zao. Hoja za matumizi ya mitaala tofauti haina mashiko kwa sababu lengo la utafiti ni kuweza kuibua hisia za jamii kwa wakati ule. Haiwezekani vyombo viwili tofauti vikatofautiana kiasi hicho katika kubainisha hisia za jamii ileile. Haya ni matokeo ya kupika matokeo tu ndiyo yanaweza kuleta taswira ya tofauti hizo juu ya hisia za jamii ileile.
3) Wilaya zipo zaidi ya 110 hivi sampuli ya watu elfu mbili hivi, si yamaanisha chini ya watu ishirini kila wilaya. Utawapataje na kwa vigezo vipi ili kuhakikisha kila wilaya au jimbo la uchaguzi hisia zake zimewakilishwa ipasavyo na idadi ndogo hiyo ya watu hasa kwenye jamii yetu isiyo na utamaduni wa kuweka na kutunza rekodi za wanajamii?
4) Kwa nini jamii inaonyesha kutoridhika na tafiti hizi mbili hasa ukizingatia ya kuwa SYNOVATE iliahidi kufanya utafiti kabla ya uchaguzi lakini baada ye REDET kuandamwa na jamii SYNOVATE wakatoa matokeo ya utafiti ambao kulingana na kauli zao wenyewe za SYNOVATE ni kwamba yaekea matokeo ya utafiti wao waliutoa kwenye droo ya meza na wala siyo kutoka kwenye jamii. Haiwezekani baada ya wiki moja tu baada ya Chadema kuwalalamikia na wao SYNOVATE kuahidi kufanya utafiti huo siku chache kabla ya uchaguzi halafu wiki inayofuata tayari wawe na matokeo mezani. Ni dhahiri huu tafiti hiyo ni wa kupika tu