Kibonzo cha Kipanya leo kina ujumbe gani?

Mbona maana iko wazi tuu:

1. Hiko ni chumba cha mtu (nchi). Chumba tayari kilikuwa kimepakwa rangi ya bluu. Lkn CCM & CDM wanafosi kupaka upya rangi zao wenyewe (kijani & nyekundu), na kwa kuwa hawana maelewano basi wanajikuta wanachafua ukuta tuu maana hapa rangi ya kijani, mara pale ya nyekundu, kule kijani basi ni vululuvululu tupuu.

2. CCM na CDM wote wanatumia kitanda kimoja (Tanzania) lakini wanakichafua kwa kupaka rangi zao.

3. Shuka lina rangi ya CCM, mto una rangi ya CDM. Kama CCM ni shuka, basi CDM ni mto. Lkn tukumbuke kitanda huwezi kukilalia bila shuka na mto.

4. Wenye chumba/kitanda (wananchi) nao hawana vichwa wapo wapo tuu hivyo hawana la kufanya zaidi ya kuangalia chumba chao kikichafuliwa ovyo.
Unforgetable
Madini yako nmeyaelewa
 
Nilichoelewa hapo huyo msela hapo ni Magu, amejaribu kuifanya Tanzania yote ionekane ni CCM kwa miaka mitano ili wakati wa uchaguzi atulie tu lakini bado imeshindikana, na sasa wapinzani wanazidi kumnyima usingizi. Amechoka kufanya kazi na akijaribu kulala usingizi hapati kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom