Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?


Swadakta!
 
Perception. Kama 2million mtu unaona ni nyingi utaona mtu ana hadhi.Nilionaga picha Dangote kashika simu ya "kichovu"..sasa sijui na yy akiona mtu ana iphone atamwona ana hadhi..
 
Iphone ni aina ya simu zinazoitwa Highend smartphones. Kawaida company yao hawatoi simu za lower end. Mfano Huwezi kuta iphone inauzwa elfu themanini, laki moja, laki 2, tatu ama tano..

Hivyo kulingana na Bei zake hufanya wateja wao worldwide ni watu matajiri watako zi afford. Kwa mujibu za takwimu za Bloomberg mwaka jana iphone users ndio matajiri duniani. Ukilinganisha na watumkaji wa simu za aina nyingine.

Ukilinganisha na brands zingine duniani kama Samsung ya Korea ,na Huwawei inayo dominate soko la China nk. ambapo wanatoa simu za kuanzia lowend mpaka high end.

Tecno wako kwenye category ya Lowend smartphones.
Zingine ni Xtigi, Zero, Itel , Infinix, simu hizi ni kwa ujumla hazipokei Update za maboresho ya operating systems zao. Ukishanunua Rununu unaitumia mpaka unaitupa, unakua haujawahi kupokea update yoyote.

Ukitaka kupata Android 8 aureo utalazimika kununua simu mpya.

Pia simu hizi zinatumia mediatek chipset ambayo inapata joto haraka. Na kuifanya simu ichemke.
Pia zinakua sandwiched na core mbalimbaki kama octacore, dual core., Mali chipset. Nk.chipset ambazo ni dhaifu kwa ujumla.
 
WANATAKA IPHONE HALAFU KUITUMIA HAWAJUI.

IPHONE WATUMIAJI NI WACHACHE KWA NCH ZA KIAFRIKA. MFN TZ, UNAWEZA KWENDA WILAYA NZIMA IPHONE UKAZIKUTA MBILI AU 3

ILA TECNO HADI MTOTO WA SHULE ANAYO

Samsung zimezagaa kama nywele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…