Sauti ya mtu aliaye nyikani, itengenezen njia ya Bwana , yanyoshen mapito yake..,
Niseme, tumefika mahali kanisa linaacha njia na sasa hatari inaingia ya kuchanganya dini na siasa. Inashangaza sana kuona dhehebu linajikita kuanza kuandika nyaraka kwa mamlaka zingine badala ya kuwaelekeza waumini waingie magotini katika maombi kuombea viongozi wa serkali yetu 1Tim 2 ;1-4. Kiongozi wa kanisa mkuu Yesu Kristo alisema ya Kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu.
Hapo zamani ilipoonekana pia kanisa lilijichanganya na mambo ya dunia tunasoma likaonywa ’ Ni Heri kuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu Ufu 3 :14-19 , mtasitasita katika njia mbili hadi lini? Mkitaka kufanya siasa vueni majoho yenu ungana na vyama vya siasa ijulikane moja, kama ni dini bac ijulikane mnatumikia dini zenu. Nasema dini zenu maana mkisema mnasimama badala ya watumish wa Mungu basi mmekua watumishi waliojikinai, kumbukeni huyo mnayemsonta na nyaraka zenu naye ni mtumish wa Mungu mwenzenu ! utaniambia kivipi ? Hebu someni Warumi 13 ;1..kila mtu aitii mamlaka iliyo kuu..maana iliyopo imeamuriwa na Mungu,….hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu, nao washindanao watajipatia hukumu, …..13 ;6 kwa kuwa yeye (JPM) ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema, ufanyapo mabaya ogopa maana hauchukui upanga bure, kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu’…
Watumish maaskofu wetu mbona mmejikinai hivi badala ya kujivika roho ya unyenyekevu , mnaandika nyaraka zisizo na tija rohoni ! mnajihesabia haki ninyi ? Luka 18 ;9-14? Ole imewajia maana ninyi si tofauti na mafarisayo ambao Yesu aliwaonya na kuwakemea sana ingawa wao walijiona wako sawa. Hata sasa mwasema hatutishiki wala kunyamazishwa! Ole inakuja ! Kumbukeni !
· Askofu ni kazi ya Kutaka (kuomba) na kuchaguliwa, na sio ya kuitwa na Mungu kwa mujibu wa maandiko,?1Tim 3 ;1 Mtu akitaka kazi ya uaskofu..(lakini kazi za kuitwa na Mungu zimeainishwa ktk Efeso 4 ;11-12 yaani Nabii, Mtume, Mwinjilist, Mchungaji na Mwalimu , hawa ndio wenye kulijenga kanisa. Sasa ninyi mnabadili maandiko na kuifanya kazi yenu hiyo kuwa wasemaji wa Mungu badala ya Manabii na Mitume wenye kazi hiyo ambao ndio wajenzi wa kanisa?
· Majukumu ya askofu ni kutekeleza yale yote yaliyoainishwa katika wadhifa wake kulingana na katiba ya dhehebu husika . ambapo madhehebu yote yamesajiliwa chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi yetu kwa mujibu wa katiba ya JMT
· Ni matarajio ya wengi kuwa nyingi ya katiba hizo zina lengo la kumhubiri Kristo kwa kuishi maisha ya utauwa na kukemea maovu bila kujali yanatendwa na mtu wa namna gani ukijianzia mwenyewe
· Je hamjui kuwa JPM pia ni mtumishi wa Mungu kama ninyi ‘Rum13 ;6, kwa kuwa yeye (JPM) ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema,’ tena yeye mwangalizi mkuu yaani askofu wa nchi kwa upande mwingine ? na madhehebu yote yako chini yake maana ameyasajiri na anaweza kuyafuta yasipofuata taratibu zilizokubalika hadi kusajiliwa?. Ingawa Kanisa halisi la rohoni halionekani na haliwez kufutwa maana ni mwili wa Kristo !
NASHAURI
· Vita vyenu sio vya damu na nyama ili kupambana kwa mwili Efeso 6 ;10, bali ni ya Roho katika uliwengu wa Roho. Ukiona kanisa linapigania kuandika Waraka na kutoa matamko jua limeacha njia …uuuuh bali jua tuna dhehebu linalopigania maslahi fulani likiwa na limejivika ngozi ya kanisa kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali wasiolihurumia Taifa. Ikiwa watu wa dunia kama vyama, mashirika wanatoa matamko je kanisa nalo litoe tamko ? huko ni kufilisika kiroho.
· Kanisa sio dhehebu kama wengi wanavyodhani bali KANISA ni mwili wa Kristo, haliandikishwi, wala halifi, lina mamlaka ya kufunga na kufungua chochote duniani ktk ulimwengu wa roho na lina sura ya Kristo ndani. Ebr 5 ;7 Yeye kristo hakuandika waraka bali alinyenyekea kama kielelezo. Mkiacha njia kristo ananyanyua hata mawe yamtumikie, hivyo msijimilikishe kuwa dhehebu ndio kanisa, kristo awajua walio wake ndo maana asema sio wote wasemao Bwana Bwana wataurith ufalme bali wale wayatendao mapenzi yake yeye tu.
· KANISA linapaswa limwombe Mungu sio kutoa nyaraka, huko ni kujitetea kama dunia na ni kutoka nje ya njia. Ebr 5;7-9, 1Tim 2 ;1-3, ‘Basi kabla ya mambo yote nataka Dua, na sala, na maombezi, na Shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme,na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na Ustahivu’ hilo lapendeza tena ni zuri’ lakini pia ni vema kumuuliza Mungu kujua mapenzi halisi yake ni nini maana angalia unaweza kuwa unaingia katika maombi ya kushindana na mapenzi ya Mungu pia.
· Tujiulize ikiwa sisi ni watumishi wa Mungu na mamlaka iliyoko madarakan ni watumish wa Mungu, je Mungu amsikie nani na amwache nani ? lakini ikiwa kinachotendeka ni maovu basi Bwana atafanya njia. Ukisoma Mdo 12 ;1-10 wakati ule Herode alipomkamata Petro apate kumwua, maandiko yanasema Kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi na Mungu akalisikia, angalia akafanya njia kumtuma malaika na kumtoa Petro katika gereza, sio kulalamika.
Kwa msingi huu, mtumish mwenzenu JPM yuko sawa kuwasahihisha kwa kuwaambia, ikiwa mmeshindwa kuhubiri na kufanya yale mliyoagizwa kufanya, basi anzeni kuhubiri viwanda ! Kwa maana yeye kapewa kujenga viwanda anajua wajibu wake, mkitaka kumsaidia hubirini viwanda.
Hivi hamuoni kuwa kanisa lina hali mbaya ya kiroho ? hakuna injili ya kweli bali injili ya tena bali kuchuma kwa ajili matumbo tu ! Angalieni jinsi manabii wanavyowaibia watu mali na pesa wazi wazi kwa hila mnawaangalia tu, wanafunzi kila kukicha mimba mashuleni hadi aibu mnaangalia tu, ndoa za jinsia moja kanisani uchafu gani huo ? maadili hakuna kuanzia maaskofu wenyewe wachungaji na mapadiri, kwani ni siri wengine wamefungwa hadi gerezani? watoto lukuki mitaani wamezaliwa na hao wanaitwa watumish ? aibu ! ugomvi makanisani mpaka kushitakiana mahakamani je hayapo ? ufisadi ndani ya maeneo yenu je mmemaliza ? mbaya zaidi kugombea cheo hicho cha uaskofu wengine wengi wenu mmeenda mpaka kwa Sangoma kwani ni siri ? au mpaka mtajwe ? kati yenu wengi je hamjahonga kupata cheo ? dunia imeingia makanisani kwa njia ya miziki na uimbaji wa kidunia hakuna makemeo, mahubiri ya uongo kwa wizi wa kujitajirisha nk lakini hatusikii neno la kukemea juu ya hayo ! kanisa mmelipeleka mwilini na sio rohoni 1Kor 3 ;1-3,ninyi mmekua wa Tabia ya mwilini na sio rohoni ! sikiliza ushauri wa Yesu ! . Luka 6;41-42 ” Basi mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako huiangalii ?..,Mnafiki wewe itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako”
Hata ninyi mna mapungufu mengi maana hamjakamilika, sasa iweje juu ya haya ?nadhani ni wakati wa kuona aibu na kujisahihisha,kutubu na kuirudia njia ya mwenyezi. Ati maaskofu wanaongelea katiba kwenye kwenye madhabahu ya Bwana !? kiroho kwishney
Hitimisho,
· Watanzania wamempa ridhaa JPM aongoze nchi, jiulize kama wewe ni dereva wa basi la abiria , wakati unaendesha kila mtu anakueleza la kwake ufanye je utafuata lipi ? mwingine anasema
o Simamama sioni kule uendako !
o Ongeza mwendo dereva, wakati huo huo mwingine anasema
o Punguza mwendo, mwingine anasema nimechoka nataka kupumzika simamisha gari, mwingine ahirisha safari mabonde mengi subiri lami mwakani ndo uendelee na safari. Kisha dereva anaamua asisikilize mtu yeyote je ninyi mliopo kwenye gari mtachukua hatua gani ? au mtachukua usukani mwendeshe au mtamshitaki kwenye mamlaka husikaaa? Kinachotakiwa jamani
§ Mwachen dereva ( JPM ) aendeshe maana aliomba kazi ya kutuendesha miaka mitano,
§ Kama hamridhiki na uendeshaji wa dereva piga simu Yer33;3 kwa mwenye gari atamsaidia yaani kwenye mamlaka husika nawe utasikiwa,lkn kubali majibu maana yaweza kuwa hapana au ndiyo au subiri.
§ Ama sivyo mkifika mwambien mwenye gari yeye atachukua hatua, stahiki. si ndio kusema ikiisha hiyo miaka yake mhukumuni kwenye sanduku la kura maana mtamshitaki kwa wananchi! sio oooh huyoo anavunja katiba mara ooh huyu eeh....nini hii rubish
§ au subirini kwenye interview nyingine kaombeni na ninyi muwe madereva si mnazo leseni????? Shida nn?
§ Kama hujui dereva aendako basi shuka kwenye gari kapande gari jingine ( kaishi huko nje kama huyo dada alivofanya na ukae kimya kale maisha hakuna atakayekusumbua) au kaangalie mbele ya kioo cha gari utakuta kimeandikwa hapa kazi tu, viwanda , maendeleo
§ Ikiwa mliwahi kutoa waraka wenye sifa za rais ajaye wa awamu hii, niwaulize je mtu huyo ndiye huyu au bado mnaye mnaemdhania ndiye? Kama ndiye basi mpeni ushirikiano sio malumbano, pia vilevile kama siye kwa mujibu wa maombi yenu bado kiongozi aliyewekwa na Mungu kwa mujibu wa maandiko anapaswa kuheshimiwa na ikiwa ni ushauri basi apewe kwa unyenyekevu wote.
§ Tutakushangaa saana ukiamua kutoboa tairi au kuharibu gari au kurukia usukani ili uendeshe kisa ati wote tusimame tusiendelee na safari kwa kuwa dereva hakusikilizi, hapo ndipo utakapoona hasira za tajiri na abiria wenzako wakisema we vipi? Namba za kuripoti unazijua, mamlaka zipo, sasa si ukaripoti ukiona kuwa kama katiba inavunjwa si uende Mahakamani ndipo haki ya kikatiba ilipoooo ! haya mambo ya nyaraka, maandamano yanatoka wapi?
Hawakawii kusema napigia debe kitu flan, mm si mwanachana wa chama chochote cha siasa, ni mtumish mwenzenu wa Jehova ila naunga mkono juhudi za mamlaka iliyoko madarakani kutuletea maendeleo. Tulihitaj kiongozi mwenye kuchukua hatua ndiye huyu tuliyepewa, Tumuombee Mungu aendelee kumpa hekima na maarifa. Kumbukeni Jambo lolote likiharibika ktk nchi, tatizo huwa ni kanisa kwani huwa limelala usingizi halioni ila nashukuru Mungu baadhi ya watumish wamefumbuliwa macho na wanaona kisawasawa hutawaona wakija na matamko bali maombi. Kumbukeni TB Joshua alipokuja wakati wa uchaguzi je aliwatolea matamko??? Lakini alikuja na ujumbe maalum kwa walengwa kimya kimya! jifunzeni basi kwa wengine. Tunamuombea saana Rais wetu mpendwa apewe neema atufikishe kwenye nchi ya asali na maziwa. Amina
Wasalam