Kibao cha Aziz Ally Mtoni na Historia Yake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,122
30,476
AZIZ ALLY MJENZI WA MISIKITI
Aziz Ally alipofariki mwaka wa 1951 muda mfupi baada ya.kutoka hijja gazeti la Tanganyika Standard katika kueleza kifo chake liliandika "Mjenzi wa Misikiti Amefariki."

Kabla hajajenga nyumba yake mashuhuri ya Mtoni leo panaitwa Mtoni kwa Aziz Ali, Azizi Ali alikuwa anaishi Gerezani Mtaa wa Congo na Mbaruku.
Haya hapo chini aliyafanya wakati akiishi Gerezani:

KUMBUKUMBU YA RAMADHANI 7: FUTARI KWA AZIZ ALI MTAA WA MBARUKU NA CONGO 1940s

Aziz Ali alikuwa tajiri na akaupamba utajiri wake kwa ukarimu.

Yeye alikuwa mjenzi wa majumba na alikuwa akimjengea mtu nyumba na akashindwa kumlipa alimpa muda alipe kwa taratibu.

Kwa wema wake huu watu wa Dar es Salaam wakampa jina la ''Aziz'' yaani ''Kipenzi.''

Lakabu hii ikaua jina lake la Ali Kidonyo akafahamika kwa jina la Aziz Ali.

Nyumbani kwake Mwezi wa Ramadhani kuanzia tarehe mosi hadi mwisho wa mfungo ikiingia magharibi watoto wake wa kiume Waziri (Dossa), Ramadhani na Hamza na watoto wa jirani walikuwa wanajumuika kufagia uwanja na kutandika majamvi kwa ajili ya watu watakokuja kufuturu barazani kwao.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Mbaruku na Congo jirani na nyumba ya babu yangu Salum Abdallah.

Miezi ya kawaida Aziz Ali nyumbani kwake ikiingia magharib mwanae Hamza alikuwa na kazi ya kuwasha karabai na kuzitawanya katika misikiti yote ya Kariakoo.

Baada ya sala ya Isha Hamza atazipitia karabai zote kuzirejesha nyumbani kwa matayarisho ya siku ya pili.

Hii ndiyo ilikuwa kazi yake Hamza Aziz na haya kanieleza mwenyewe kwa kinywa chake.

Miaka hiyo misikiti ya Kariakoo ilikuwa haina umeme.

Misikiti mingi ya Dar es Salaam ilijengwa na Aziz Ali na alipofariki Tanganyika Standard liliandika kwa wino uliokoza: ''Aziz Ali Mjenga Misikiti Amefariki.''

Aziz Ali alikataa kumpeleka mwanae mkubwa shule Dossa kuanza darasa la kwanza hadi kwanza aingie chuoni ahitimu mashafu.

Haya kanieleza mwenyewe Dossa nyumbani kwake Mlandizi mbele ya Ally Sykes.

Mzee Dossa anasema kwa ajili hii alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 14 na ndiyo sababu yeye kusoma darasa moja na Abbas Sykes ambae kwake alikuwa mdogo kwa umri.

Akanambia na ndiyo sababu ya urafiki wake na Abbas Sykes kuwa mkubwa kuliko urafiki aliokuwanao na kaka zake Abdulwahid na Ally.

Aziz Ally alijenga jumba la fahari la vioo na vigae Mtoni na sehemu ilipo nyumba yake hii inaitwa Mtoni kwa Aziz Ali hadi leo.

Kwa miaka ile hakuna Mwafrika alikuwa na nyumba kama ile.
Nyumba mfano wa hiyo zilikuwa Oyster Bay makazi ya Wazungu.

Aziz Ally barza yake kubwa ya maongezi ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu nyumbani kwa Kleist Sykes na ndipo lilipokuwa duka lake la vifaa vya ujenzi.

Hii ilikuwa barza maarufu ya wazee wa Dar es Salaam.
Barza hii ilififia baada ya kifo cha Kleist Sykes mwaka wa 1949.

Aziz Ali alikufa muda mfupi baada ya kutoka safari ya Hijja mwaka wa 1951.
Picha: Aziz Ali ujanani na uzeeni.

1715697126078.png

1715697055127.jpeg

1715696949056.jpeg

Naomba kufahamu hili gazeti lilimilikiwa na wakina nani na je hicho kichwa cha habari hakikuwa chenye dhihaka au udini ndani yake?
 
Mzee wangu Mohamed Said, nakushukuru sana kwa bandiko hili... Ila nina swali kidogo, Ule mtaa wa sasa Kwa Aziz Ali, una mahusiano gani na Ndugu huyu, Ali Kidonyo?
 
Angeja na shule pia maana kaacha jamii nyingine inakazana kusoma elimu ahera kuliko kusoma elimu dunia

Afu baadae wanalalamika propaganda za kipumbavu eti mfumo kristo mara sijui nyerere ....wakati wako busy kusoma elimu ahera tu
 
AZIZ ALLY MJENZI WA MISIKITI
Aziz Ally alipofariki mwaka wa 1951 muda mfupi baada ya.kutoka hijja gazeti la Tanganyika Standard katika kueleza kifo chake liliandika "Mjenzi wa Misikiti Amefariki."

Kabla hajajenga nyumba yake mashuhuri ya Mtoni leo panaitwa Mtoni kwa Aziz Ali, Azizi Ali alikuwa anaishi Gerezani Mtaa wa Congo na Mbaruku.
Haya hapo chini aliyafanya wakati akiishi Gerezani:

KUMBUKUMBU YA RAMADHANI 7: FUTARI KWA AZIZ ALI MTAA WA MBARUKU NA CONGO 1940s

Aziz Ali alikuwa tajiri na akaupamba utajiri wake kwa ukarimu.

Yeye alikuwa mjenzi wa majumba na alikuwa akimjengea mtu nyumba na akashindwa kumlipa alimpa muda alipe kwa taratibu.

Kwa wema wake huu watu wa Dar es Salaam wakampa jina la ''Aziz'' yaani ''Kipenzi.''

Lakabu hii ikaua jina lake la Ali Kidonyo akafahamika kwa jina la Aziz Ali.

Nyumbani kwake Mwezi wa Ramadhani kuanzia tarehe mosi hadi mwisho wa mfungo ikiingia magharibi watoto wake wa kiume Waziri (Dossa), Ramadhani na Hamza na watoto wa jirani walikuwa wanajumuika kufagia uwanja na kutandika majamvi kwa ajili ya watu watakokuja kufuturu barazani kwao.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Mbaruku na Congo jirani na nyumba ya babu yangu Salum Abdallah.

Miezi ya kawaida Aziz Ali nyumbani kwake ikiingia magharib mwanae Hamza alikuwa na kazi ya kuwasha karabai na kuzitawanya katika misikiti yote ya Kariakoo.

Baada ya sala ya Isha Hamza atazipitia karabai zote kuzirejesha nyumbani kwa matayarisho ya siku ya pili.

Hii ndiyo ilikuwa kazi yake Hamza Aziz na haya kanieleza mwenyewe kwa kinywa chake.

Miaka hiyo misikiti ya Kariakoo ilikuwa haina umeme.

Misikiti mingi ya Dar es Salaam ilijengwa na Aziz Ali na alipofariki Tanganyika Standard liliandika kwa wino uliokoza: ''Aziz Ali Mjenga Misikiti Amefariki.''

Aziz Ali alikataa kumpeleka mwanae mkubwa shule Dossa kuanza darasa la kwanza hadi kwanza aingie chuoni ahitimu mashafu.

Haya kanieleza mwenyewe Dossa nyumbani kwake Mlandizi mbele ya Ally Sykes.

Mzee Dossa anasema kwa ajili hii alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 14 na ndiyo sababu yeye kusoma darasa moja na Abbas Sykes ambae kwake alikuwa mdogo kwa umri.

Akanambia na ndiyo sababu ya urafiki wake na Abbas Sykes kuwa mkubwa kuliko urafiki aliokuwanao na kaka zake Abdulwahid na Ally.

Aziz Ally alijenga jumba la fahari la vioo na vigae Mtoni na sehemu ilipo nyumba yake hii inaitwa Mtoni kwa Aziz Ali hadi leo.

Kwa miaka ile hakuna Mwafrika alikuwa na nyumba kama ile.
Nyumba mfano wa hiyo zilikuwa Oyster Bay makazi ya Wazungu.

Aziz Ally barza yake kubwa ya maongezi ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu nyumbani kwa Kleist Sykes na ndipo lilipokuwa duka lake la vifaa vya ujenzi.

Hii ilikuwa barza maarufu ya wazee wa Dar es Salaam.
Barza hii ilififia baada ya kifo cha Kleist Sykes mwaka wa 1949.

Aziz Ali alikufa muda mfupi baada ya kutoka safari ya Hijja mwaka wa 1951.
Picha: Aziz Ali ujanani na uzeeni.

Samahani huyu jamaa alikuwa mwenyeji wa wapi? Mmanyema kama wewe au Mzaramo?
 
Angeja na shule pia maana kaacha jamii nyingine inakazana kusoma elimu ahera kuliko kusoma elimu dunia

Afu baadae wanalalamika propaganda za kipumbavu eti mfumo kristo mara sijui nyerere ....wakati wako busy kusoma elimu ahera tu
 
S

Hakujenga shule kwa sababu alijua wewe utajenga. In short kaacha wewe ukajenge
 
Angeja na shule pia maana kaacha jamii nyingine inakazana kusoma elimu ahera kuliko kusoma elimu dunia

Afu baadae wanalalamika propaganda za kipumbavu eti mfumo kristo mara sijui nyerere ....wakati wako busy kusoma elimu ahera tu
Ashampoo...
Angejenga na shule...

Shule ilijengwa kupitia Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933.

Jengo la shule hiyo lipo hadi leo na limetaifishwa na serikali.

Serikali imeombwa na Waislam warejeshewe jengo lao lakini hadi leo bado halijarejeshwa.

Tukiwa katika suala hili la ujenzi wa shule nifahamishe unamjua tajiri gani kwenu ulikotoka aliyejenga shule miaka hiyo ya 1930s.

Shule zilikuwa zikijengwa na Wamishionari na Serikali.

Hii lugha ya "kulalamika," na "propaganda za kipumbavu," haipendezi.

Kusoma elimu akhera.
Huna elimu ya kutosha kujadili.

Nakushauri ukae kitako ujifunze historia ya Uislam na Elimu katika Pwani ya Afrika ya Mashariki.
 
Kuna la kujifunza katika hii historia ya maisha yake. Hakika alikuwa mtu mwema japo hakuna mkamilifu. Asante kwa andiko zuri
 
Asante kwa historia hii,niliwa kaa hapo pembeni ya jumba lake ,na mle ndani nishaingia mara kadhaa.
 
Sasa ka
Ashampoo...
Angejenga na shule...

Shule ilijengwa kupitia Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933.

Jengo la shule hiyo lipo hadi leo na limetaifishwa na serikali.

Serikali imeombwa na Waislam warejeshewe jengo lao lakini hadi leo bado halijarejeshwa.

Tukiwa katika suala hili la ujenzi wa shule nifahamishe unamjua tajiri gani kwenu ulikotoka aliyejenga shule miaka hiyo ya 1930s.

Shule zilikuwa zikijengwa na Wamishionari na Serikali.

Hii lugha ya "kulalamika," na "propaganda za kipumbavu," haipendezi.

Kusoma elimu akhera.
Huna elimu ya kutosha kujadili.

Nakushauri ukae kitako ujifunze historia ya Uislam na Elimu katika Pwani ya Afrika ya Mashariki.
Sasa mbona wengi wenu akili hamna pwani yote hakuna la maana za dsm ...uislam ni janga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom