Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
HARRY BELAFONTE NA HAMZA AZIZ
Hamza Aziz kazaliwa Mtaa wa Kipata mtaa ambao mimi nimezaliwa.
Babu yangu Salum Abdalah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Hamza na Dossa Aziz.
Kwa ajili hii Hamza Aziz wamejuana na baba yangu toka udogoni kwao.
Hamza Aziz kwangu alikuwa baba na rafiki na tukizungumza mengi sana hadi alipotangulia mbele ya haki tulikuwa hivi.
Jana niliweka picha ya Harry Belafonte na Sidney Poitier na nikasema kuwa watu hawa maarufu walikuwa nyumbani kwa Ally Sykes.
Rose Aziz bint ya Hamza Aziz jana usiku kaniletea ujumbe baada ya kuona picha ile na kunifahamisha kuwa pale ni nyumbani kwao Msasani na baba yake ndiye siku hiyo aliyewaalika Harry Belafonte na Sidney Poitier nyumbani kwao pamoja na Ally Sykes na John Malecela.
Kwenye picha ya kwanza John Malecela amekaa pembeni ya Sidney Poitier.
Naweka hapa picha za siku hiyo adhimu wakati Harry Belafonte na Sidney Poitier walipokuwa wageni wa Hamza Aziz nyumbani kwake Msasani.
Rose amenieleza kuwa Hamza Aziz alikutana tena na Harry Belafonte Canada na Sidney Poitier Marekani na wakabakia kuwa marafiki wa karibu.
Mzee Hamza Aziz mimi na yeye tukimpenda Nat King Cole na akanieleza kuwa katika ujana wake akiziimba nyimbo zake.
Siku moja aliniimbia nyimbo ya Nat King Cole, ''I Love You For Sentimental Reasons.''
Abbas Sykes na Hamza walikuwa marafiki wakubwa sana.
Balozi Sykes alikuwa akimtania Hamza Aziz kwa kumwita jina lake la utani ''Nat King Cole'' akilifupisha kwa kumwita ''Nat.''
Hamza Aziz na yeye akimwita Balozi Sykes ''Spencer Tracey'' jina la muigizaji maarufu katika miaka ya 1950 hadi 1960.
Mwenyezi Mungu awarehemu wazee wetu hawa.
Picha tatu za chini kulia ni Hamza Aziz, Sidney Poitier na Harry Belafonte.
Walio simama kulia Hamza Aziz na Harry Belafonte chini kulia Sidney Poitier na John Malecela
Kulia Harry Belafonte, Sidney Poitier na Hamza Aziz
Harry Balafonte

Sidney Poitier
Hamza Aziz
Hamza Aziz