Zanzibar 2020 Kibandamaiti, Zanzibar: Uzinduzi wa kampeni za Maalim Seif usipime

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,237
Ni hivi , kama kuna Mwanaccm yeyote anayetegemea Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya sanduku la kura basi ni vema akaendelea na shughuli zingine , kwa hali ilivyo Zanzibar tangu asubuhi ya leo, ambayo ndio siku ya uzinduzi wa kampeni za Maalim Seif wa ACT WAZALENDO hakuna namna yoyote ya Hussein Mwinyi kushinda , Hakuna!

Labda kama atatumia njia alizotumia baba yake ambaye ni Rais mstaafu , ikumbukwe kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya kuteuliwa tu kwenye vikao vilivyofanyika Dodoma , hakuwahi kupigiwa kura na Wazanzibar.

=====

Kampeni za ACT zatikisa Zanzibar

UZINDUZI wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo jana, uliutikisa mji wa Zanzibar, ambapo umati wa wakazi ulijitokeza katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti.
seif.jpg

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AKUHUTUBIA WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CHAMA HICHO KATIKA VIWANJA VYA KIBANDAMAITI ZANZIBAR JANA. PICHA: MTANDAO

Uzinduzi huo uliendana na kampeni za kuwanadi wagombea urais wa Zanzibar, uwakilishi, ubunge na udiwani kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Licha ya jua kali lililokuwa likiwaka, lakini wananchi na wafuasi wa chama hicho walifika mapema majira ya saa nne asubuhi viwanjani hapo, ambapo viongozi wa chama hicho walianza kuzungumza majira ya saa kumi jioni.

Katika viwanja hivyo vilipambwa kwa rangi ya zambarau na nyeupe, huku wasanii mbalimbali wakitumbuiza.

MEMBE AKOSEKANA
Wafuasi wa chama hicho walitarajia kumuona mgombea wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe, kuhudhuria mkutano huo, lakini hakuwapo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, huku ikielezwa kuwa kesho chama hicho kitaendelea na mikutano yake ya kampeni Kisiwani Pemba.

MAALIM SEIF ATAJA VIPAUMBELE
Akiwahutubia wananchi na wapenzi wa chama hicho, mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema akipewa ridhaa atahakikisha Zanzibar inakuwa na katiba mpya yenye maamuzi kamili.

Alieleza kuwa pia atahakikisha anaimarisha uchumi na kutafuta vyanzo vipya vya mapato ikiwamo kujenga bandari mpya na uwanja wa ndege wa kisasa.

Maalim Seif aliwataka vijana ambao hawajaoa kujiandaa kuoa na wale ambao wana mke mmoja kujiandaa kuongeza mke kwa sababu akiingia madarakani uchumi utaimarika.

Alieleza kuwa Zanzibar ina utajiri mkubwa na vyanzo vingi vya mapato, lakini bado hakuna ubunifu wa kuvitumia vyanzo hivyo. “Nikipewa ridhaa na wananchi kuiongoza Zanzibar nitahakikisha tunakuwa na Katiba mpya yenye maamuzi kamili,” alisema Maalim Seif.

Aidha, aliendeleza kauli yake ya kuwa hatokubali kunyang’anywa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, na kuwataka wafuasi wa chama hicho kulinda kura zao.

Alieleza kuwa atahakikisha anaboresha sekta ya elimu na kutoa elimu bure hadi chuo kikuu ili nchi iweze kupata wataalamu na kuwa na maendeleo.

Alisema hivi sasa milango ya kwenda ikulu ipo wazi baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumthibitisha kuwa mgombea kutokana na kuwekewa pingamizi, lakini alishinda pingamizi hiyo.

KAULI ZA ZITTO
Naye Zitto Kabwe alisema kuwa chama hicho kitakaposhinda katika uchaguzi mkuu kitahikikisha kinaunda akaunti ya pamoja kwa ajili ya mapato ya muungano ili Zanzibar iweze kufaidika na mgao wa Muungano.

Aliwataka Wazanzibari kumchagua Maalim Seif ili kuwaletea maendeleo, na kwamba maendeleo hayo hayawezi kupatikana bila ya kuwa na serikali tatu. Alisema ACT itahakikisha inasimamia Katiba mpya ili Zanzibar iweze kunufaika na maendeleo.

Alieleza kuwa watahakikisha kuwa wagombea wao walioenguliwa na tume ya uchaguzi wanarejeshwa na watafanya maandamano kisiwani Pemba kesho.

FB_IMG_1599946040434.jpg
FB_IMG_1600002849676.jpg
FB_IMG_1600002807741.jpg
FB_IMG_1600002801856.jpg

1600062477621.png
1600062490397.png
1600062503527.png
1600062536774.png
1600062551995.png

 
"Tunamalizia pale tulipopaacha 2020". Sijaelewa. Au ilikusudiwa "...pale tulipopaacha 2015"?
 
Ni hivi , kama kuna Mwanaccm yeyote anayetegemea Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya sanduku la kura basi ni vema akaendelea na shughuli zingine , kwa hali ilivyo Zanzibar tangu asubuhi ya leo , ambayo ndio siku ya uzinduzi wa kampeni za Maalim Seif wa ACT WAZALENDO hakuna namna yoyote ya Hussein Mwinyi kushinda , Hakuna !

Labda kama atatumia njia alizotumia baba yake ambaye ni Rais mstaafu , ikumbukwe kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya kuteuliwa tu kwenye vikao vilivyofanyika Dodoma , hakuwahi kupigiwa kura na Wazanzibar .

View attachment 1568384
"Uanisi sasa basi" mpaka mtu akitumia kauli hizi ujuwe jambo lipoo.. sasa wafanye huo uanisi wao waone!


HEKO Ndugu Erythrocyte
HEKO MAALIM KIPENZI CHA WAZANZIBARI
 
Nov 2020 mtarudi na hadithi za Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya
Mwaka huu Ccm mjiandae kung'atuka maana hata like bao la mkono halitakuwepo. Mgombea wenu baada ya kuingia ikulu alijisahau sana hata waliomsaidia aliwageuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom