KIBANDA: Nilisikia akimwambia Mwenzake AFANDE 'mshuti... mshuti'

Kwa matamshi hayo,basi hii awamu ni awamu ya "magaidi"

mkuu Salary Slip hakuna wakati serikali ya Tz imewahi kuwa dhaifu kama awamu wa nne,hakuna mtu anaejihisi yu salama chini ya vyombo hivi vya ulinzi na usalama.
 
Last edited by a moderator:
Utawala unapofika mwisho tegemea haya yote kutokea.Kadri unyanyasaji unavyozidi dhidi ya watu wake ni dalili tosha ya kuanguka kwa serikari iliyopo madarakani.
 
Inahuzunisha sana! Mungu amjaalie apone haraka.

Wasi wsi wangu ni kuwa kuna watu wana ajenda ya siri na serikali. Wana plot haya matukio ili kuichafua serikali iliyopo madarakani. Kimantiki, baada ya tukio la Ulimboka, usingetegemea serikali (kama ndio waliohusika na Ulimboka) kurudia the same tactics. Haingii akilini. Serikali lazima iact seriously na hili genge la wahalifu, kinyume chake wananchi watashindwa kuofautisha.
 
Na hizi kampuni za ulinzi binafsi hazilitumii hili neno?

NI kweli zinatumia, lakini angalia mazingira ya mhanga wa tukio, mwandishi wa habari ambae serikali na polisi wana issues nae kuhusu uandishi wake, halafu anza process ya "ku-eliminate" suspects, kwa kujiuliza swali kama, nani wanaotumia neno afande na wako likely kutenda jambo hili na kwa nini, Kampuni za Ulinzi? Jeshi la Magereza? Jeshi la Wananchi? Jeshi la Polisi?
 
Mungu amsaidie katika kupona kwake kama alivyomsaidia katika kuifanya bunduki i-jam. Amina
 
NI kweli zinatumia, lakini angalia mazingira ya mhanga wa tukio, mwandishi wa habari ambae serikali na polisi wana issues nae kuhusu uandishi wake, halafu anza process ya "ku-eliminate" suspects, kwa kujiuliza swali kama, nani wanaotumia neno afande na wako likely kutenda jambo hili na kwa nini, Kampuni za Ulinzi? Jeshi la Magereza? Jeshi la Wananchi? Jeshi la Polisi?

Nilikuwa najaribu kupanua wigo wa upelelezi !
 
Ndugu wapelelezi, mashahidi, mahakimu, wazee wa baraza, mawakili na mahakimu wa jf muwe na subira,mana tayari mshaleta mashtaka tena wenyewe mkayatolea hukumu.tumuombe Mungu polisi wetu wafanye kazi kwa weledi wa hali ya juu ili mabaradhuli waloyatenda haya wapatikane na kufikishwa ktk vyombo vya sheria.
 
Inahuzunisha sana! Mungu amjaalie apone haraka.

Wasi wsi wangu ni kuwa kuna watu wana ajenda ya siri na serikali. Wana plot haya matukio ili kuichafua serikali iliyopo madarakani.

Kimantiki, baada ya tukio la Ulimboka, usingetegemea serikali (kama ndio waliohusika na Ulimboka) kurudia the same tactics.

Haingii akilini. Serikali lazima iact seriously na hili genge la wahalifu, kinyume chake wananchi watashindwa kuofautisha.


.......

Serikali ndio genge la wahalifu. Kutekwa kwa ulimboka hata mwanafunzi aliyepata zero form 4 angepewa access ktk vyombo husika asingeshndwa kugundua kuwa Ikulu ndiyo iliyohusika..genge la waharifu haliwezi kujichunguza.
 
jamani watanzania kwanini tusisimame kwa pamoja na kusema sasa yatosha!! Jamani inawezekana? Tutayaangalia mambo ya kinyama kama haya mpaka lin??

......

Siri ya kwanza ya ushindi vitani ni kumtambua adui yako....wa kweli.....asiwe wa kuchonga......
 
Hayo mambo ya kuteka na kupiga wanaharakati tulikuwa tukiyasikia tu kwa majirani zetu hasa Kenya, sasa yameingia na Tz, Ee Mungu inusuru Mama yetu Tanzania, naomba serikali sikivu chini ya Kanali Jakaya Mrisho Kikwetu iyaone mambo haya, usalama wa taifa wapo, jeshi la polisi lipo tunakoelekea siko watanzania, tulirithishwa Tanzania yenye amani tele na wazee wetu, hivi sisi tutawarithisha watoto wetu Tanzania ya aina gani?. Mungu ibariki Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom