mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
KIBANDA MPIGANAJI AU MPIGAJI?
Mwandishi mweredi au mjuvi hujipambanua kwa Falsafa/msimamo wake. Mara nyingi waandishi wa fasihi andishi huonesha falsafa zao katika mfululizo wa maandishi yao. Falsafa hiyo hujengwa na mwandishi kutokana na msimamo wake katika jambo au mambo fulani.
Mfano mwandishi anaweza kuwa ana falsafa ya kimapinduzi, mwandishi wa aina hii hujipambanua katika maandishi yake pasi kuyumba au kuyumbishwa. Mwandishi wa aina hii hata akiandika dhana ya mapenzi, huyaonesha katika umapinduzi.
Waandishi wengi wasasa, hujipambanua kama wapiganaji sijui ni tafsiri ya mapinduzi? Sijui, lakini wamekuwa watetezi wa waslahi ya matumbo yao. Nimeamua kuandika haya mara baada ya kuonekana kuwa Kibanda ni mwandishi mahiri tena mwenye msimamo usiyoyumba.
Jambo ambalo mimi naliona kinyume kabisa, naona kuwa Kibanda ana msimamo katika kutetea maslahi yake binafsi. Naomba nisihusike na matatizo aliyoyapata Kibanda (sio woga) bali nihusike katika kukosoa weredi na msimamo unaosemekana anao Kibanda.
Kibanda kama mwandishi aliyejipambanua kutetea maslahi ya mwajiri wake na chama cha mwajiri wake, alikuwa mwiba wa kuikosoa serikali ya awamu ya nne hata pale penye kuisifia ama kuipa pongezi. Ni nani aiyejua jua juu ya tamko la pale mwembe yanga juu ya mafsadi, lilienezwa na kupambwa na vichwa vya habari motomoto na vyenye naksi murua, ili kuvutia wasomaji.
Nnani asiyejua gazeti la Tanzania Daima lilishadadia juu ya kashfa ya Richmond likiweka na mapambio mbele? Ni nani asiyejua baada ya Zitto Kabwe kutofautiana na mwajiri wa Kibanda alianza kusakamwa kama ruba mwilini. Hapa Kibanda alionesha msimamo ambao kila mtu alimuona ni mwandishi mpiganaji asiyeyumba.
Dhana ya utazamishwaji na uhalisia, Kibanda aliwatazamisha watu ili wamuone kuwa yeye ni bora na anasimamia maslahi ya umma, lakini hasha, Kibanda anasimamia Tumbo lake na jamaa zake. Hana jipya ambalo anaweza kujipambanua nalo. Mzalendo wa kweli hujipambanua na husimamia kweli basi kuyumba, hawezi kuungana na dhariri hata kidogo. Kibanda amekuwa ni mtu wa kuvizia, yaani mwenye kisu kikali ndiye mla nyama.
Kitendo cha Kibanda kujiunga na New habari Corporation ni aibu kwa waandishi wanaojipambanua kama wapiganaji na watetezi wa umma. Hii inaonekana ni watazamishaji, na huwafanya watu kuwa vizuu ambao hawajui kusoma hata irabu "a".
Kampuni ya New Habari Corporation ni kampuni ya Rostam Aziz ambaye Kibanda alimtusi na kumuita fisadi, pia kampuni hii niya kada wa CCM, chama ambacho Kibanda kwa vazi alililokuwa nalo hapo awali asingeweza hata kidogo kuunga nayo.
Msimamo wa Kibanda uko wapi, huyu ni mwandishi chapwa, ambaye hufikiria tumbo lake na kutumia upepo wa wananchi kuwapumbaza ili aonekane shujaa na aaminiwe.
Pole Kibanda, naandika haya sio kwasababu Kibanda amefanyiwa tendo baya ambalo mwanadamu hastahili. Bali ni mtizamo tu juu ya waandishi vigeugeu. Natamani aliyemjeruhi Kibanda nimfahamu ili nijue kwanini alifanya hivi.
1. Kwa kumjua tutajua kweli huyu alikuwa mpiganaji au mpigaji
2. Kwa kumjua tutajua alitetea wananchi au tumbo Lake.
Najua nitahukumiwa chanya ama hasi kwa mtazamo wangu huu.