Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
Mwisho Mkuu Mwita Maranya,miongoni mwa watu ambao huwa wanaheshimu hoja zao humu ndani Jamvini ni mimi,lakini leo hii nashangaa umekua na jazba sana na Kibanda,au kwa sababu ameigusa CHADEMA?,mbona siku zote za Nyuma ulikuwa mfuasi mkuu a Kibanda hata kama alikuwa ameandika Utumbo katika kuisifia CHADEMA ama kiongozi yoyote wa CHADEMA,hizi hasira zako za leo zinatoka wapi Mkuu?
Sio kwamba ana kesi huyu Kibanda na anataka kupotezea kwa kusifia MAGAMBA ili afutiwe mashtaka?
Maranya hizi ni propaganda tu,na nahisi ninyi ndio mnaowapotosha hao wanaotaka mapinduzi ya nchi hii,na nashawishika kuamini kwamba wewe utakuwa ni mpinzani namba moja ya wale wanaohitaji mabadiliko kwa sababu unasimamia uongo na upotoshaji.
Kama ni ukweli kwamba Kinana ni Kimbunga kwanini asiseme? Sioni ubaya wa kusema hayo!Huyu bado tu hataenda habari corporation?
Kumsifia mtu ndio UKWELI(maadili), kweli hii taaluma inatumika kama mpira wa kiume!
Huwezi amini kama ndio mwenyekiti wa jukwaa la wahariri
Ni kipi ulichoona hakina msingi na kwamba kinaitia aibu taaluma ya uandishi? Tumpinge kwa hoja. kauli ipi umeona haina maana na ni ya aibu?Ni aibu kubwa kwa waandishi kama hawa katika Tanzania.
Sijaelewa bado. Napata taabu sana kuona wengi mnampinga Kibanda pasipo kusema tatizo lake lipo wapi? Anamwongelea Kinana kwamba ni mwanasiasa mwenye nguvu, wewe unasemaje? Ningekuona una hoja kama ungeleta maelezo ya kina kupinga kwamba Kinana hana nguvu, na kueleza ni kwa kiasi gani Slaa au CHADEMA ina nguvu kuliko Kinana.Kifupi ni kwamba Kibanda anajiandaa kuondoka FREE MEDIA. Ila sasa style anayoondoka nayo ya kutafuta Bifu na mwajiri ndiyo ya kushangaza, a childish and old style.
Kweli ni ipi? Tuambie hiyo kweli unayoifahamu kuhusu uwezo wa Kinana, kama hana nguvu kama Kibanda anavyomsifia or not. Na utupe mapendekezo tufanyeje ili kuzikabili nguvu zake.Walikuwepo wengi wa hivyo wakapita, huyu naye atapita; Na mbwembwe zake zitapita, na uandishi wake Utapita.
Lakini kitu kimoja tu ambacho hakitapita ni UKWELI
Kweli ya Mungu Itabakia na hakuna Changanya changanya
Mkuu unaamini Kinana ni Kimbunga? ndio maandili ya uandishi wa Habari?Kama ni ukweli kwamba Kinana ni Kimbunga kwanini asiseme? Sioni ubaya wa kusema hayo!.
Ukisoma makala ya mwandishi na maoni ya watu wengi humu janvini utagundua kuwa, mwandishi, CHEDEMA na mashabiki wengi humu jf wana matatizo yaleyale.
Mwandishi yeye anapenda watu wamuone kama perfect in everything. Katika makala yake, sikuona au kusoma sehemu yeyote ambayo ameeleza upungufu au makosa katika maamuzi au maono yake toka mwaka 1995 mpaka anapoandika makala hii zaidi ya kusema yeye siyo nabii wa siasa za Tanzania. Hakuna binadamu perfect in everything hapa duniani. Ningeweza kuona umaana halisia wa kile alichokiandika kama angeonyesha katika makala yake kuwa naye ni binadamu ambaye kuna sehemu maamuzi yake katika miaka 19 ya uandishi wa habari alifanya makosa.
Kile anachokilalamikia kwa CHADEMA na mashabiki kuwa ni walevi wa fikra na yeye ndicho hicho anachokifanya kwa sasa.
CHADEMA na Mashabiki wake wengi lazima nao wajifunze na wakubali kuwa nao sio perfect in everything. Lazima wakubali kukoselewa, na wajifunze kushukuru pale wanapokoselewa kwa sababu siyo rahisi kupata wakosoaji wasiowatakia mema katika utendaji wao. Kutokubali kukoselewa ni dalili ya chama na mashabiki kubweteka na huo mara nyingi huwa ni mtaji wa failure.
Abi Kibanda! Nakushangaa sana. Kwanza wewe ni mwongo msahaulifu na pia jua kuwa atakaye kukosoa hapa ni kijana mdogo.
UMESEMA mwaka 1995 hukuunga mkonn harakati za Mwl . Nyerere (udikteta katka demokrasia) ili Mkapa awe mgombea urais kupitia CCM, na umethibitisha kwa kusema utabiri wako ulitimia kwa Mkapa kuboronga mwishoni. Lakini pia umesema ulipinga 2005 Kikwete kugombea urais na hadi ukakwaruzana na Rostam, hata hivyo Kikwete alishinda na kwamba wote tunashuhudia kuboronga kwake.
Sasa huyu ndo Kikwete aliyepokonywa karata na Mwl. 1995 kwa kumpendekeza Mkapa, sasa 1995 wewe ulikuwa upo kwa mgombea yupi? Au Kikwete wa 2005 uliyempinga alikuwa sio yule aliyefanyiwa udikteta 1995?
Tukiendelea zaidi pia umesema, Mrema 1995 kupitia NCCR hukumkubali. Je mwaka huo basi wewe ulikuwa huna mgombea wa kumpa kura yako?
Au alikuwa wa chama kipi mbali na hivyo viwili.
POMPO mimi simjui Kinana, ndiyo maana nataka watu watupe facts za kwanini Kinana si Kimbunga. Huyu mtu amekuwa meneja wa kampeni za CCM tangu mwaka 1995, kwa hiyo anajua propaganda za kisiasa zote, ameshakabiliana na akina Mrema, Lipumba, Mbowe na Slaa. Anawajua inn and out. Ni kwa vipi humuoni kama ni tishio katika anga za kisiasa? Ni nani wa upinzania mwenye uzoefu mkubwa kama wa Kinana? Hapa mimi nafikiri upinzani tujipange tu, na si kubeza uwezo wa Kinana. Namna pekee ya kummaliza Kinana labda ni kuzihuisha hizo propaganda za kwamba ni mwizi. Labda hiyo itasaidia kumpunguzia nguvu, otherwise, ni lazima tukubali ukweli kwamba Kinana ni tishio.Mkuu unaamini Kinana ni Kimbunga? ndio maandili ya uandishi wa Habari?
Wewe ndiye unapiga propaganda hapa wabhejasana.
Juzi mwenyekiti wa ccm taifa raisi Jakaya Kikwete amezungumza mbele ya kamera za waandishi wa habari akiwaasa kwamba sasa waache kutegemea polisi kukabiliana na Chadema na hoja zao, kwamba sasa ni wakati muafaka wa wao kujitokeza hadharani kufanya mikutano ya hadhara kujibu hoja za Chadema. Sasa unataka uambiwe ama usikie nini na kutoka kwa nani ili uridhike kwamba usalama wa ccm kubaki madarakani uko mikononi mwa vyombo vya dola?
Hawa ccm tukiachiwa tucheze nao siasa kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi na kama vyombo vya dola vitaamua kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi, vikaachana na tabia ya kuilinda ccm, nakuhakikishia kwamba itakufa moja kwa moja. Hilo wanalitambua sana na ndiuo maana wanatumia vyombo vya dola kadri wanavyoweza kuhakikisha kwamba wanaimaliza Chadema kwani bila hivyo hawana uungwaji mkono wowote katika kuiongoza nchi hii.
Mkuu 2010 alikuwa kampeni maneja wa JK, mbona alianza kulalamika kuwa familia ya JK inamuingilia majukumu yake?POMPO mimi simjui Kinana, ndiyo maana nataka watu watupe facts za kwanini Kinana si Kimbunga. Huyu mtu amekuwa meneja wa kampeni za CCM tangu mwaka 1995, kwa hiyo anajua propaganda za kisiasa zote, ameshakabiliana na akina Mrema, Lipumba, Mbowe na Slaa. Anawajua inn and out. Ni kwa vipi humuoni kama ni tishio katika anga za kisiasa? Ni nani wa upinzania mwenye uzoefu mkubwa kama wa Kinana? Hapa mimi nafikiri upinzani tujipange tu, na si kubeza uwezo wa Kinana. Namna pekee ya kummaliza Kinana labda ni kuzihuisha hizo propaganda za kwamba ni mwizi. Labda hiyo itasaidia kumpunguzia nguvu, otherwise, ni lazima tukubali ukweli kwamba Kinana ni tishio.
Mkuu Free Media, ni mali ya Chadema.