Wana-JF!!
Mnamkumbuka mhariri ABSALOM KIBANDA? AMBAE ALITEKWA NA KUTESWA?, amesema yafuatayo kuhusu wahusika ambao walimfanyia vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vimempa ulemavu wa kudumu wa jicho lake. Nanukuu;
"Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia. Mmoja wa watu walio nishambulia ana fanana kwa sura na umbile la Ludovick Rwezaura yule kada wa CHADEMA aliyewekwa ndani na Lwakatare ambae nimemuona kupitia magazeti na mitandao ya kijamii. Nimeshangazwa sana mtu huyu yupo karibu na baadhi ya wahariri wenzangu na hata msaidizi wangu bwana Ansbert Ngurumo, bado napata shaka ni kuwa watu wana fanana au?"
My take;
Ndugu Ludovick ambae kwa sasa bado yupo mahabusu, alikuwa ni mfanyakazi wa CHADEMA makao makuu, chini ya kurugenzi ya ULINZI na USALAMA kabla ya kukutwa na mkasa wake ambao ndio umemuweka rumande mpaka hivi sasa. Kuwepo kwa kijana huyu kwenye hii kurugenzi na maelezo ya bwana Kibanda nadhani wana-JF mnaweza ku-connect dots.
CHADEMA ukweli ni kwamba mwaka 2013 umekuwa mwaka 'tasa' kwenu, kwani mikakati mingi ya kichama imekuwa ikibuma na mbaya zaidi ni pale mpaka siri za ndani ya chama kuzagaa mitaani, haya yote ya kubuma na kuvuja kwa siri ovyo ovyo hivi, kuna sababishwa na 'uchanga' wenu katika kusimamia shughuli za kichama, mna safari ndefu sana.
Source: DIRA YA MTANZANIA.
Baada ya kuwasiliana na Kibanda, katutumia ujumbe ambao yeye aliuandika. Alichokiandika yeye ni kama kinavyoonekana kwenye mabano chini:

====================
UPDATE from JamiiForums
====================
UPDATE from JamiiForums
====================
Baada ya kuwasiliana na Kibanda, katutumia ujumbe ambao yeye aliuandika. Alichokiandika yeye ni kama kinavyoonekana kwenye mabano chini:
Kibanda said:Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia,
Mmoja wa watu walionishambulia anafanana kwa sura na umbile na Ludo ambaye nimemuona kupitia katika picha mtandaoni na katika magazeti.
Bado naendelea kutafakari iwapo ni kufanana (maana watu ni wawili wawili) au wana unasaba na mmoja wa watesi wangu... Jamani hadi sasa hii ni dhana tu maana nimeambiwa kule mahabusu aliko amekataa katakata kuwa alihusika katika tukio langu....
==========
1. Nina imani kubwa na jamvi hili ambalo mijadala na wana jamvi wake ni watu walio dhahiri na halisi kwa majina na wasifu wao. Naamini jamvi hili litaleta mabadiliko ya kweli katika taifa hili huko Tuendako. Tusubiri tuone.
2. Bado nina maswali mengi kuhusu kile kilichonifika na kuhusu baadhi ya watu ambao kimsingi ningependa kama taifa tushirikiane kuwachunga na kuwachunguza akiwamo huyo mwana mabadiliko mwenzetu Ludo.
3. Kuchokoza hoja ili hatimaye tupate ufumbuzi na majibu halisi kuhusu kile kilichonitokea hasa baada ya kuwapo kwa jitihada kubwa ndani ya vyombo vya dola na hata miongoni mwa wana habari na wahariri kulipindisha kwa malengo ambayo binafsi siyajui.
Sipendi kuwa mtu wa kwanza kumnyoshea yeyote kidole kuhusu kile kilichonipata. Niseme wazi nilianza kwa kujinyoshea kidole/ vidole mwenyewe kwa tukio lile na kimsingi nimekuwa katika mchakato wa kuangalia nyufa ambazo pengine zilitoa mwanya au kusababisha kijeruhiwa kwangu.
Nataka kutetewa kwa haki na katika misingi halisi na ya kweli. Kwangu Ludo ni kitendawili kigumu sana. Wasifu wake ni tata kweli kweli. Amekuwa mtu wa karibu na watu wengi ambao nimepata kufanya nao kazi kwa karibu na kwa muda mrefu, ingawa hajapata hata mara moja kinifikia au hata kujitambulisha kwangu kwa namna yoyote ile. Bado nautafakari mwenendo huu iwapo ni wa bahati mbaya au uliokuwa umepangwa.
Pamoja na kumpa pole ndugu yangu kifamilia Maggid na mkewe, nilizungumza naye pia namna anavyomfahamu Ludo na kupitia maelezo yake ambayo sina sababu ya kuyatilia shaka nilibaini alikuwa hamjui sawasawa.
Hakujua kwamba ni kada wa Chadema na kwamba alipata kuwa katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama hicho. Hakupata kujua kwamba Ludo alikuwa pia uhusiano ambao hadi sasa hauko wazi na baadhi ya wanahabari na wahariri kwa kiwango ambacho nashangaa kinafunikwafunikwa.
Ludo alipohusishwa na Dennis Msacky na kisha Maggid vyombo vya habari vilishabikia sana hoja hiyo lakini alipokuja kuhusishwa na Ansbert, Balile na Chadema hali ikageuka na kuwa mbaya sana.
Angalau moyo wangu ulitulia baada ya kujua kile ambacho Dennis, Balile na Maggid walikuwa wakiwasiliana na Ludovick.
Hadi leo hii bado sijajua kwa ufasaha na kwa undani uhusiano kati ya Ludovick na Ansbert ambaye mbali ya kuwa msaidizi wangu Free Media Ltd, rafiki yangu wa miaka mingi na mwana habari mwenzangu tunayefanya kazi kwa karibu sana hatujapata kukaa na kulizungumza hili kwa kina.
Wana jamvi uhusiano wa Ludo na Nchemba, Lwakatare, Chadema na Wanasiasa wengine ni jambo ambalo pia linaonekana kufunikwa funikwa sana. Iwapo kweli tunadai mabadiliko ya kweli katika taifa hili tutimize wajibu wetu kuyaleta mabadiliko hayo.
Absalom Kibanda