Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,099
- 9,268
Hoja yako imepoteza uhalali. Mbona hii kitu ilisha pitwa na wakati! Kwani kilicho mfanya Ludovick kuachwa solemba na CHADEMA unajifanya hukijui?
Haya, ushatimiza wajibu wako ulio tumwa na MABWANA zako, chapchap Lumumba kasaini vocha.
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?
Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.
Mwigulu Nchemba ndiye aliyemtuma Ludovick akamdhulu Kibanda ili apate cha kusema kuhusu video ya Lwakatare ambayo waliitengeneza na Ludovick.
Asante sana mhangaikaji! Subiri ufurahie kifo cha CHADEMA ndugu yangu!Acheni zeni nyinyi, Mwigulu akumtaja jina mtu aliyempa pesa za vifaa kwa ajili ya shughuli ya kumrekodi Lwakatare, kwa taarifa yako, bado yuko humo humo CHADEMA.
Huyu kijana CHADEMA mmeamua kumchinjia baharini lakini sio vyema, hemu angalia alipotoka na CHADEMA;
Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)
Halafu hapo hapo anatengeneza video ya Lwekatare, Kisha anampa Mwigulu, halafu anapewa Pesa na Mwigulu halafu anaendelea kuwasiliana na Mwigulu kama mtu na mkewe, halafu anahakikishiwa na CCM kuwa atalindwa.
Hamy-D,
Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda.
I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi.
Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa. Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.
Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote.
Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii.
Hamy-D,
Nimevumilia kwa muda mrefu upuzi na upotoshwaji wako. Uzalendo umenishinda. I challenge you,
Iwapo Ludovick ni mfanyikazi wa Makao Makuu toa basi ushahidi aliajiriwa lini, nani kamwajiri na kwa barua ya Tarehe ngapi, na Kitambulisho chake ni namba ngapi. Nadhani upotoshwaji ni lazima ufike mwisho sasa.Kama walivyo volunteers wengi, Kumbukumbuku ya Makao Makuu ni kuwa Ludovick alikuwa Volunteer, lakini si mwajiriwa Kama unavyotaka kuaminisha jamii. Iwapo utashindwa kutoa ushahidi huo mpaka leo jioni, nitawaomba wanaJF wakohesabu mwongo aliyekubuhi, na JF na Jamii nzima ya Watanzania wakupuuze wewe na posts zako zote. .
Hivi wewe na akili zako timamu ulikubaliana na maelezo ya Marando na zile kauli za wabunge kuhusu hizo pesa alizotuma Mwigulu?
Mbona mnaichukulia hii ishu kirahisi rahisi hivyo? sikiliza mkuu, intelijensia yangu sina shaka nayo, haya yote unayoyaweka hapa usidhani unanishangaza, yote yamekuwa yakisemwa na kuaminiwa na watu wenye maono mafupi kama wewe, mimi nachimba na kutafuta kiini zaidi cha huu mkasa.
Kujaribu kumtenga Ludovick wakati huu ni mchezo wa kitoto. Ludovick ni insider na ameshriki operations nyingi tu za CHADEMA. Nadhani mkiendelea kum-frustrate huyu dogo atawaumbua sana. Watch out!