Kibanda apelekwa kutibiwa Afrika Kusini

Sio wote waliorudi, nasikia kuna Wakenya zaidi ya 500 000 wanaishi nchini kwetu, hivyo wengine wamebaki wengi tu, ndio maana uhalifu hauishi!


......

Ila kweli ee?. Hivi!.....na wale wakenya walioibaga hela za benki mchana kweupe pale benki ya nbc Ubungo walipelekwaga wapi?
 
Mkuu Mag3, breaking news ya Tina ilishushwa humu saa 8 usiku na ikadumu hivyo hivyo hadi saa 2 asubuhi, six hours!, without any update or any collaboration. Nilipopata confirmation toka mtandao mwingine, niliomba msamaha kwa Tina, nikaweka ile confirmation pamoja na picha, ile ile confirmation, post hiyo ilifutwa!, nilianzisha thread ya Kibanda Kama Dr. Ulimboka!, Nae Kupelekwa Afrika Kusini ..., thread hii ikafungwa!.

Mara tuu baada ya kutekwa kwa Dr. Ulimboka, nilianzisha thread ya Mkasa wa Dr. Ulimboka: Inawezekana Kabisa Sio 'Inside Job'!, bali ... hivyo hiki kilichomtokea Kibanda, kimekuwa crafted very carefully ili kifanane na kisa cha Ulimboka just to "make belive" kuwa ni wale wale "wa Ulimboka!" kwa lengo la kupoteza tuu watu maboya!.

Kwa sasa naomba tuzizungumze mengi, lets keep wish him a speedy recovery then we can dig to the bottom of it!.

Pole sana Kibanda, get well soon!.
Pasco.
wamefanya copycat ili tukio lifanane na la ulimboka.Tatizo motive inagoma .mtuhumiwa namba moja hapa lazima atakua bosi wake wa zamani.
 
Hapa kuna pointi ya msingi sana. Ni wachache sana wanaweza iona.
Mkuu Mkeshaji, reading "in between the lines", kunahitaji "levels" fulani za uelewa, wengi wengi bado, but with time and uzoefu, hatimaye tutakuja kuelewana tuu!.

Tuendelee kumtakia Kibanda, uponyaji wa haraka.

Pasco.
 
Hivi watanzania mtaendelea kukimbia nchini kwenu mpaka lini kila mnapohitaji medical attention?
Ina maana hospitali zote zilizopo hapa Tz na sera ya kibepari iliyoanzishwa na magamba ya uwekezaji yote hii ni White Elephants? Hizo hela tunazotumia kutibu viongozi nje ya nchi zingekuwa invested kwenye hii huduma isingewezekana kuongeza ufanisi kwenye hii sekta nyeti dunia nzima?
Kuna siku mtaondoka Tanzania wote muende mkaishi nje ya nchi na hii nchi sijui mtamuachia nani.
Prisoners and slaves in your own country. Pathetic
Ptuuuuuu

Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda, kwa sasa yuko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.

Ndege imekodiwa na mwajiri wake. Hali yake si nzuri.

Tuungane kumwomba Mungu amjalie apone-arejee salama.
 
wamefanya copycat ili tukio lifanane na la ulimboka.Tatizo motive inagoma .mtuhumiwa namba moja hapa lazima atakua bosi wake wa zamani.
Mkuu Elungata, take it from me kuwa hii sio kazi ya Chadema!, bali imefanywa hivyo ili watu waelewe hivyo kama sasa unavyoelewa wewe!.

Hili la Kibanda, ni among "the bad games people play!", "from within!", na amini usiamini, hii ni "ngoma ya nyumbani!", mbona "ole rasmi" ilishatangazwa kupitia .., tungekuwa na TISS ya ukweli, zaidi ya hii "hopeless iliyopo!", walishapaswa kuwajua to keep track on them such that if anything happens to any of them, we know straight forward who is behind!. Nisije nikasema sana na mimi nikaingizwa kwenye "elimination target!".

NB. Kwa sasa nawaomba msiniulize kitu chochote kwanza, hebu tusubiri Kibanda apone, ndipo tusemezane!.

Pasco.
 
Mkuu Mkeshaji, reading "in between the lines", kunahitaji "levels" fulani za uelewa, wengi wengi bado, but with time and uzoefu, hatimaye tutakuja kuelewana tuu!.

Tuendelee kumtakia Kibanda, uponyaji wa haraka.

Pasco.
Then why don't you co- oporate with Police because it seems you know everything!!

Mbona ujagusia wale Waislamu wa Markaz ambao walilionya Gazeti la mtanzaia juu ya habari ya kuendesha mafunzo ya kigaidi kule Ukerewe?

Sintoshangazwa mtu wa kariba yako nikisikia amemwagiwa Tindikali aina ya watu kama wewe ni hatari sana katika jamii sawa na ile redio station ya Rwanda iliyokuwa inachochea mauwaji na ile Radio station ya Kenya.
 
Na siku chache baada ya pasco kuandika hiyo issue ya slaa kumkacha Jk, wilbroad slaa akaenda ikulu.
Yaani baada ya jamaa kuhit point.
 
Then why don't you co- oporate with Police because it seems you know everything!!

Mbona ujagusia wale Waislamu wa Markaz ambao walilionya Gazeti la mtanzaia juu ya habari ya kuendesha mafunzo ya kigaidi kule Ukerewe?

Sintoshangazwa mtu wa kariba yako nikisikia amemwagiwa Tindikali aina ya watu kama wewe ni hatari sana katika jamii sawa na ile redio station ya Rwanda iliyokuwa inachochea mauwaji na ile Radio station ya Kenya.


.......

"If wishes were horses, beggars would have ride!", endeleza tuu hizo dua zako za kuku!, kiukweli, niliwahi kulalamikia baadhi yetu humu ambao ni "prophets of the doom!", wakisema jambo linatokea!, yameishanikutwa makubwa na mpaka sasa naendesha maisha yangu in a "living hell!", hivyo don't just wish me nimwagiwe tindikali tuu, you can as well wish me dead!.

Kiukweli kitendo cha kuhusianisha udini na karibu kila uhalifu ni "utaahira!" its very unfair!. Mhalifu ni mhalifu tuu regardless na dini yake!.

Kibanda get well soon!.

Pasco.
 
Naona intelejensia ya Chadema inafanya kazi ya polisi na vyombo vyengine vya usalama, suala la kujiuliza ni kwa mantiki ipi na kwa maslahi ya nani?
 
jamani hali ya namna hii mpaka lini?kweli watanzania tumefikia hatua ya kutesana kiasi hiki,INUMA SANA
 
Mhhhhhhh!!!! Kwa hiyo unataka kutwambia nini hapa??? kwamba nyie ndo mlishiriki kumtesa Dr. Ulimboka??? Bira shaka ni kweli ni nyie na ndo maana mkaa kimya kana kwamba hakuna kitu kilichotendeka!!! Unafikiri nikisema huu ni mpango ambao umesukwa ili kuibambikia CHADEMA mkasa huu ili mje na sababu hizi ulizokuja nazo??? Je umeshajiuliza ni nini kilimbadilisha Kibanda kuwaona watu aliwahi kuwaona ni mafisadi na baadae wanaonekana hao hao ni wasafi?? Nadhani kuna kitu kimejificha ambacho hatukijui ila tunakurupuka tu kupandikiza chuki kwa vitu ambavyo wala havitatusaidia kamwe. Kumbuka kuwa siku zote "Penye ukweli uongo ujitenga" hata kama itachelewa lakini ipo siku itafahamika.

Na mkaamua machadema kumsulubu Kibanda kwa style yenu ile ile
KUSHAMBULIWA KWA KIBANDA-NIMUHANGA WA ALICHOKIANDIKA..? Connected dots…!
Jana usiku limetokea tukio baya la kuvamiwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Ndugu Abdalom Kibanda.
Tukio hilo ambalo limesababisha sintofahamu kubwa miongoni mwa watanzania wanahabari, wapenda uwazi na ukweli na wale wenye kusimamia misingi ya Amani na utulivu katika nchi hii.
Aina ya tukio lenyewe na upekee wa utokeaji wake umegubikwa na utata mkubwa kiasi kwamba akili yangu ikanituma kutafakari kwa kina na kuyaandika haya, ikiwa ni miongoni mwa YAWEZEKANAYO kuwa ndiyo yaliyosababisha tukio ilo la kusikitisha kutokea kwa Mtanzania mwenzetu huyu kipenzi cha wanahabari.
•Mengi yanahusuanishwa na tukio hili, lakini wengi wakihusianisha tukio hili na kazi ya mhusika ya Uandishi, ambapo tukio hili linamkuta katika kipindi ambacho mtindo wa uandishi wake umebadilika na mfumo wa hoja zake umekuwa wa mlengwa wa kati. Lakini pia wapo wachache wanaohusianisha tukio hilo na ujambazi ama unyang’anyi, hisia ambazo binafsi nazipinga kwani Watu waliomvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake hawakuchukua kitu chochote katika vitu ambavyo Mhariri huyo anavimiliki kuanzia gari, simu na pesa.
•Hivyo, nalihusianisha tukio hili na aina ya kazi ambayo mhanga anaifanya, kazi ya UHARIRI WA HABARI katika vyombo vya habari, na hisia zangu zimenipeleka huko baada ya kuzingatia kwa umakini mkubwa matukio yafuatayo.
a)14th November 2012, Baada ya kuundwa kwa sekretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kibanda akiwa ni Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima ambalo linafahamika wazi kuwa ni chombo cha propaganda cha Chadema chini ya Mbowe, aliandika makala ambayo ilikuwa ikisifu safu hiyo mpya ya uongozi ya CCM,
huku akinukuu kauli mbalimbali za viongozi wa upinzani akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Znz, Mhe. Maalim Seif Sharif. Baada ya tukio hili wakuu wa gazeti hilo walimuita na kumuonya juu ya makala yake hiyo.
Lakini katibu Mkuu wa Chadema hakuishia na kuridhishwa kwa kuonywa kwa Kibanda bali alienda mbele zaidi na kumjibu; ambapo tarehe 16th November 2012, sehemu ya nukuu yake alipokuwa akimjibu Kibanda inapatikana katika link hii; Dk Slaa awashambulia walioteuliwa sekretarieti mpya ya CCM, asema wapo kwenye kashfa ya EPA

Na link nyingine ndani ya Tanzania Daima la ijumaa ya tarehe 16 th Nov 2012 ni hii;

Dk. Slaa aichambua CCM

b)Lakini mara tu ya jibu hilo la Slaa kwa Kibanda, Mhariri huyo kwa ufundi mkubwa aliandika makala nyingine ambayo ilikuwa ikimsifu zaidi Katibu Mkuu mpya wa CCM, ndugu Abdulrahaman Kinana, ambae Slaa alimkosoa katika majibu yake dhidi ya Kibanda. Mhariri huyo makini alieleza bayana kuwa kuiponda sekreatieti mpya ya CCM ni sawa na kukosa akili, akaendelea kufafanua na kutaja wasifu wa kila kiongozi kwa kadri alivyowafahamu yeye, akielekeza nguvu zaidi kwa Katibu Mkuu Kinana na kuelezea umahiri wa kinana kama strategist tangu akiwa jeshini, lakini akataja uzoefu wake ndani ya chama na pia kutaja alivyoshiriki katika chaguzi mbalimbali na kuwawezesha wagombea urais wa Awamu ya tatu na Nne kushinda kwa kishindo.
Baada ya Makala hiyo ya pili, ulizaliwa mgogoro wa haja ndani ya kampuni hiyo ya freemedia uliomuhusisha Kibanda na wamiliki wa kampuni na Chama kinacholitumia gazeti hilo. Mgogoro ambao ulipelekea Kibanda kuihama Freemedia na kuhamia katika New Habari Corporation ambayo kimsingi ni ya wadau wa Chama Cha Mapinduzi na kampuni ambayo kwa namna moja ama nyingine inaruhusu kuandikwa habari katika mandhari na tafsir ya HABARI bila propaganda wala upendeleo. Kwa maana nyingine ni kuwa Ndugu Kibanda alikuwa akihariri habari ambazo zinasema ukweli wa mazuri ya chama cha Mapinduzi na kuimwagia sifa kwa mipango yake ya kuiletea nchi Maendeleo lakini pia kwa kasi ya utekelezaji wa Ilani ya chama.
Baada ya Uamuzi huo wa Kibanda kuhamia New Habari Corporation na kuiandika habari zenye mlengwa wa Kati, wakuu wa Free media walimuita ili kufanya nae mazungumzo ya kumtaka kurejea katika kampuni yao, hasa baada ya Gazeti lao la Tanzania Daima kuanza kupoteza dira na kuandika habari ambazo hazina mvuto hivyo kulifanya kushuka kimauzo na kipropaganda dhidi ya Chama Cha Mapinduzi. Lakini Kibanda aliendelea kukataa kurudi na kuwa pamoja na viongozi hao wasiojua nini maana ya kuwa kiongozi, hawaheshimu taaluma wala hawataki kuruhusu fikra huru kuchukua nafasi katika chama na Kampuni zao.
Kulingana na ukweli huo wa kuwepo kwa uhasama baina ya Mhariri Huyu makini na mabosi wake wa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi hapo awali, hisia zangu zinanipelekea kuamini kuwa yawezekana kabisa mpango huu wa kumvamia, kumshambulia na kuhatarisha maisha yake umeratibiwa na viongozi hao ambao hali nao sahani moja, na ndiyo asili ya swali JE, KIBANDA ni muhanga wa alichokiandika..?
 
Nahisi South Africa wataanzisha kitengo rasmi cha kupokea majeruhi wa aina hii toka tanzania!
 
Naona intelejensia ya Chadema inafanya kazi ya polisi na vyombo vyengine vya usalama, suala la kujiuliza ni kwa mantiki ipi na kwa maslahi ya nani?

......

Al shabaab huwa tunawagunduwa kwa miandiko yao tu.
 
wamefanya copycat ili tukio lifanane na la ulimboka.Tatizo motive inagoma .mtuhumiwa namba moja hapa lazima atakua bosi wake wa zamani.

..........
Huko kwa bosi wake wa zamani alikuwa na umuhimu mkubwa kiasi gani na baada ya kuondoka amesababisha madhara kiasi gani hadi waamue kumfanyia hivyo?

Hakuna watu wanaomchukia na pia wenye uadui na huyo bosi wake wa zamani wanaoweza kufanya hivyo kwa advantage ya kumsingizia huyo bosi wake wa zamani?

Kubenea alivyomwagiwa tindikali inawezekana nae alikuwa ni bosi wake wa zamani?
 
Mungu amponye Kibanda arudi tena ulingoni. Quick recovery and total healing of the wounds in Jesus Name
 
Mbeya! Mbeya! Mmekosa nini?

1. Mwakyembe
2. Mwangosi,
3. Ulimboka,
4. Kibanda,
5. ...........
6. .......... to mention few,

Mungu nusuru watu wako toka mbeya maana hatujui baada ya Kibanda nani atafuata. Mungu wapige upofu wote wanaofanya mabaya haya. na kama kuna anayejiandaa, Mungu muabishe kabla hajafanya. Tuepushe tusisikie jingine Mungu wetu.
 
Back
Top Bottom