Kibanda apelekwa kutibiwa Afrika Kusini

Alianza Ulimboka akaja Kibanda atakaefuta mungu amuepushe kazia hiyo

Mkuu Mungu ''alishatuepusha'' na kadhia kama hizi kwa kutupa akili za kuweza kujilinda na kujitetea tunapokumbwa na vitu kama hivi. Naomba nisieleweke vibaya kwani nia yangu ni kusisitiza umuhimu wa sisi watnzania wote kupinga na kulaani kwa nguvu zote matukio kama haya. Kwa mfano Ulimboka alipofanyiwa unyama sisi kama watanzania wenzake tulichukua hatua gani? Haya kwa Kibanda tutachukua hatua gani? Tukiamua kulialia na kusema Mungu tuepusha (wakati alishatupa akili na maarifa) haitasaidia. Tutaendelea kulizwa mmoja baada ya mwingine kama pundamilia wa kule Manyara.
 
Tumefika huko tena, tulianza kusahau ya akina Dr. Ulimboka sasa naona yameanza tena. Itakuwa life style, South Africa kila siku mbona pesa yetu itaishia huko, tujenge na kuimarisha hospitali zetu maana majuzi tu tuliona, Manumba DCI, Dr Ulimboka nk.

Wapi police na taarifa za upelezi wao jamani ama system iko down.
 
mwajiri wake ni nani? tupeni taarifa ya tukio zima alitekwa? alivamiwa? au ni nini yaani hii kitu sielewi kabisa
Muajili wake ni Rostam Aziz chini ya Mkurugenzi Mtendaji Hussein Bashe. kampuni Habari Corporation.
 
mwajiri wake ni nani? tupeni taarifa ya tukio zima alitekwa? alivamiwa? au ni nini yaani hii kitu sielewi kabisa
ni fisadi mzoefu rostam bin aziz,kibanda aliamua kufanya kazi kwa mwizi wa rasilmali za watanzania na kusema wimbo wanaoimba chadema wa ufisadi hauna mashiko na wa kishamba,huyo ndio absalom kibanda.
get well soon brother
 
Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda, kwa sasa yuko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.

Ndege imekodiwa na mwajiri wake. Hali yake si nzuri.

Tuungane kumwomba Mungu amjalie apone-arejee salama.
Ila mengine hayamuhusu mungu yapo ndani ya uwezo wa binadamu, style iliyotumika kumtesa Dr Ulimboka ndio hiyo hiyo aliyofanyiwa Kibanda, Kung'olewa meno, kung'olewa kucha na kutobolewa macho.

Tunataka kuona weledi wenu Waandishi wa Tanzania katika hili na si kusubili maigizo ya Kova na wapelelezi wake wa kufikirika.

This is the same Mafia Gang, i don't buy any other story.
 
Hivi tunapoambiwa jeshi la police linalinda raia na mali zao manake nini? Hawa police wako wapi raia wanatendewa unyama kila kukicha ktk nchi yao? Pole sana KIBANDA
 
Hivi tunapoambiwa jeshi la police linalinda raia na mali zao manake nini? Hawa police wako wapi raia wanatendewa unyama kila kukicha ktk nchi yao? Pole sana KIBANDA

polisi kumpa bodyguard kila mtanzania itakua very expensive...bajeti haitoshi.
 
hospital ya rufaa ya taifa inayotoa first aid service...inasikitisha.....sasa na zahanati zifanyeje? then serikali inapuuza madai ya kuimarisha huduma za afya na vifaa tiba ktk hospital kama hiyo yenye hadhi ya taifa.
 
Suleman kova yuko studio, kuweni wapole muda sio mrefu filamu mpya itatangazwa rasmi.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Hii filamu ni mahsusi kwa ajili ya kutuondoa katika mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne na serikali kutokuwa na mitaala ya elimu nchini kitu kinachosababisha elimu yetu kuzidi kuporomoka kila kukicha.
 
Mbona wanasema kabondwa na kitu kizito chenye ncha kali kimetoka kusiko julikana.
 
Back
Top Bottom