raiamwematz24
Member
- Dec 6, 2025
- 8
- 20
Kibamba wengi bado tunalazimika kununua maji ya chumvi
Licha ya Serikali kukiri kuwa Tanzania si masikini wa vyanzo vya maji, bado kero ya maji imeendelea kukithiri hasa kwa miji mikubwa kama Dar es Salaam.
Kero hiyo imedhihirika tena mwisho mwa mwaka 2025, kwa jiji la Dar es Salaam kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji, hali iliyowafanya wakazi wake kutaabika kuyasaka kwa gharama kubwa.
Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Jimbo la Kibamba lenye makazi mapya kutokanana ongezeko la watu, makazi mapya na shughuli za kiuchumi.
Licha ya kuwepo kwa miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wakazi wengi wa Kibamba bado wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ya bomba.
Salma Kitesi, mkazi wa eneo la matenki mawili huko Kibamba anasema ni muda mrefu maji hayajatoka, na si eneo lake tu bali maeneo mengi ya mtaa huo.
‘‘Tangu nimeweka bomba hapa nje, maji ni jambo geni, kwa sababu tunanunua wanaouza kwenye madumu kwa shilingi 500 hadi 1,000 wakati mwingine, kiukweli inatuumiza, tunakuwa kama tuko vijijini,’’ anasema Salma.
Dustan John, ni mwendesha mkokoteni anayefanya biashara ya kuuza maji kwenye madumu anadai kwake ni faida, ingawa anayapata kwa umbali mrefu hali inayolazimu kuuza kwa gharama kubwa.
‘‘Kuna wakati nauza dumu moja shilingi 700 hadi elfu moja, ukweli maeneo haya sehemu kubwa hakuna maji na wenye hayo ya chumvi pia hayatoki mara kwa mara,’’ amesema.
Mmoja wa Wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Baba Rose anasema waliwahi kwenda ofisi za DAWASA zilizopo Kibaha lakini wanachojibiwa ni kwamba mafundi wanashughulikia jambo ambalo halijawahi kuzaa matunda.
Taarifa Zaidi katika eneo hilo zilisema kuwa matangi ya maji hufungwa ili kuwezesha biashara ya maji kufanyika.
Mikakati ya Serikali
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, kwa sasa wamefikia zaidi ya asilimia 35 ya utekelezaji wa bwawa la Kidunda ambapo kufikia mwishoni wa Mwaka 2026, litakapokuwa limekamilika litatochea uzalishaji wa maji katika vyanzo mbalimbali vya maji.
Hata hivyo ripoti ya Wizara ya Maji inaeleza Bwawa la Kidunda linalojengwa Mkoani Morogoro lina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita Bilioni 190 za maji hali ambayo itaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Katika kutafuta suluhu ya kudumu, licha ya Waziri Aweso ameielekeza DAWASA kuwasha mitambo yote ya kusukuma maji ili kuondoa mgao wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani, kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha maji katika Mto Ruvu baada ya hatua za dharura kufanyika katika chanzo na mvua takribani milimita 50 kunyesha katika safu za milima ya Uluguru.
Aidha, mipango hiyo inaonesha kuwa kwa uwepo wa Mradi wa Bwawa la Maji la Kidunda linalotarajiwa kukamilika Mwaka 2026, sambamba na ujenzi wa awamu ya pili ya Mradi wa maji wa visima vya Kigamboni kuhitimisha mpango mkakati ambao tayari umefanyiwa upembuzi yakinifu wa Ujenzi wa mradi wa Maji Rufiji kutaondoa changamoto hiyo kabisa.
Akizungumza katika mahojiano katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Desemba 2025, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema Tanzania ina vyanzo vya kutosha vya maji, hivyo Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji ili kuwafikia wananchi.
Swali linaloendelea kubaki vichwani ni je, adha hii ya maji itaondoka kwa mijini tu au bado suluhu itaendelea kuwa maji ya chumvi na si ya bomba? Hapa ndipo tafakari inapaswa kutatuliwa na serikali.