Kibaka Mbinguni!

Kibaka Mbinguni!

Hmaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
346
Reaction score
86
Kuna kijana mmoja alikuwa kibaka sana hapa duniani na alipofariki na kuzikwa akatokea mbinguni. Akiwa mbinguni akakuta watu wengi wakikabidhiwa tiketi kwa ajili ya kwenda aidha peponi au motoni. Tiketi nyekundu walikuwa wakipewa wenye dhambi na zile za bluu wale wasio na dhambi kisha wanajipanga mstari mmoja hadi geti kuu ambapo hutenganishwa. Jamaa alikuwa hana furaha na hivyo akapanga kumwibia padri aliye mbele yake tiketi ya bluu ambayo aliiweka mfuko wa nyuma wa suluali yake, akafanikiwa kwa kumbadilishia na yake. Walipofika lango kuu padri alishangaa alipojikuta na tiketi nyekundu badala ya bluu lakini akajipa moyo na kuingia motoni na kibaka akaingia peponi. Kwa kawaida kila kundi huwa linaandaliwa mazingira yanayofanana na alikotoka kwa wiki kadhaa kabla ya moto au pepo, hivyo kwa upande wa wenye dhambi waliandaliwa starehe bab kubwa huku wakinywa, wakicheza miziki, wakijirusha na masuala ya ngono na anasa zote na wale wasio na dhambi waliandaliwa kwaya za kumtukuza mungu na ibada za kila wakati. Yule padri muda wote hakuwa na furaha hasa akifikiria kwa vile alinyoibiwa tiketi yake na yule kijana kibaka pia hakuwa na raha kwa vile angependa kupata starehe za upande wa pili hivyo akaamua kutangaza kwamba alimwibia ile tiketi padri kwa hiyo alitaka kumrudishia ili aende akajirushe, wasaidizi wakampa padri tiketi yake na kumwingiza peponi na jamaa akaingizwa motoni. RAHA HIZO!
 
kwani huyu Hmaster..hajui nini maana ya vichekesho...au anajifunza kutype..time waster..
 
Hakukwwambia ucheke, so huna haja ya kucheka
 
Back
Top Bottom