Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,726
- 3,739
Watu wengi wanahangaika usiku na mchana kutafuta raha na starehe za dunia hii, ambazo ni za muda mfupi, lakini hawajishughulishi kuhakikisha wanayo “tiketi” ya kuingia mbinguni kwenye raha na furaha ya milele. Labda ni kwa sababu hawajui maisha ya mbinguni yatakuwa ya namna gani. Nakutajia hapa mambo mazuri ya mbinguni. Mbinguni...
“Ee Mungu wa mbinguni, nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, lakini leo natubu kwa moyo wangu wote. Naamini kuwa Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, akafufuka ili nipate uzima wa milele. Bwana Yesu, naomba unisafishe kwa damu yako. Ninakukaribisha moyoni mwangu uwe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Nisaidie kuishi maisha mapya ya utakatifu. Kuanzia leo namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na kunipa “tiketi” ya kuingia mbinguni. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amina.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wote, tayari umeokoka na umepata “tiketi” ya kuingia mbinguni.
Ili uendelee vizuri na maisha ya wokovu, hakikisha unasoma Biblia na kuomba kila siku. Lakini pia ungana na waumini wengine katika Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha maisha ya utakatifu, watakuelekeza mambo mengine yakupasayo kufanya. Ubarikiwe sana.
- Maisha ni matamu mno. Utamu huo unafanya miaka 1000 ionekane kama siku moja tu.(2 Petro 3:8)
- Hakuna kilio wala maombolezo – Ufunuo 21:4
- Hakuna kuzeeka. Tutakuwa na miili mipya ya utukufu – Wafilipi 3:21
- Hakuna njaa wala kiu – Ufunuo 7:16
- Hakuna magonjwa wala ulemavu – Isaya 35:5-6
- Hakuna dhambi wala majaribu –Ufunuo 21:27
- Kuna furaha isiyo na mwisho – Zaburi 16:11
- Tutaishi milele. Hakutakuwa na kifo kabisa – 1 Yohana 2:25; Ufunuo 20:6; Ufunuo 21:4
- Tutaishi na Mungu na kumuona uso kwa uso – Ufunuo 22:4; Ufunuo 21:3
- Tutakuwa kama malaika, hakuna kuoa wala kuolewa – Mathayo 22:30
Kwa sababu hiyo hakuna matatizo ya ndoa! - Hakutakuwa na giza wala usiku – Ufunuo 22:5
- Hatutakula kwa jasho. Tutakula matunda, bure – Ufunuo 2:7
- Hakuna vita wala maadui – Isaya 11:9
- Tutaimba nyimbo tamu kwa lugha moja – Ezra 3:11
- Tutapokea taji za thawabu – 2 Timotheo 4:8
- Tutashiriki karamu(sherehe kubwa) ya arusi ya Mwana-Kondoo(Ufunuo 22:4). Karamu hiyo inapita mara elfu elfu karamu zote zinazofanyika hapa duniani.
- Kubali kuwa wewe ni mwenye dhambi – Warumi 3:23 – “Kwa maana wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”
- Amini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka –Warumi 10:9 – “Kwa sababu ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”
- Tubu dhambi zako kwa moyo wa dhati na usitende dhambi tena – Matendo 3:19 – “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.”
- Mpokee Yesu moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako – Yohana 1:12 – “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake.”