Khatib ataka mrithi wa JK atoke Z'bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Khatib ataka mrithi wa JK atoke Z'bar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Apr 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib amependekeza mgombea wa kiti cha urais atakayemrithi rais wa sasa Jakaya Kikwete, atoke visiwa vya Zanzibar.

  Waziri Khatib alitoa pendekezo hilo jana, siku ambayo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa unatimiza miaka 46 tangu waasisi wa mataifa haya mawili, Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, walipotekeleza ndoto zao za kuungana.

  Hata hivyo, Muungano huo unaonekana kuongezeka kasoro licha ya serikali kuweka vyombo vya kughulikia kupunguza kero zilizopo.

  Waziri Khatibu, ambaye anatajwa kuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) kinachorushwa hewani kila siku kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 2:00 asubuhi.

  Waziri huyo, ambaye hajakanusha tuhuma hizo akitaka watu wasubiri muda utakapofika, alisema jana kuwa kuwa katika kuongoza nchi, ni vema kukawa na utaratibu wa zamu baina ya Wazanzibari na Watanzania Bara unaotambulika kikatiba.

  “Kwa sasa hatuna utaratibu huo wa kuongoza nchi kwa zamu, lakini ni vema tukawa na utaratibu huu wa kupokezana,” alisema Waziri Khatib bila kueleza hili litasaidia nini.

  Kwa mujibu wa Khatib, katiba ya sasa imeweka zamu katika nafasi ya makamu wa rais pekee, ikieleza kuwa kama rais atatoka Tanzania Bara, makamu wake lazima atoke Zanzibar na kama atatoka Zanzibar, makamu atoke bara.

  “Ni vizuri viongozi wetu wa kisiasa waliopo madarakani hivi sasa wakawaandaa vijana wazuri kwa ajili ya nafasi ya urais, ili muda ukifika tusipate tabu,” alisema Waziri Khatib.

  “Pamoja na kwamba ni vema tukawa na zamu za kutawala nchi yetu, tuna kila sababu ya kuhakikisha tunapata viongozi wazuri, walioandaliwa na wenye uwezo wa kuongoza.”

  Hadi sasa ni Ali Hassan Mwinyi, aliyeongoza serikali ya awamu ya pili, ndiye Mzanzibari pekee aliyewahi kuwa rais wa Serikali ya Muungano baada ya kuongoza nchi kutoka mwaka 1985 hadi 1995 wakati kulipofanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

  Waziri Khatib asema: “Ni jambo jema kuwa na zamu za kuongoza nchi baina ya pande mbili za Muungano, lakini hatulazimishi iwe hivyo kwa sababu halipo kikatiba kwa sasa.”

  Alisema kwa sasa serikali inafuata katiba katika kupata wagombwea urais, lakini kama katiba itafanyiwa marekebisho leo na kuweka zamu za kuongoza nchi, basi serikali haina budi kufuata katiba hiyo.

  “Kama katiba itafanyiwa marekebisho leo na kuweka utaratibu wa zamu wa kuongoza nchi basi sisi serikali na chama tutafuata katiba, lakini kwa sasa sual hilo halipo kikatiba,” alisema Waziri Khatib.

  Waziri Khatib anaweza akawa waziri wa kwanza ndani ya serikali ya Muungano kutoa pendekezo la namna hiyo, ambalo kimsingi linaweza kuibua mjadala mpya.

  Waziri Khatib pia alikiri kuwa kuna matukio mbalimbali yaliyosababishwa na kero za Muungano na hivyo kuutikisa, hata hivyo, alisema Muungano bado ni imara.

  Akitaja matukio hayo, waziri Khatib alisema ni pamoja na lile la wabunge waliotaka serikali tatu, kundi lililojulikana kama G55 na kujiuzulu kwa aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, ambaye alikuwa makamu wa rais na makamu mwenyekiti wa CCM.

  “Unajua Zanzibar ilipita katika kipindi cha vuguvugu la kisiasa na ikashutumiwa kuwa, mheshimiwa Aboud Jumbe alikuwa katika mpango wa kuanzisha serikali ya tatu ndani ya muungano, kwa hiyo baada ya kikao cha chama kilichofanyika CBE Dodoma, akasema anawajibika kwa kujiuzulu,” alisema Khatib.

  “Lakini pia hatuwezi kusahahu malumbano na mijadala mikali ambayo ilihatarisha Muungano baina ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu hoja ya hadhi ya Zanzibar na suala la mafuta,” aliongeza Waziri Khatib.

  “Mtukio haya yalitikisa sana Muungano wetu, lakini tunashukuru pamoja na misukosuko hiyo bado muungano upo imara.”

  Kuhusu utatuzi wa kero za Muungano, Khatib alisema wamefikia mahali pazuri na kwamba hadi sasa tayari mambo makubwa matatu yameshatafutiwa ufumbuzi.

  “Moja ni Sheria ya Uvuvi ambayo makao makuu yake ni Zanzibar, biashara ya meli na Sheria ya Haki za Binadamu; haya ni mambo matatu makubwa katika kero za Muungano ambayo tumeyafanikisha,” alisema Waziri Khatib.

  Hata hivyo alikiri kuwapo kwa kero nyingine nyingi, likiwemo suala la mgawanyo wa mapato na uchangiaji baina ya Bara na Visiwani.

  Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema amesema utaratibu wa kupokezana uongozi kwa zamu si mbaya, lakini usiwekwe kikatiba.

  “Tangu Muungano ulipoasisiwa, misingi tuliyowekewa na waasisio ni kupatikana marais kwa utamaduni wa mapenzi na makubaliano na sio kikatiba,” alisema Mrema.

  Alisema Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walikubaliana kwa mapenzi tu kwamba Nyerere awe rais na Karume awe makamo.

  “Wala Karume hakusema kwamba awamu inayokuja mimi ndio niwe rais. Mimi nadhani ni utamaduni mzuri, tunaweza kupeana zamu za kuiongoza lakini isiwe kitu cha kikatiba,” alisema Mrema.

  Alisema hatari ya kuweka utaratibu huo katika katiba ni uwezekano wa kupata viongozi wasio na uwezo na hivyo kusababisha migogoro ndani ya nchi.

  “Nadhani waziri angesema kama kuna matatizo ya msingi katika Muungano, lakini tusitafute visingizio tu,” alisema Mrema.

  Hata hivyo mwenyekiti Mwenza wa Mpango wa Utafiti wa Maendeleo ya Demokrasia nchini (REDET), Dk Benson Bana alisema wazo la Waziri Khatib si zuri kwa kuwa linaweza kuligawa taifa.

  “Katika urais tunapima uwezo wa mtu na hatuangalii rangi, dini, kabila wa eneo la mtu. Tusijali mazingira anayotoka; tunaangalia ‘vision’ (dira) na uwezo wa mtu hata kama anatoka Pemba au Bukoba tunampa urais,” alisema Dk Bana.

  “Hii ya waziri italigawa taifa, sisi sote ni Watanzania na tumeshatoka katika ubaguzi wa kikabila, kikanda, kidini na hata rangi wala hatuwezi tena kurudi nyuma tulikotoka,” aliongeza Dk Bana.

  “Mimi nadhani inatosha hii ya kupokezana katika nafasi ya umakamu, yani kama rais atatoka bara makamu wake awe Mzanzibari na kama rais atatoka Zanzibar basi makamu wake atoke Tanzania Bara,” alisema Dk Bana.

  Chanzo:
  Mwananchi
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zanzibar ni NCHI. Raia wa nchi nyingine ataitawala vipi Tanzania? Zanzibar wana bendera yao, wimbo wao wa TAIFA, wana majeshi yao kama KMKM, JKU,....Wanataka wawe na marais wangapi?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa mayakhe wa Visiwani wanachekesha kweli kweli! Katika mchakato wa uteuzi wa urais mwaka 2005 kulikuwapo mgombea mmoja wa urais wa muungano ambaye alikuwa very strong, lakini hao hao mayakhe walimfanyia fitina na ghilba kubwa hadi akaukosa uteuzi. Sasa hivi wanataka nini?

  Hebu fikiria: Kwa hali ya kawaida huwa ni sifa kubwa kwa upande mdogo wa muungano (muungano wowote ule) kutoa Rais. Lakini hawa wenzetu wa visiwani hawako hivyo. Mwaka 2005 waliona kuwa ni bora upande wa Bara wakaendelea tu kutoa marais, 'sisi huku hatuna tatizo na hilo.'

  Ni watu wa ajabu kweli kweli. Itachukuwa miongo mingi sana kabla Wavisiwani kupata mgombea strong kama yule wa 2005.
   
 4. bona

  bona JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  kuna mkristo zenji? maana urais tunapokezana waislam then mkristo, akitoka kikwete obvious rais ajae lazima awe mkristo so nafasi ya zenji kutoa mrithi wa kikwete inazidi kua finyu kwa ukweli kwamba zenji hakuna mkristo mwanasiasa wa kuja chukua nafasi iyo!
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I don't believe in alternating between religions, regions or Zanzibar and Tanzania mainland. What we need is good leaders be it from any part of the Union. This saying that a certain person should be president simply because he comes from one part of the Union is stupid. It will show weakness in the part of Zanzibar if they need to be given a turn to govern. Like Khatib said, Zanzibar should prepare good leaders who can become president then they won't have to worry about who's turn it is to be president.

  Also this policy of alternation doesn't seem practical for a multi party state. So if this becomes law opposition parties will also be forced to chose a person from one side of the Union to run for president? What if their best candidate is from the part whose turn is not to produce a president? We want to build a stronger union but we are finding more ways of people saying "Mimi Mtannzania bara, mimi Mzanzibari".
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  What you are suggesting is dangerous. It doesn't matter what religion a person is. When will we learn to chose leaders by merit and not this stupid classification of regions and religion. As long as everybody is given an equal opportunity to run for office these other things don't matter!
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  That's what I don't get. In 2005 they had a legitimate chance of putting a Zanzibari into power democratically without this petty favoritism that Khatib wants put in the constitution. They had a man who arguably had the best CV among all candidates be it from mainland or Tanzania with positions like ambassador, minister and prime minister under his belt. So to me it is strange that Khatib is advocating for this while they don't need it to put a Zanzibari into the state house. Unless Khati himself has his own political ambitions and wants a clear path for himself in 2015.


  What is funny is that they weren't talking about alternating in 2005 when Zanzibar had the best qualified candidate. Now when it seems that they have no likely strong candidate (thus far) a person like Khatib is trying to advocate it. If they really wanted alternation between Mainland and Zanzibar to be precedent they had a chance to push for it in 2005.
   
 8. M

  Mndamba Member

  #8
  Apr 27, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Na huyu Mheshimiwa ni Senior Minister. Hebu angalia mawazo yanayotoka kwake. Alikuwa wapi 2005???. Watu wengine mawazo yao ni ya hovyo kabisa. Au anataka kutuaminisha kwamba yeye atakuwa better kuliko SMS.
   
 9. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sio sahihi kusema kwamba urais wa URT unapokezana kati ya waisilamu na wakristo. Imetokea hivyo kibahati tu haijawekwa KIKATIBA. Watanzania tunataka rais mwenye sifa na anayefaa kuiongoza Tanzania atakayeaminiwa kwanza na chama chake halafu watanzania watampigia kura bila kujali ametoka sehemu gani ya Tanzania na wala bila kuajali ni wa dini gani. Hakuna swala la UDINI katika kumpata rais wa Tanzania.
   
 10. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Hawa Wazanzibari naona wanataka kubebwa sana, wanadhani uraisi ni kupokezana kama kopo la mbege??? Waache kulialia bwana, wajipange mwenye sifa atachaguliwa na wananchi na siyo kupokezana kama wanAVYODHANI. eti kwa sababu ya Muungano. Wanataka kila kitu 50/50, mbona walipoambiwa tu kuwa Huko zanzibar kuna mafuta wakaanza kulia eti suala la mafuta si la muungano. Hata hivyo si wanaye raisi wao kwani huyo hatoshi??? Walilia bendera wakapewa, wakalilia wimbo wa kataifa kao wakapewa (Japokuwa huku kwetu bara tunakaita Ka-mkoa) Sasa wanalilia Uraisi, Kesho watataka na kingine. Waache kudeka kihivyo eti kisa MUUNGANO. Nasi bara tutakapoanza kudai haki za taifa letu Tanganyika si itakuwa Mshike mshike! Waachane na huo U-ZANZIBARI wao unawaponza, wachukue U-TANZANIA utawasaidi na kuwapunguzia kudeka!!!!!!
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Apr 27, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Huyu uroho wa madaraka utamuua

  Ok,yaani hakuna hoja ya maana aliyoleta hapo.Haoni kwamba sasa tutakuwa tunajiwekea limit ya kupata viongozi wazuri merely because kuna uzanzibari na utanganyika? Huyu ni tamaa ya madaraka tu ndiyo inayomsukuma na ni mtu hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,424
  Trophy Points: 280
  nachelea kuwaita huyu jamaa khatib..hajatumia akili...

  nilipata kusema hapa sio siri ..zanzibar walipoteza nafasi ya kutoa rais mwaka 2005 ...pale walipoamua kama bloc kumpigia kura kikwete..akapita ....na kuamua kumtosa mzazibar SALIM AHMED SALIM...ambaye anakubalika sana ...

  pale chimwaga..wajumbe wa zanzibar wangeamua kumpa kura zao SALIM basi angemwacha kikwete mbali au wangerudia....
  kwani salim siku ile alipata kura almost 550...kikwete kura 940 ...na mwandosya 300..what happened ni kuwa kura 550 alizopata salim alipewa na wajumbe wa bara....tuseme mwaka 2005 kwa kura za bara salim na jk walipata kura sawa....alichomzidi mwenzake kikwete ni fitna...zilizopenyezwa na mtandao zanziba hadi wakaja kupiga kura chimwaga kwa kuapizana salim asipite[meneno mengii ooh hizbu..,etc]...wajumbe wa zanzibar walikuwa wanakaribia 500 na kura zao ndizo zilizomvusha kikwetee ......

  sasa leo huyu ghatib ..ndio anakuja na upupu gani ....eti wakati waliikataa fursa yao mwaka 2005...kwa ajili ya ubaguzi wao...haya maneno akaongelee ******...aone aibu!!!

  sioni candidate zanzibar anayeweza kukubalika huku kwetu hasa kwenye siasa za ushindani,..zaidi ya salim...na sioni kama kati ya miaka 20 ijayo kwa wanasiasa wenye miaka 25 kwenda juu toka zanzibar...sioni hata mmoja ambaye anaweza kuwa presidential material ......miaka 20 mbele...hata huyo salim ambaye anapendwa bara ....alianza kuonekana anafaaa kuwa rais tangu miaka zaidi ya 25 iliyopita!
   
 13. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #13
  Apr 27, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi sielewi huu utalatibu wa rais ambao tayari ulisha vunjwa nakumbuka wakati wa Mwalimu kulikua na utaratibu ya kua Rais ktk kipindi chafulani akitoka bara na kipindi kifuatacho atoke visiwan

  Naamini ya kuwa rais asichaguliwe kwa vigezo anatoka wapi bali kwa uwezo wake naamini kama haya yangezingatiwa tungelikua na Rais Salim Ahamed Salimu na sio huyu msanii au Vasco Da gama JK/ labda kwa Tanzania bara tuwe na utaratibu ya kua Rais awe anabadilishwa kimkoa JK toka pwani afuatae atoke Morogoro n.k

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Chogo wewe vipi ? Waliofanya hivyo ni kikundi kidogo kisicho na ridhaa ya wengi (CCM). Iwejeuseme Wazanzibari ndio walioamuwa na hata hivyo huu ulikuwa usaliti wa Bara si nyie mliokuwa wazi hadi vyombo vya habari kuwa mgombea huyo ni Mwarabu si Mtanzania?
  Iwapo hili jambo likiwekwa Kikatiba si nyie na utashi wenu wala si wachache (CCM) watakaofanya ufisadi.
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Trivial issues mnavifanya vya maana na kuondowa vilivyo vya maana Muungano ni Zanzibar na Tanganyika sio Uislamu na Ukiristo!
   
 16. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hapa naona amejieleza wazi kuwa uroho wa madaraka umemmaliza akili. Mawazo finyu namna hii sijapata kutegemea yatoke kwa waziri wa siku nyingi kama Khatib. Hana vision kabisa, na hawa ndiyo unakuta wanachaguliwa kutuongoza Tanzania kwa sababu ya mfumo mzima wa kuchaguana kwa makundi ndani ya CCM. Wakati huo viongozi wenye mawazo kama haya wakiwa ikulu nchi inazidi kudidimia tuu. Kiongozi kama huyu akiingia pale Ikulu atakachofanya ni kufunga ndoa mbili za haraka haraka mieizi sita ya mwanzo. Kwanza kwa mawazo haya na Wizara anayoongoza, inaonekana wazi yeye ndiyo chanzo cha migogoro mingi ya muungano. Lakini yeye anadai kuwa kaimaliza au anaimalizia maana muungano ni imara. Hawa ndiyo viongozi ambao wa-Tanzania tunategemea watuongoze tuweze kuendelea kweli? Hivi amepewa nafasi TBC kweli na ikawa hewani? IT'S A SHAME! Sasa yetu macho si tunasema walikosea 2005? Huenda huu ndiyo mwendo wanatuandaa kushangaa maana hao wakwao 500 wote wakimuunga mkono na wachache wengine bara, ambao najua wapo kwa sababu nyingine ambazo sina nia ya kuzitaja hapa, huyu tunaweza kuta kaingia Ikulu. Watch out!! Ni haruzi tupu kule Ikulu!!
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Unapoingia Makubaliano na mtu huwa kunahitajika makubaliano yenye matakwa ya pande mbili. Hili la kujifikiria binafsi ni utamaduni wenu watu wa Bara na ndio tatizo kubwa kwa Muungano.

  Hivyo katika Historia ya Tanzania nani kaleta maajabu kwenye Urais na nini kigezo halisi tulivyotumia kuamuwa uwezo wa Marais wetu? Naona hadi sasa kila anaekuja ni failure kuliko anaepita, sasa huu uwezo unaotaka wewe ni upi hata katika kipindi cha upande unaohusika akosekane mtu wa kuwa Rais?
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wabongo wana sifa ya kutwist mambo! Hebu rudi nyuma uangalie kuchaguliwa kwa Karume at the expense ya uamuzi wa Wazanzibari. Jawabu linaonekana wazi na badfala yake mnalaumu Wazanzibari. Si mlimchaguwa Karume makusudi kwa kujilinda na mwaka 2005, na matakwa yenu yalifanikiwa. Msijifanye Werevu na kuwaona Wazanzibari wajinga. Suwala hapa ni kuwa kwa vile Zanzibar ni koloni lenu basi mtaamuwa mtakavyo na baadae kuleta visi
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nani kaji fikiria binafsi? Kusema nataka raisi anayefaa regardless ya upande gani wa muungano anaotoka ni ubinafsi? Mimi I don't mind kuongozwa na hata maraisi wanne mfululizo kutoka Zanzibar shida yangu ni raisi apatikane regardless ya geography.

  Kuhusu makubaliano basi nitajie ni wapi kwenye makubaliano ya Muungano ambapo wali kubaliana ni lazima raisi akitoka upande huu basi ajae atoke upande mwingine? Maana kila sik nyie mnaongea kukiukwa makubaliano haya basi onyesha ni wapi wali kubaliana hicho anacho pendekeza khatib.

  Na kama unavyo sema ni ukweli, kuwa at any given point hakuwezi kukosekana mtu anaye weza kuwa raisi kutoka upande wowote ule what is exactly your argument? Kama mtu hawezi kukosekana basi kwa nini asijitokezee pamoja na wengine? Au mpaka tuseme kabisa leo ni zamu ya Zanzibar ndiyo wata jitokeza? Bila hivyo hawa jitokezi?
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wewe ndiyo una twist mambo. Raisi wa Zanzibar ni lazima awe Mzanzibari so how can you compare that kwenye mada iliyopo? Jibu swali, Salim hakuwekewa zengwe na Zanzibar 2005 or not? Tuongelee hoja ya huyo huyo Salim kwanza since yeyendiyo ana correlate na hii mada kisha tuje kwa huyo Karume.
   
Loading...