Elections 2010 Khatib ataka mrithi wa JK atoke Z'bar

HUYU WAZIRI ASEME BAYANA TU,URAIS TUPOKEZANE TANZANIA BARA NA UNGUJA NDIPO NITAMWELEWA HAWA SI WALIMKATAA SALIM KISA MPEMBA ATI NI HIZBU,WALINIUZI KWELI KIPINDI KILE.SASA KWA KUWA HAMJUI KUCHAGUA TULIENI,TUTAWACHAGULIA RAIS AJAE NA ATAPITA TU HATA KWA VIBOKO.[udogo wa kichwa ni kufubaa kwa ubongo ndio maana hamna vichogo nyie]
 
Hii ndiyo tafsiri ya uongozi kwa baadhi ya watu tunaodhani ni mawaziri. Uongozi kwao ni mambo ya maslahi zaidi, kwamba wanaopata maslahi hayo ni wabara, kwa hiyo itamkwe wazi wazanzibari watapata lini. Huyu ni mmoja tu ambaye ameongea hadharani, hakika yawezekana ni mawazo ya watu wengi kwenye hilo baraza la mawaziri, kwamba Urais ni kukaa na kuchekacheka, na kufaidi, hali kadhalika uwaziri ni sifa tu. Hapa ndio tatizo letu lilipo, mara nyingi watu hawaangalii uwezo wa utawala na akili ya mgombea, wanamweka mtu ambaye atatekeleza maslahi yao, kuwapa vyeo, na kuwafanya wawe juu ya sheria, hii ndiyo CCM. Kwa mtaji huu hatuwezi kufika mbali. Ni lazima ifike mahali tuchoshwe na huu upunguani na kuwaweka watu tunaodhani wanaweza kutupeleka mbele kimaendeleo.
 
Chogo wewe vipi ? Waliofanya hivyo ni kikundi kidogo kisicho na ridhaa ya wengi (CCM). Iwejeuseme Wazanzibari ndio walioamuwa na hata hivyo huu ulikuwa usaliti wa Bara si nyie mliokuwa wazi hadi vyombo vya habari kuwa mgombea huyo ni Mwarabu si Mtanzania?
Iwapo hili jambo likiwekwa Kikatiba si nyie na utashi wenu wala si wachache (CCM) watakaofanya ufisadi.


HUYU WAZIRI ASEME BAYANA TU,URAIS TUPOKEZANE TANZANIA BARA NA UNGUJA NDIPO NITAMWELEWA HAWA SI WALIMKATAA SALIM KISA MPEMBA ATI NI HIZBU,WALINIUZI KWELI KIPINDI KILE.SASA KWA KUWA HAMJUI KUCHAGUA TULIENI,TUTAWACHAGULIA RAIS AJAE NA ATAPITA TU HATA KWA VIBOKO.[udogo wa kichwa ni kufubaa kwa ubongo ndio maana hamna vichogo nyie]
 
Kwani Mwinyi alitokea wapi? Mi naungana nao wote wanaofikiri kuwa issue hapa si upande gani mtu anatoka, au dini gani mtu aliyenayo ili aweze kuwa Rais. Tunataka Rais atakayepeleka mbele gurudumu la Utanzania na maendeleo yake. Haya mambo yakulazimisha mahali na kabila na dini ili mtu awe kiongozi, tutakuja kufanya makosa makubwa sana. Mwenye uwezo popote pale alipo aje awe rais.
 
Je, mgombea kutoka bara anaweza kugombea urais Zanzibar? Mbona sasa hivi hao wenyewe Wazanzibari wana sera za kujitengatenga (mafuta, uanachama wa FIFA, sovereignity, bendera yao, wimbo wao wa taifa, vitambulisho vyao, n.k).
 
Nadhani mawazo ya huyu Seif Khatib ni ya mtu mwenye maradhi kwahiyo tumsamehe!! Mwaka 2005 alikuwa mbele kabisa kumpinga mzanzibari mwenzie asipate urais kwa kutumia hisia zao za kibaguzi, ati leo ndio analeta hoja kama hii!!
 
Nadhani mawazo ya huyu Seif Khatib ni ya mtu mwenye maradhi kwahiyo tumsamehe!! Mwaka 2005 alikuwa mbele kabisa kumpinga mzanzibari mwenzie asipate urais kwa kutumia hisia zao za kibaguzi, ati leo ndio analeta hoja kama hii!!

Ukweli mtupu..hawa jamaa wanafiki sana..
 
kuna mkristo zenji? maana urais tunapokezana waislam then mkristo, akitoka kikwete obvious rais ajae lazima awe mkristo so nafasi ya zenji kutoa mrithi wa kikwete inazidi kua finyu kwa ukweli kwamba zenji hakuna mkristo mwanasiasa wa kuja chukua nafasi iyo!

Huko unakotaka kutupeleka siyo kwenyewe
 
Hii kauli ya Khatibu inamdisqualify kabisa kuwa kiongozi. Huyu dogo anaropoka sana halafu anajiona mtetezi wa Wazanzibar sana - actually he is after cheap popularity.
 
kuna mkristo zenji? maana urais tunapokezana waislam then mkristo, akitoka kikwete obvious rais ajae lazima awe mkristo so nafasi ya zenji kutoa mrithi wa kikwete inazidi kua finyu kwa ukweli kwamba zenji hakuna mkristo mwanasiasa wa kuja chukua nafasi iyo!
Nani kasema udini ni burgaining chhip yet Tz, tusifikishwe huko mkuu wangu hata Khatibu kidogo ameteleza ila kidogo inazungumzika
 
kuna mkristo zenji? maana urais tunapokezana waislam then mkristo, akitoka kikwete obvious rais ajae lazima awe mkristo so nafasi ya zenji kutoa mrithi wa kikwete inazidi kua finyu kwa ukweli kwamba zenji hakuna mkristo mwanasiasa wa kuja chukua nafasi iyo!

...Wengi tu yakhe.
 
Hawa mayakhe wa Visiwani wanachekesha kweli kweli! Katika mchakato wa uteuzi wa urais mwaka 2005 kulikuwapo mgombea mmoja wa urais wa muungano ambaye alikuwa very strong, lakini hao hao mayakhe walimfanyia fitina na ghilba kubwa hadi akaukosa uteuzi. Sasa hivi wanataka nini?

Hebu fikiria: Kwa hali ya kawaida huwa ni sifa kubwa kwa upande mdogo wa muungano (muungano wowote ule) kutoa Rais. Lakini hawa wenzetu wa visiwani hawako hivyo. Mwaka 2005 waliona kuwa ni bora upande wa Bara wakaendelea tu kutoa marais, 'sisi huku hatuna tatizo na hilo.'

Ni watu wa ajabu kweli kweli. Itachukuwa miongo mingi sana kabla Wavisiwani kupata mgombea strong kama yule wa 2005.
tena walimsinvizia kuwa ni mwanachama wa HIZBU
 
Kwanza katiba hairuhusu na hata kama itapitishwa kwenye katiba bado itapingana na katiba yenyewe. Iwapo mtu anataka kugombea mwaka huu atazuiliwaje kisa tu last president alitokea upande mmoja wa Muungano. Hizi ni ajenda zake ili apate kitu cha kuongea iwapo atagombea Zanzibar. Rais anatakiwa achaguliwe kwa merits siyo kwa kutazama katoka upande gani wa Muungano. Propaganda za wanasiasa kama hawa ndiyo zinazoongeza chokochoko katika muungano
 
nachelea kuwaita huyu jamaa khatib..hajatumia akili...

nilipata kusema hapa sio siri ..zanzibar walipoteza nafasi ya kutoa rais mwaka 2005 ...pale walipoamua kama bloc kumpigia kura kikwete..akapita ....na kuamua kumtosa mzazibar SALIM AHMED SALIM...ambaye anakubalika sana ...

pale chimwaga..wajumbe wa zanzibar wangeamua kumpa kura zao SALIM basi angemwacha kikwete mbali au wangerudia....
kwani salim siku ile alipata kura almost 550...kikwete kura 940 ...na mwandosya 300..what happened ni kuwa kura 550 alizopata salim alipewa na wajumbe wa bara....tuseme mwaka 2005 kwa kura za bara salim na jk walipata kura sawa....alichomzidi mwenzake kikwete ni fitna...zilizopenyezwa na mtandao zanziba hadi wakaja kupiga kura chimwaga kwa kuapizana salim asipite[meneno mengii ooh hizbu..,etc]...wajumbe wa zanzibar walikuwa wanakaribia 500 na kura zao ndizo zilizomvusha kikwetee ......

sasa leo huyu ghatib ..ndio anakuja na upupu gani ....eti wakati waliikataa fursa yao mwaka 2005...kwa ajili ya ubaguzi wao...haya maneno akaongelee ******...aone aibu!!!

sioni candidate zanzibar anayeweza kukubalika huku kwetu hasa kwenye siasa za ushindani,..zaidi ya salim...na sioni kama kati ya miaka 20 ijayo kwa wanasiasa wenye miaka 25 kwenda juu toka zanzibar...sioni hata mmoja ambaye anaweza kuwa presidential material ......miaka 20 mbele...hata huyo salim ambaye anapendwa bara ....alianza kuonekana anafaaa kuwa rais tangu miaka zaidi ya 25 iliyopita!

Una uhakika gani kuwa waliomtosa 2005 walikuwa Wazanzibar...? Umesema CCM-ZNZ walikua 500..hata kama wote wangemchagua wasingeweza kumpitisha ...!!!
Salim alitakiwa achaguliwe na wote...Usiwatie waznz kimavi...Wakati wote CCM yote ilishiriki kumsulubu Salim....!!!

Unaposema huoni znz kuwa na presidential Materials in the next 25yrs....?How...? Hii ni kauli ya Dharau brother....Nani alimfikiria Mkapa kuwa RAIS...? km si Nyerere peke yake...?

Let us discuss FACT...Hapa tunazungumzia Katiba ya CCM au Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa TZ.???? Wazanzibar kama wameona wamechezewa Rafu 2005 za kubadilisha katiba sasa wameamka na wanataka fare play...!!! na Hizi kauli za akina Philimone ati haoni anaefaa kuwa Rais hadi after 25yrs..ndio ambayo inachochoea waznz kuweka madai yao mbele....!!! Hivi ni Nani Mainland anaefaa kuwa RAIS after JK...? mie kwasasa simuoni....!!!
 
Je, mgombea kutoka bara anaweza kugombea urais Zanzibar? Mbona sasa hivi hao wenyewe Wazanzibari wana sera za kujitengatenga (mafuta, uanachama wa FIFA, sovereignity, bendera yao, wimbo wao wa taifa, vitambulisho vyao, n.k).

Mzee Mwinyi ametokea Mkuranga na yeye alikuwa Rais wa Zanzibar.
Na mwanawe alikuwa mbunge wa Mkuranga na sasa hivi kuna tetesi anataka kugombea urais wa Zanzibar.
 
...Wengi tu yakhe.

Mkuu si mchana, ni adhuhuri. Huyu Khatibu ni mpuuzi sana au anajiona yeye ndiye anafaa kuwa rais? ikiwa ni kwa kupokezana basi ni zamu ya wapemba Rais awe mpemba na makamu atoke bara.

Hivi huyu Khatibu alimuunga mkono Salim?
 
Kwa nini tusiangalie kwanza muundo wake?Nchi gani mbili zimeungana alafu kukawa na marais wawili? nasikia hata mikataba waliyosaini Mwalimu na Karume haipo,sijui ilienda wapi? ilikuwa inasemaje? hakuna reference ndo maana leo ni mvurugano tu,mara mafuta yakipatikana ni huku,madini ni ya kwetu tu,Rais atoke huku,na sisi tunaanzisha wimbo na bendera zetu.Na mbona gharama ya kuziendesha hizi serikali mbili ni kubwa mno?mambo yangekaa sawa si wafanyakazi wangelipwa hata laki nne! achana na hizo tatu na nusu ambazo hawatazipata hata wakigoma miaka nane!

Mi naona kwa sababu viongozi wetu wameshindwa kukaa chini na kutatua matatizo ya msingi(pamoja na kuanzishwa kwa wizara ya muungano),huu muungano tuuvunje tu! tuanze na moja tukifuata zile taratibu za kutengeneza muungano wa kiuchumi maana tumekimbilia wa kisiasa umetushinda.
 
Back
Top Bottom