mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,843
- 3,128
Hivi Mbowe alipo pokea mlungula wa Lowassa, aliwatoa?. Au mnapiga propaganda free kwa kua nyie hamjui matumizi ya pesa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Ok tukubali kuwa cdm imempokea fisadi mmoja yaani lowasa ,ccm wamebaki wafisadi wangapi? Cdm ndiyo pekee inatakiwa kuwa watakatifu? Nyie ccm mnapoteza muda kuwadanganya watz, mnafikiri tumesahau list of shame?Hivi Mbowe alipo pokea mlungula wa Lowassa, aliwatoa?. Au mnapiga propaganda free kwa kua nyie hamjui matumizi ya pesa?
Sent using Jamii Forums mobile app
mshindi wa nini? hicho kichwa usifugie nywele
Huu mgogoro unaofukuta ndani ya CUF kwa ugomvi kati ya Katibu Mkuu halali wa CUF Mhe. Maalimu Seifu na Mwenyekiti fake Prof(njaa) Haruna Lipumba umelenga kuimaliza CUF kisiasa.
Kwa msaada wa Serikali na vyombo vya ulinzi na Usalama CUF halali lazima iangamie ili isiendelee kuisumbua CCM ya Serikali ya Awamu ya 5. Figisu zote zinazoendelea lengo ni Maalimu Seifu na lazima amalizwe kisiasa kabla ya 2020!!
Serikali wanajua kabisa kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Maalimu Seifu alishinda kwa kishindo na kama Uhuru,Haki na Demokrasia ya kweli vingetamalaki na kuzingatiwa na ZEC hivi leo Maalimu Seifu angelikuwa yuko Ikulu ya Zanzibar akiongoza Visiwa vya Marashi ya Pemba.
Kwa hali inavyoelekea imebakia kete moja tu kwa Maalimu Seifu ambayo itamwokoa kisiasa nayo ni KUANZISHA CHAMA KIPYA CHA SIASA. Lazima CUF halali wajifunze kwa Wapinzani Kenya kina Raila Odinga, William Ruto, Uhuru Kenyata na wengineo. Kwamba jina la Chama sio hoja. Leo hakuna KANU tena wala ODM badala yake tuna JUBILEE na NASA na siasa zinakwenda! Jambo la msingi hapa ni WATU au UMMA ulio nyuma yako. Nina hakika kama Maalimu ataondoka leo na kuachana na CUF ambayo Lipumba ameamua kuisambaratisha na kuunda Chama kingine kwa Jina lolote kwa ajili ya kuwakomboa Wazanzibari na Wazanzibara toka utawala kandamizi wa CCM umma wote utakuwa nyuma yake.
Kwa kufanya hivo Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watakuwa wamepoteza uanachama wa CUF kama wale wa kuteuliwa(Special Seats) walivyopoteza juzi baada ya kutimuliwa na CUF ya Lipumba. Kitakachofuata ni Tume ya Uchaguzi kuitisha Uchaguzi na Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watarudi Bungeni kwa jina la Chama kipya na ushindi mkubwa. Kwa mtaji huo CUF ya Lipumba watakuwa hawana Wabunge wa Kuchaguliwa na kwa mantiki hiyo hawatakuwa na Wabunge wa Viti Maalumu na hawatakuwa na RUZUKU tena.CUF watabaki na Lipumba na Sakaya na ndiyo itakuwa hitima ya CUF Tanzania.
Wateule,
Umechangia kwa umakini kiasi kwamba umenishawishi nikubaliane na wewe kwa Maalimu kujiunga na CHADEMA.
My question is: Je, Maalimu Seifu na Waunguja na Wapemba watakuwa tayari kuhamia CHADEMA? Lakini pia tusisahu kuna sumu au dhana moja potofu sana ilishajengwa kuhusu Udini kwenye vyama vya siasa!!. Kwamba CHADEMA ni chama cha Kikristo na CUF ni chama cha Kiislamu. Sasa kwa watu ambao hawasomi katikati ya mistari kwa ndugu zetu wa Visiwani wakisikia Ukristo basi wanajua ni kuingilia imani zao na hii inawatoa nje!
Itakuwa ni wakti mwafaka sasa kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA kukaa na Maalimu, kina Salim Mwalimu kuwaelimisha Wazalendo wote walioko Visiwani ili waelewe hilo somo na wajue adui yao ni nani. Ukristo ni just DINI wala haina issue kwenye Politics. Adui namba 1 wa Wazanzibar ni CCM na huyu ndo anatakiwa ashambuliwe toka kona zote ili kumsambaratisha kama KANU ya Moi ilivyopotea huko Kenya!!!
Acheni kuwapotosha wana CUF kwa janja janja. Infact hiki kitu ndo CDM miaka yote wanaomba kitokee ili wajijenge Kisiasa Zanzibar sehemu ambayo hawakubaliki hata na panya. Kwa maalim kujiunga na CDM ni kujimaliza kabisa kisiasa na kuipa nguvu mpya CDM. Kwa ushawishi alionao maalim ni mara mia akaunda chama chake kuliko kujitumbukiza kwenye genge la wafanyabishara wanaowaza kuongeza ruzuku kila siku.Mzalendo 2015,
Wapo kweli namba ya Wazanzibari wanaoamini hivyo. Lakini, hizi propaganda za udini (na pacha wake "amani") zinakuzwa zaidi na CCM ili kuwapunguzia CUF na upinzani kwa ujumla nguvu ya kuwapa wafuasi.
Kama Seif, atahamia CHADEMA kama tulivyoshauri hapa, basi nina imani kabisa hizo propaganda za udini hazitofua dafu, na Wazanzibari watakuwa tayari kumuunga mkono Seif kwa maslahi ya nchi yao ambayo imegeuzwa koloni la CCM (wala sio la Tanganyika kama inavyoaminika).
Wazanzibari wa Pemba na wengi wa Unguja kama matokeo ya 2015 yalivyoonyesha, wameshajua adui yao mkubwa ni CCM na wala sio kingine chochote. Watakuwa pamoja na CHADEMA na maalim. Bado haitokuwa rahisi kuitoa CCM madarakani kutokana na hila zake za kila aina, lakini itakuwa kwenye wakati mgumu sana, na uwezekano wa kuizika kama KANU utakuwa ni mkubwa.
Asante.
Maalimu hawezi kuhamia chadema, kwa sababu zifuatazo. Mosi, sera za chadema na Cuf zinatofautiana, ataacha sera alizopigania kwa miaka yote hiyo na aanze kupigania sera za Cdm? Haiwezekani, mpaka sasa najua maalimu anaichukia cdm kwani asili ya mgogoro wa cuf ni cdm kupitia ukawa, najua hili mtalipinga ila lina ukweli, kwani tafsiri yake ni kuwa tangu mwanzo nia ya cdm ilikuwa ni kuiua cuf. Cuf ina kaunasaba ka dini ya Kiislamu zanzibar na bara, cdm ina kaunasaba ka kiruthel tangu kauli ile ya ni zamu yetu, hivyo maalimu kujiunga na cdm ni sawa na kubatizwa, hivyo hatakubali pamoja na wafuasi wake, mi naona hana jingine ila tu kuanzisha chama kingine, japo hakitakiki. Ila itanailaani sana cdm kwa kuivuruga cuf
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo ccm ni chama cha dini gani ? Haya wakate kujiunga chadema watawaliwe na ccm katoliki.
Siasa zinabadilika watambue hilo ,hata wakisusia uchaguzi watawapa ccm tu maushindi ya burebure
Mkuu,Sefu anatafunwa na karma ya kumpora Mapalala CUF, usihangaike.Hata maji Marefu ni Profesa. Yaani Lipumba ni dola kumtumia ndiko kunakomfanya aonekane na watu kama nyie kumuona ni Profesa na siyo "Pro-pesa" lakini yeye mwenyewe akiachwa na Maalim ni mwepesi kuliko unyoya wa kuku.
Na lengo la CCM kumtumia Lipumba sidhani kama litafanikiwa kwani ni yeye mwisho wa siku ndiye atakayedharauliwa!
Yaonekana una hofu baada kutambua kuwa mnaweza kuua CUF, lakini sio mitazamo ya kimaendeleo ya kina Maalim Seif. Upinzani sasa ndo utaongezeka nguvu. Hila na mabavu ya ccmserikali vitasaidia kujenga upinzani makini zaidi, kama ilivyokuwa kwa ANC wakati wa Afrika ya kusini ya makaburu.Maalimu hawezi kuhamia chadema, kwa sababu zifuatazo. Mosi, sera za chadema na Cuf zinatofautiana, ataacha sera alizopigania kwa miaka yote hiyo na aanze kupigania sera za Cdm? Haiwezekani, mpaka sasa najua maalimu anaichukia cdm kwani asili ya mgogoro wa cuf ni cdm kupitia ukawa, najua hili mtalipinga ila lina ukweli, kwani tafsiri yake ni kuwa tangu mwanzo nia ya cdm ilikuwa ni kuiua cuf. Cuf ina kaunasaba ka dini ya Kiislamu zanzibar na bara, cdm ina kaunasaba ka kiruthel tangu kauli ile ya ni zamu yetu, hivyo maalimu kujiunga na cdm ni sawa na kubatizwa, hivyo hatakubali pamoja na wafuasi wake, mi naona hana jingine ila tu kuanzisha chama kingine, japo hakitakiki. Ila itanailaani sana cdm kwa kuivuruga cuf
Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa umenena vyema 100%.Huu mgogoro unaofukuta ndani ya CUF kwa ugomvi kati ya Katibu Mkuu halali wa CUF Mhe. Maalimu Seifu na Mwenyekiti fake Prof(njaa) Haruna Lipumba umelenga kuimaliza CUF kisiasa.
Kwa msaada wa Serikali na vyombo vya ulinzi na Usalama CUF halali lazima iangamie ili isiendelee kuisumbua CCM ya Serikali ya Awamu ya 5. Figisu zote zinazoendelea lengo ni Maalimu Seifu na lazima amalizwe kisiasa kabla ya 2020!!
Serikali wanajua kabisa kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Maalimu Seifu alishinda kwa kishindo na kama Uhuru,Haki na Demokrasia ya kweli vingetamalaki na kuzingatiwa na ZEC hivi leo Maalimu Seifu angelikuwa yuko Ikulu ya Zanzibar akiongoza Visiwa vya Marashi ya Pemba.
Kwa hali inavyoelekea imebakia kete moja tu kwa Maalimu Seifu ambayo itamwokoa kisiasa nayo ni KUANZISHA CHAMA KIPYA CHA SIASA. Lazima CUF halali wajifunze kwa Wapinzani Kenya kina Raila Odinga, William Ruto, Uhuru Kenyata na wengineo. Kwamba jina la Chama sio hoja. Leo hakuna KANU tena wala ODM badala yake tuna JUBILEE na NASA na siasa zinakwenda! Jambo la msingi hapa ni WATU au UMMA ulio nyuma yako. Nina hakika kama Maalimu ataondoka leo na kuachana na CUF ambayo Lipumba ameamua kuisambaratisha na kuunda Chama kingine kwa Jina lolote kwa ajili ya kuwakomboa Wazanzibari na Wazanzibara toka utawala kandamizi wa CCM umma wote utakuwa nyuma yake.
Kwa kufanya hivo Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watakuwa wamepoteza uanachama wa CUF kama wale wa kuteuliwa(Special Seats) walivyopoteza juzi baada ya kutimuliwa na CUF ya Lipumba. Kitakachofuata ni Tume ya Uchaguzi kuitisha Uchaguzi na Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watarudi Bungeni kwa jina la Chama kipya na ushindi mkubwa. Kwa mtaji huo CUF ya Lipumba watakuwa hawana Wabunge wa Kuchaguliwa na kwa mantiki hiyo hawatakuwa na Wabunge wa Viti Maalumu na hawatakuwa na RUZUKU tena.CUF watabaki na Lipumba na Sakaya na ndiyo itakuwa hitima ya CUF Tanzania.
Usitake kupotosha wala kuchanganya mambo hapa. Hiyo 2015 cuf na cdm zilishiriki uchaguzi huo ndani ya ukawa na huko visiwani cdm waliachiwa nadhani jimbo moja alilokuwa Salim Mwalimu basi. Na mgombea wa urais kwa tiketi ya muungano huko visiwani alikuwa ni Lowassa na yeye alipata kura nyingi kuliko hata Magu. Kwa sasa iwapo Cuf waligoma kushiriki uchaguzi wa marudio ni wazi wameshapoteza sana, hivyo wamuache Lipumba atambe kupitia mgongo wa serekali kwa muda mfupi sana. Inafahamika Cuf ya Seif ndio yenye nguvu kwa wananchi hivyo uchaguzi ujao Lipumba atabaki na ofisi tu kwani uwezo wa kupata kura hana, na hilo analifahamu. Hata haya mapendekezo ya Seif kuhamia cdm wanaccm hawayapendi maana wanajua Lipumba hana watu, na iwapo Seif atahamia cdm sasa itaimarika zaidi kwani itakuwa na nguvu bara na visiwani.