Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Huu mgogoro unaofukuta ndani ya CUF kwa ugomvi kati ya Katibu Mkuu halali wa CUF Mhe. Maalimu Seifu na Mwenyekiti fake Prof(njaa) Haruna Lipumba umelenga kuimaliza CUF kisiasa.
Kwa msaada wa Serikali na vyombo vya ulinzi na Usalama CUF halali lazima iangamie ili isiendelee kuisumbua CCM ya Serikali ya Awamu ya 5. Figisu zote zinazoendelea lengo ni Maalimu Seifu na lazima amalizwe kisiasa kabla ya 2020!!
Serikali wanajua kabisa kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 Maalimu Seifu alishinda kwa kishindo na kama Uhuru,Haki na Demokrasia ya kweli vingetamalaki na kuzingatiwa na ZEC hivi leo Maalimu Seifu angelikuwa yuko Ikulu ya Zanzibar akiongoza Visiwa vya Marashi ya Pemba.
Kwa hali inavyoelekea imebakia kete moja tu kwa Maalimu Seifu ambayo itamwokoa kisiasa nayo ni KUANZISHA CHAMA KIPYA CHA SIASA. Lazima CUF halali wajifunze kwa Wapinzani Kenya kina Raila Odinga, William Ruto, Uhuru Kenyata na wengineo. Kwamba jina la Chama sio hoja. Leo hakuna KANU tena wala ODM badala yake tuna JUBILEE na NASA na siasa zinakwenda! Jambo la msingi hapa ni WATU au UMMA ulio nyuma yako. Nina hakika kama Maalimu ataondoka leo na kuachana na CUF ambayo Lipumba ameamua kuisambaratisha na kuunda Chama kingine kwa Jina lolote kwa ajili ya kuwakomboa Wazanzibari na Wazanzibara toka utawala kandamizi wa CCM umma wote utakuwa nyuma yake.
Kwa kufanya hivo Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watakuwa wamepoteza uanachama wa CUF kama wale wa kuteuliwa(Special Seats) walivyopoteza juzi baada ya kutimuliwa na CUF ya Lipumba. Kitakachofuata ni Tume ya Uchaguzi kuitisha Uchaguzi na Wabunge wote wa Kuchaguliwa CUF watarudi Bungeni kwa jina la Chama kipya na ushindi mkubwa. Kwa mtaji huo CUF ya Lipumba watakuwa hawana Wabunge wa Kuchaguliwa na kwa mantiki hiyo hawatakuwa na Wabunge wa Viti Maalumu na hawatakuwa na RUZUKU tena.CUF watabaki na Lipumba na Sakaya na ndiyo itakuwa hitima ya CUF Tanzania.