Kesi za mimba za wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi za mimba za wanafunzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Sep 27, 2010.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini hizi kesi za wanaume kuwapa mimba wanafunzi mara nyingi zinaishia kwa mazungumzo ya kifamilia na hazifiki mahakamani na kama zikifika mahakamani wengi hawahukumiwi.

  Maana kumpa mimba mwanafunzi kwa mujibu wa sheria unafungwa miaka 30 lakini toka hiyo sheria ipite miaka kama 10 iliypita sidhani kama waliofungwa wanafikia 50 wakati kila siku vibinti vinabebeshwa jazz band

  Hivi imekaaje hii wadau?
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,463
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu wakubwa wa nchi nao wanahusika.......na wanafunzi wana viherehere....hivo kesi hazitaendesheka kirahisi
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  hivi umewahi kusikia mtu kafungwa kwa kumpa mimba denti?
   
 4. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  wanaopeana mimba ndo tayari washaanzisha family, ukimfunga miaka 30 huyo dogo atakaezaliwa hatapata mapenzi ya baba mpaka afikie umri kama wangu na kuendelea, dah!!
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kama inakuwa wamebakwa sawa. lakini kwa vibinti hivi vinavyo jishebedua na kujipeleka peleka kwa tamaa za maisha! mi sioni kama wanabebeshwa mimba ila wanajitakia wenyewe.kwani wanawake hawana akili? kitendo walichokubaliana wote wawili halafu sheria imuhukumu mmoja tu! labda tukubaliane wanawake niwapungufu wa akili.:playball:
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,324
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  Tatizo vibinti vinajidai vinajua sana kupenda.
  Vikiambiwa vimtaje aliyemkandika mimba, vinagoma, vinakuwa vikali na kutishia kujiua ili tu bwana mbebeshaji mimba asifikishwe mahakamani na kuhukumiwa kifungo.
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Umaskini unachangia .wengine hawana sent ya kununulia hata kakofuli ndio maana wakipewa nao wanajiachia .
   
 8. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  hilo nalo neno
   
 9. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  kitendo cha kumpa mwanafunzi mimba ni kosa kwa mwanaume na mwanamke thats why huwa wanamaliza kwa mazungumzo,ukisema mwanaume afungwe ina maana alimbaka huyo binti?i gues walikubaliana ila kosa, binti anatakiwa ajitambue kwamba yeye ni mwanafunzi as well kijana anatakiwa atambue kuwa binti anahitaji kusoma. sidhani kama ni busara kuubana upande mmoja wakati tendo lifanywa kwa ushirikiano wa bint na kijana tena kwa makubaliano na appointment iliyosubiriwa kwa hamu.
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  sasa mjazaji akienda selo 30 years nani atalea mimba, mama na mtoto?
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wanafunzi wanaobebeshwa mimba ni kwa sababu ya viherehere vyao-JK
   
 12. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  nadhani prezida hapa alitereza
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,463
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Na huyu mtoto akukuwa ataimba '' Papa was a rolling stone....wherever he laid his hat was his home''


  [​IMG]
   
 14. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kwa sababu ni vimbelembele vyao vinawapelekea kupata mimba ndio maana hakuna mtu wa kufuatilia kesi.
   
 15. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hivi mnaposikia jela miaka 30 mnadhani mchezo. Hiyo sheria imekuwa ngumu kutekelezeka kutokana na ukali iliyo nayo. Wangefanya hata ka miaak 3 tu inatosha kumtia mtu adabu. Hiyo sheria ilitungwa kwa jazba na ndo mana wote walioshiriki kuitunga wanajisikia vibaya kwa makali iliyokuwa nayo.
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  inawezekana hii reason uliyotoa nayo inachangia naona hii sheria inatakiwa kuangaliwa upya
   
 17. 2my

  2my JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi inakuwaje pale wanapopeana mimba both wakiwa madent!hii sheria ya 30 yrs selo iko applied hapa!au hii ikoje?
   
 18. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  hapo inakuwa ngoma droo itatumika sheria ya shule tu ya kuwafukuza shule wote haraka
   
 19. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hilo swali zuri nami napenda nipate jibu lake. Hiyo miaka 30 inakuwa kwa wote wawili?
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  hiyo ya denti kwa denti sheria haitumiki inatumika kwa denti na mtu wa nje (tena mkubwa kiumri)
   
Loading...