Kesi ya Wakili Fatuma Karume dhidi ya afisa wa polisi imefikia wapi?

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,826
5,451
Ni takriban wiki mbili au tatu sasa tangu wakili msomi Fatuma Karume alipoenda kufungua kesi dhidi ya afisa wa polisi kwa madai ya kudharirishwa. Ni kesi iliyovuta hisia za watu wengi mno hasa kwa wafuasi wa vyama vya siasa.

Mara ya mwisho nilisikia tu wakili msomi Tundu lisu kuungana na mawakili wengine 29 kumtetea Fatuma Karume katika hiyo kesi ambayo yeye anadai alipwe bil 5 kama fidia baada ya kudharirishwa. Naomba yeyote mwenye kujua nini kinaendelea ktk hiyo kesi anifahamishe.Ahsante.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Mkuu kama sijakosea hakimu alijitoa kwa kuisogeza kesi,

karume hakutaka isogezwe na hakimu hakuwa na nafasi tarehe za karibuni, akaamua kujitoa, wakili karume akazinguana naye, huko huko ndani
 
Kesi zisizo na mashiko hizi zinapumbaza raia wengi sana. Cha ajabu hata mawakili nao wanazikimbilia hizi utadhani hawana kazi za kufanya. Mleta mada kwa nini usiombe mrejesho wa kesi waliofungua wananchi wanaobomolewa nyumba zao?
 
Mkuu kama sijakosea hakimu alijitoa kwa kuisogeza kesi,

karume hakutaka isogezwe na hakimu hakuwa na nafasi tarehe za karibuni, akaamua kujitoa, wakili karume akazinguana naye, huko huko ndani
Hili ni shauri jingne ambalo halimhusu yeye moja kwamoja bali ni anamtetea mteja wake mwenye case ya madai na ni ya muda mrefu wanaipiga tarehe tu
 
Mkuu kama sijakosea hakimu alijitoa kwa kuisogeza kesi,

karume hakutaka isogezwe na hakimu hakuwa na nafasi tarehe za karibuni, akaamua kujitoa, wakili karume akazinguana naye, huko huko ndani

Huyu dada wakili ni shida sana. Akiwa mahakamani huwa anataka yeye ndio awe hakimu/jaji. kila atakacho yeye ndio kiwe hivyo. Huwa inafikia wakati hata wateja wake wanalalamika mahakamani kwa upuuzi wake.
 
Toa mifano ya baadhi ya kesi ambazo wateja wake walimlalamikia vinginevo wewe ni muongo nq mkurupukaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi zisizo na mashiko hizi zinapumbaza raia wengi sana. Cha ajabu hata mawakili nao wanazikimbilia hizi utadhani hawana kazi za kufanya. Mleta mada kwa nini usiombe mrejesho wa kesi waliofungua wananchi wanaobomolewa barabara zao?
Wanaobomolewa nyumba zao
 
Msichana Mharifu hushikwa popote na police katika mwili wake haijalishi wa kike au wa kiume ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola kujibu uhalifu wake.
Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom