DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu tayari amepandishwa kizimbani kwenye chumba namba moja (1) cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Oktoba 10.2025 kwaajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa kwa mfululizo Mahakamani hapo chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru inaendelea leo kwa mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe kuanza kumuuliza maswali ya dodoso (cross examination) shahidi wa pili (2) wa Jamhuri Inspekta wa Jeshi la Polisi John Kaaya.
Pia Soma:Tundu Lissu afikishwa tena mahakamani leo Oktoba 9, 2025, Mawakili wa Jamhuri kumuhoji shahidi namba moja wa Jamhuri
Wakuu jana tuliishia sehemu ya 84 karibuni katika sehemu ya 85
Part 85
Mhe. Lissu ameingia,
Majaji wote watatu wameingia.
Leo humu ndani wameweka Ma TV mengi sana.
Sijui ndio wanataka kucheza hizo video lipo lingine la kama inch 70 huko lipo katikati ya Judge na Mh. Lissu.
Linawafanya wasionane kabisa.
Naona Jaji kama anaongea na Karani kuwa inapaswa hiyo ihamishwe hapo.
Inatukinga hajazungumza kwa sauti lakini tunamuelewa alichokuwa anakisema. Kwasababu ndio kinachotekelezwa hapa.
Sasa kesi inasomwa na karani hapa.
Anasima Renatus Mkude ni Wakili wa serikali Mkuu, Niko na Ajuaye Zengeli, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukos, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa. Lissu yupo na ajitetea Mwenyewe.
Shauri linakuja kwa mshitakiwa kumuhoji maswali ya Dodoso.
Mh. Lissu wale wageni wangu wameambiwa hawawezi kuingia ndani ya Mahakama hii hadi wapate kibali cha idara ya Uhamiaji.
Sasa wataendelea kuwepo hadi watakapofukuzwa kuwepo nchini hadi kibali chao cha kuwepo Tanzania kitakapoisha.
Tunataka tujue Dunia ijue kama kweli uhuru wa Mahakama upo kweli au ni maneno tu.
Kwahiyo nitaendelela kusema na naomba mnisamehe kwa hilo na mnivumilie.
Majaji wanateta hapa kidogo.
Mahakamani hapa yupo Makamu Mwenyekiti wa Chama, John Heche, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa, Mjumbe wa Kamati Kuu God bless Lema, Katibu Mkuu wa Bavicha Dua Lyamzito na viongozi pamoja na wanachama wengine wengi.
Majaji wanateta kama dakika tano hivi hapa Mahakamani.
Wamemaliza kuongea.
Jaji Ndunguru amewasha kipaza sauti chake anasema naomba tuisemee hii hoja kwamba sisi tunafuata utaratibu tuliojiwekea kwa kuzingatia idadi ya watu pia.
Kwahiyo tumeambiwa jambo hilo linashughulikiwa na ofisi ya Msajili naomba ndugu zako wawasiliane na Ofisi ya Msajili ili wakalimalize.
Jaji Ndunguru Nadhani tuko vizuri sasa tunaweza kuendelea.
Mhe. Lissu anamjibu tuko vizuri kabisa.
Sasa Jaji anamuonya Shahidi hapa kuwa uko chini ya kiapo.
Ukumbuke hilo.
Haya Mshitakiwa karibu sana umuulize Maswali Shahidi.
Shahidi amevaa kisweta fulani cha damu ya Mzee muonekano wake haeleweki kama anataka kulia au kucheka.
Mhe. Lissu : Insp. John Kaaya ni majina yako.
Kaaya: Ndio.
Mhe. Lissu : Nikikuuliza ndio au hapana jibu hivyo. Nikisema fafanua unafanya hivyo.
Tukienda hivyo tutamaliza upesi. Usipofanya hivyo tutaenda mpaka week ijayo.
Mhe. Lissu: Jana ulisema maneno yafuatayo ndio yalikufanya uone kauli yangu ya tar. 03/04 yalikuwa na lengo la kuitisha Serikali "Tunahamasisha uasi, tutavuruga sana sana......" ulisema hivyo.
Kaaya: Ndio kwa sauti ya chini sana.
Mhe. Lissu: Ongeza sauti Bwana we si ni askari.
Mhe. Lissu: Uchaguzi upo kwa sheria ulisema. Ni kweli au sio kweli?
Kaaya: Anajibu kuwa ni Kweli.
Mhe.Lissu : ulisema kuzuia uchaguzi bila kufuata utaratibu kama vile kupata order ya mahakama nia yake ni kuitisha serikali?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa eleza mahakama kwamba kwa miaka mingi zaidi ya miaka 30 viongozi na wanachama wamekuwa wakitumia njia ya mahakama kupinga mfumo huu wa Uchaguzi?
Kaaya: Hilo sifahamu.
Mhe. Lissu : Unafahamu kama 1993 aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party Mtikila akipinga sheria za uchaguzi alifungua kesi mahakama kuu na kesi nyingine kupinga zuio la vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara?
Kaaya: Mimi SIJUI.
Mhe. Lissu: Unanfahamu kama Mch. Mtikila vilevile alifungua mashauri hapa mahakama kuu kupinga zuio la watu wasio wa vyama vya siasa kugombea nafasi za kisiasa?
Kaaya: Nilikuwa Shule.
Mhe. Lissu: We polisi nimekuuliza unafahamu au hufahamu?
Kaaya: SIJUI.
Mhe. Lissu : Jibu hivyo ili twende harakaharaka. Je kwenye kesi hiyo ya Mtikila mahakama kuu hii ilisema hicho kifungu cha Katiba kinachokataza watu kugombea wasio na vyama hakipo sahihi unafahamu hilo?
Kaaya: Mwaka gani ilikuwa?
Part 86
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Insp Kaaya Cross-examination
Mhe. Lissu: Mimi ndio nakuuliza Maswali au
wewe?
Haya unafahamu katika kesi ya Mtikila kupinga kifungu cha Katiba kinachozuia wagombea binafsi kilikubaliana na hoja zake na kifungu hicho kinakiuka misingi ya katiba na kifutwe?
Kaaya: SIFAHAMU.
Watu wanacheka 😀😀😀
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama unafahamu kwamba baada ya mahakama kuu kuamuru kifungu hicho kifutwe mahakama ya rufani ilitengua uamuzi huo na kusema kibaki?
Kaaya: Sifahamu kiukweli.
Mhe. Lissu : Unafahamu kwamba baada ya mahakama ya rufani kumkatalia kukataa kufanya mabadiliko kwa njia mahakama alienda kufungua kesi mahakama ya Afrika kupinga mambo hayo?
Kaaya: Hilo Sifahamu.
Mhe. Lissu : Waeleze unafahamu au hufahamu mwaka 2011 Mahakama ya Africa ya haki za binadamu iliiamuru Tanzania kufuta hivyo vifungu vinavyokataza wagombea huru?
INSP. KAAYA: Hilo Sifahamu.
Mhe. Lissu : Mwaka 2019 viongozi wafuatao Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Hasheem Spunda Rungwe, Seif Sharif Hamad na LHRC walifungua kesi mahakama ya afrika mashariki dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa JMT wakipinga vifungu mbalimbali ya vyama vya siasa? Unafahamu hilo? Kama msajili kusema ondoa Mpina asiwe Mgombea wa Urais. Unafahamu hilo wewe POLISI?
Insp. Kaaya: HILO SIFAHAMU.
Mhe. Lissu : Tarehe 25/03/2022 Mahakama hiyo iliitaka Tanzania kubadilisha hivyo vifungu?
Insp. Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu : Unafahamu BOB CHACHA WANGWE Mwanachama wa CHADEMA alifungua kesi mwaka 2021 alifungua kesi akipinga Wakurugenzi kusimamia uchaguzi kwenye sheria za Tanzania? Unafahamu hilo?
Insp. Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu : Na unafahamu Majaji walisema hivyo vifungu vinapaswa kufutwa?
Insp. Kaaya: Sikumbuki kabisa.
Mhe. Lissu : sasa waeleze majaji kama unakumbuka pia kwamba mahakama ya rufani ikasema uamuzi wa mahakama kuu haufai na ikautengua?
Insp. Kaaya: Sina kumbukumbu hizo.
Mhe. Lissu : Kama unaelewa maana ya maneno yangu ya kwamba mahakamani hakuendeki? Maanaa mmesema kuwa nilisema kuwa MAHAKAMANI HAKUENDEKI. Sasa sema maana ya niliposema mahakamani hakuendeki. Unaweza kuelewa maana ya hayo maneno?
Insp. Kaaya: inategemea na maana anayoitaka.
Mhe. Lissu: naomba ajibu swali tafadhali waheshimiwa majaji. Swali langu ni rahisi.
Jaji hebu jibu shahidi.
Insp. Kaaya yupo kama amechanganyikiwa amegoma kuongea.
Anasema naomba kueleza maudhui niliyosema mimi yapo kwenye video. Anasema maneno mengi.
Jaji shahidi hebu jibu swali ni rahisi.
Kaaya: Ndio nafahamu.
Jaji: Sasa sema yana maana gani?
Kaaya: Kauli ile ni constructive kwamba alianza kusema kuwa majaji ni watu wa Rais...
Mhe. Lissu anasema we Polisi nimekuuliza maana ya maneno ya mahakama hakuendeki maana yake ni nini?
Kaaya: Majaji ni watu wa Rais na kwakuwa ni watu wa Rais basi ni MaCCM na majaji wanafanya kazi zao ili wapandishwe vyeo ili wapandishwe na kwenye tume ndio kuna hela.
Mhe. Lissu : Anasema hawa ndio wanaotulinda.
Watu wanacheka 😀😀😀
Mhe. Lissu : Nikikueleza niliposema mahakama hakuendeki nilikuwa na maana kuwa tumeenda miaka 30 na mahakama zimetukatalia we unasemaje?
Kaaya: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Jibu kiafande mnatukoromea mitaani mkija hapa mnanywea.
Job Mrema: Mshitakiwa amepewa nafasi ya kuuliza Maswali na kumuuliza kwa namna ya kumdhalilisha upande wa Jamhuri tunaona sio sawa.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kila swali nimesema awaeleze majaji.
Hilo nimesema pia kama shahidi amejibu swali na nimekubaliana nae nafikiri nina haki ya kusema inatosha.
Jaji: tuendelee hakuna kitu cha msingi hapo.
Mhe. Lissu : unajua nje ya mahakama kumekuwa na njia nyingine nje za kudai mabadiliko ya Katiba.
Kaaya: Sikuwepo kwenye jitihada hizo.
Part 87
Mhe. Lissu : waeleze Majaji kama unafahamu kama mwezi January 1991 Rais Mwinyi aliunda tume ya Rais ya kama twende na chama kimoja au vingi?
Kaaya: Sina kumbukumbu hizo.
Mhe. Lissu : Tarehe 17 Feb. 1992 tume hiyo maarufu kama Tume ya Nyalali iliwasilisha taarifa yake kwa Rais Mwinyi?
Insp. Kaaya: Sifahamu.
Lissu anasema tukiwa vituoni huko mnatukoromea sana, Ongeza Sauti na usiwe na wasiwasi kusema hufahamu HAUTAFUNGWA.
Mhe. Lissu : Unafahamu kwamba Nyalali na tume yake walipendekeza kwamba nchi hii iwe na Katiba Mpya itakapofika September 1993?
Insp. Kaaya: Sijawahi kusikia kabisa hicho kitu.
Mhe. Lissu : Unafahamu kwamba serikali ya Rais Mwinyi ilikataa mapendekezo ya tume ya Jaji Nyalali kuipatia Katiba Mpya?
Insp. Kaaya: Sina kumbukumbu.
Huyu shahidi majibu yake ni sifahamu na sina kumbukumbu yani akibadili sana ni Sijui.😂😂😂
Acha twende.
Mhe. Lissu : Umewahi kusoma kitabu cha Rais Mwinyi kunaitwa Mzee Rukhsa kinazungumzia historia yake?
Kaaya: Nimekisikia.
Lissu: Umekisoma Je?
Kaaya: Hapana sijasoma.
Mhe. Lissu: Mzee Mwinyi kwenye kitabu hicho alieleza CCM na serikali walikataa mapendekezo ya Baba wa taifa kuwa mgombea binafsi aruhusiwe?
Kaaya: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Umejuaje wakati hujasoma?
Kaaya: Ni kweli sijasoma kwahiyo unaniuliza maswali ambayo sijasoma. Kwahiyo kiukweli sijasoma na sijui hayo mambo.
Watu wanacheka.😂😂
Mhe. Lissu: Baada ya CCM kukataa mapendekezo ya Nyalali Mkapa mwaka 1998 aliteua tume nyingine ya Jaji Kisanga ili kuangalia upya mfumo wa kikatiba.
Kaaya: Mimi sio mwanasiasa ndio maana siyajui hayo.
Mhe. Lissu: Jaji Robert Kisanga alikuwa ni mwanasiasa?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: sasa Unafahamu Jaji Kisanga aliteuliwa na Rais kuongoza tume hiyo mwaka 1998?
Kaaya: Huyo Jaji simfahamu na kazi zake sizifahamu.
Mhe. Lissu anasema mimi siwezi kukufunga ila napenda kukamata waongo kwahiyo hufahamu pia hata maamuzi ya tume yake?
Kaaya: Hayo yote sifahamu.
Mhe. Lissu: mwaka 2003 Rais Mkapa akaunda tume ya Jaji Mac Bomani kuongoza tume nyingine ya mabadiliko ya Katiba?
Kaaya: Sio sehemu yangu ya kazi.
Mhe. Lissu: unafahamu au hufahamu?
Kaaya: sio sehemu ya kazi yangu kwahiyo sijui.
Lissu: yalipokataliwa hujui pia?
Kaaya; sijui kila kitu yani.
Mhe. Lissu: December 31, 2011 Jakaya Kikwete alitangaza ataunda tume ya Katiba ili ikusanye maoni ya Watanzania na kuandaa rasimu ya Katiba na itakapofika mwaka 2014 tuwe na Katiba Mpya?
Kaaya: sijui.
Lissu: unanfahamu Jaji warioba aliteuliwa kuongoza tume hiyo?
Kaaya: Hilo nafahamu.
Mhe. Lissu: Tume ya warioba ilipendekeza kuwe na katiba mpya na kuandaa rasimu?
Kaaya: Hilo nafahamu lilikuwepo.
Mhe. Lissu : Bunge maalumu la Katiba lilikaa zaidi ya miezi 6?
Kaaya: Nafahamu na wewe ulikuwepo pia.
Mhe. Lissu: usiwe na kiherehere sasa. Nimeuliza unafahamu tu?
Mhe. Lissu: Pamoja na kazi yote hiyo ya miaka minne CCM na serikali walikataa mapendekezo ya warioba na hakuna katiba mpaka leo?
Kaaya: Waheshimiwa majaji mchakato wa katiba ulianzishwa na serikali na bado upo kwenye utaratibu.
Mhe. Lissu: kwahiyo kuna utaratibu unaendelea toka 2013?
Kaaya: Mchakato unaendelea ulifika Bungeni lakini taratibu zingine sifahamu kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu baada ya Kikwete kuondoka Akaja Magufuli na baadae Samia. Mwaka 2022 Rais Samia walianzisha maridhiano mwaka huo?
Kaaya: Hayo nilisikia.
Mhe. Lissu: je unafahamu kama hayo mazungumzo yaliongozwa na watu wazito kama Kinana wa CCM na Freeman Mbowe kwa Chadema?
Kaaya: Sikushiriki.
Lissu; unafahamu?
Kaay; sikushsiriki kwahiyo sifahamu
Mhe. Lissu : Unajua Chadema ilipeleka mapendekezo ya namna ya kufufua mchakato wa katiba mpya ili hadi 2024 tuwe na katiba mpy?
Kaaya: Sikuwepo kwahiyo sifahamu.
Part 88
Mhe. Lissu: Je unafahamu tarehe 31/05/2023 CCM ilikataa mapendekezo yote ya Chadema na mazungumzo yale yakaishia hapo?
Kaaya: nimeona kwenye vyombo vya habari kuna mambo yalifanyiwa kazi na serikali.
Mhe. Lissu: Nimeuliza mapendekezo ya Chadema kuhusuu Katiba mpya?
Kaaya: sikushiriki kwahiyo sifahamu.
Mhe. Lissu : December 2021 Rais Samia aliunda kikosi kazi kuangalia matatizo ya mfumo wetu wa Uchaguzi na kumteua Prof. Rwekaza Mkandala kuangalia matatizo hayo?
Kaaya: Hilo nilisikia.
Mhe. Lissu: na mapendekezo ya kikosi kazi yalikataliwa na CCM na samia huyu huyu?
Kaaya: Hilo nalo sifahamu.
Mhe. Lissu: Sasa jitihada hizi toka mwaka 1991 hadi leo nikikwambia Chadema na mimi tumejaribu mahakamani imeshindikana na njia ya mazungumzo imeshindikana utasemaje?
Kaaya: SI KWELI.
Mhe. Lissu : waeleze majaji tuna Katiba Mpya au hatuna? Fanya haraka jibu.
Kaaya: tunatumia katiba ile ile ya zamani.
Mhe. Lissu: je uliwahi kuandika maelezo yako Polisi?
Kaaya: Niliwahi kuandika
Mhe. Lissu: je kama ukionyeshwa utayatambua?
Kaaya: Ni kweli nitayatambua.
Mhe. Lissu: anamsomea maelezo yake shahidi yote hapa, anasema nataka kutumia zile stages zote, anamsomea hapa.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa Majaji sasa naomba nianze kumuonyesha maeneo ninayotaka kumcontradict.
1. Eneo la kwanza alisomea chuo cha upolisi Zanzibar
2. Alipewa Cheti cha Competence.
3. Ushahidi wake juu ya masomo
aliyoyasoma kama vile kusomea masuala ya military and safety skills, sheria ya ushahidi.
5. Cheti alichopata baada ya training.
6. Alipelekwa kwenda kusomea nafasi ya assistant Inspector Moshi na kusomea community policing.
Anamsomea maeneo zaidi ya 10 ambayo anataka kumcontradict huyu shahidi.
Hapa ataonesha ushahidi wake mahakamani alisema nini na kwenye maelezo yake ya shahidi ameandika nini?
Mhe. Lissu anaendelea kusoma maeneo anayotaka kumcontradict na muda huu ameshafikisha mambo 40 ambayo yanatofautiana kati ya maneno aliyosema mahakamani na yale aliyoandika kule kwenye maelezo yake.
Huyu shahidi sijui tutamalizana nae lini. Maana zoezi tu la kumuonesha maeneo yenye shida linachukua karibu nusu saa. Je maswali yenyewe itakuwaje?
Lazima kiwake 😂😂😂
Part 89
Wamesimama Mawakili wa Serikali wanasema tunapinga nyaraka kupokelewa kwasababu hatua hazijafuatwa.
Wanasema Mhe. Lissu hajacontradict anataka ipokelewe.
Mhe. Lissu anawajibu Waheshimiwa Majaji wao wenyewe waliniletea hizi kesi siku ya kwanza leo nimetumia utaratibu huo huo ambao waliusema wao na kuniletea kesi tena wameona nongwa.
Kwanza wanasoma sana kesi ya High Court wakati kesi ninayoitumia mimi ni kesi ya Mahakama ya rufani.
Kwahiyo naomba maelezo ya shahidi yapokelewe.
Wanarudi kufanya rejoinder Mawakili wa Serikali amesimama Igans Mwinuka, anasema Majaji mimi sipingi kabisa alichosema kuhusu kesi ya Mahakama ya rufani nakubaliana nayo kabisa.
Hivyo hata hiyo kesi utaratibu wake ni huo kabisa.
Hajaonesha hizo contradiction ni hayo tu.
Majaji wanaandika hapa kidogo.
Jaji anasema na sisi tunahitaji muda kidogo tuweze kwenda kuandika uamuzi mdogo.
Tutaendelea Jumatatu asubuhi itakuwa ni tarehe 13/10/2025.
Kesi imehairishwa mpaka siku ya Jumatatu asubuhi.