Kesi ya Ugaidi ya Freeman Mbowe

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,407
31,392
Kesi ya ugaidi ya Mwenyekiti wa Chadema Mbowe na Wenzake imeondolewa mahakamani

Si sahihi kusema kesi imekwisha, Mahakama inaonyesha 'kuna kesi ya kujibu''
Si sahihi kusema kesi imekwisha, hatukusikia utetezi
Ni makosa kusema 'kuna msamaha' hakuna hatia au hukumu iliyosomwa popote pale

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha ugaidi
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka walikuwepo mashahidi wa kumtia hatiani Mbowe na Wenzake
Kwa mujibu wa Mahakama, Mbowe na wenzake walikuwa na kesi ya kujibu.

Mwisho wa yote kesi imeondolewa mahakamani bila hitimisho

Kuna mengi ya kujiuliza, kuhoji au kushangaa yatokanayo na kesi

1. Kesi iliendeshwajwe bila kujiridhisha ikiwa kuna tatizo la uhalifu !
Jeshi la Polisi lilieleza umma uwepo wa ushahidi wa kutosha dhidi ya Watuhumiwa.
Mwendesha mashtaka na jeshi walifikisha kesi Mahakamani, wameiondoa , ilikuwaje ikafika ilipofikia.

2. Je, sheria zetu zinalinda umma au zinatumika vibaya na waliopewa dhamana!
Tuhuma za ugaidi ni nzito kitaifa na kimataifa. Sheria ya makosa ya ugaidi ni kutopewa dhamana na vifungo virefu.
Kwa haya ya kuondoa kesi bila hitimisho, je, sheria ilitumiwa kama ilivyokusudiwa?
Wanaohisi sheria imetumika kisiasa watakuwa wamekose wapi kwa dhana hiyo

3. Nani anawajibika kwa gharama za kesi
Kwa uzito wa kesi gharama zilizotumika ni pamoja na zile za mahakamani kwa ujumla wake
Kwavile hakuna matokeo ya kesi kwa hukumu , nani anabeba gharama za kesi ?
Ikiwa ni Wananchi, yapi ni maelezo ya kutosha kuhusu matumizi ya kodi zao!

4. Nani anawajibika kwa ''gharama'' za uharibifu wa taswira ya nchi!
Kesi imekuwa na ''gharama' za taswira ya nchi. Kwa kukosa hitimisho, nchi inabaki na tasiwra gani kuhusu utwala wa sheria
Je, wanaodhani kuna mfumo kandamizi dhidi ya Wananchi wamekosea wapi na utetezi wa hapana ni upi.

Kwa upande wa ndani ya nchi, kipindi cha kesi mambo mengi mazuri yanayofanywa na serikali yamefunikwa na kesi
Nani anawajibika kwa ''gharama'' ya kesi hii katika mtazamo huo!

5. Nani anawafidia waathirika
Kwa kukaa ndani miezi au mwaka na kwa ushahidi wa 'kuteswa' nani anawajibika kuwalipa gharama
Kumnyima mtu uhuru ni kosa,kwa mtazamo wa kesi kuondolewa tu mahakamani nani atawalipa waathirika.
Kumkamata mtu ni haki, kumfikisha mahakamani ni haki, na kumpa nafasi ya utetezi ni haki na haki kubwa ni kumpa hukumu
Kwa vile watuhumiwa hawakupewa nafasi ya kujitetea au kuhukumiwa, haki yao ipo wapi


6. Ni ipi taswira ya mahakama katika jicho la kutoa haki bila hiyana au upendeleo
Mwenendo wa kesi uliiacha mahakama ikitazamwa kwa jicho la shaka sana
Maamuzi yalishangaza hata wanasheria, lakini kubwa, kwa vile kulikuwa na kesi ya kujibu na shtaka likaomdolewa wapi 'kesi hii inaacha image' ya mahakama katika kutoa haki? Je, hakuna uharibifu wa integrity and credibility ya mfumo wa kutoa haki nchini!

Kesi imeondolewa lakini si bila 'athari' kwa washtakiwa, serikali na Chadema.

Kwa Washtakiwa, kunyimwa haki ya kujitetea wakiwa wametuhumiwa kwa miezi na mwaka inaacha taswira zao pabaya sana
Mfano, Mbowe ni mfanyabiasha ndani na nje ya nchi. Nani atakayemsafisha na tuhuma za ugaidi ikiwa haikutokea mahakamani?

Kwa upande wa serikali, je, mifumo na taasisi zetu zinalinda haki za wananchi au ni vyombo vinavyotumiwa tu kwa malengo nje ya yaliyokusudiwa. Ni kwa vipi wananchi wataamini tena ikitokea tuhuma kama hizo kwa kiongozi mwingine mathalani wa siasa ?
Na je, serikali iliyohakikisha lipo 'jambo' ilikubali vipi watuhumiwa wa ugaidi kuonana na mkuu wa nchi?

Kwa upande wa Chadema, kesi ya Mbowe iliwunganisha kuliko wakati mwingine. Kesi ilitoa nafasi ya kuonyesha kwanini kuna uhitaji mifumo mipya ya nchi kwa kutumia katiba mpya . Kesi imeonyesha matumizi mabaya ya sheria za nchi na kuthibitishia dunia uonevu unaozungumziwa na chama hicho. Kesi imeonyesha mshikamano wa hali ya juu kwa hali na mali kwa nyakati ngumu
Kwa ujumla kesi imekijenga Chadema badala ya kukidhoofisha na kuhakikisha umma kuwa Chadema ni taasisi bila kutegemea mtu

Lakini pia hitimisho la kesi limeacha kovu ndani ya Chadema. Kesi ''imeisha' kwa hamasa na msisimko mkuwa.
Kitendo cha Mwenyekiti Mbowe kuonana na Rais SHH siku alipofunguliwa kimezua mjadala mpana na kumwaga 'maji baridi katika moto mkali''. Je, Mwenyekiti Mbowe alichukua uamuzi sahihi kwa wakati sahihi na mahali sahihi?
Je, maliziko la kesi na hotuba ya Mbowe imejibu ''ubaridi' aliousababisha kwa kwenda Ikulu haraka ?

Hayo tunayajadili bandiko linalofuata
 
Kesi ya Mh Mbowe II

Mjadala uliopo unahusu Mh Mbowe kukutana na Rais SSH siku alipotoka magereza
Hoja si kukutana, bali uharaka wa kukutana kabla ya kukutana na Wanachama

Wana Chadema wanaaminikesi ilitokana na jitihada za Mh Mobwe kuongoza harakati za kudai katiba mpya. Mwenyekiti alikamatwa Jijini Mwanza alipokwenda kusaidia jitihada

Wanachama wanaamini tuhuma za ugadi zilikuwa kumfunga mdomo wakijua kesi haikuwa na dhamana na ingeisha kwa kifungo, na wanaamini ilifanyika kuua Chama kikuu cha upinzani.

Ushiriki wa shughuli zote za kisiasa za mashirikiano ulisitishwa kwa kauli moja, ' mwenyekiti aachiwe huru bila masharti'.

Mwenyekiti alipokuwa magereza shughuli za chama ziliendelea .
Kikubwa ilikuwa ni hamasa, si ya kumtoa M/kiti bali ya kudai katiba mpya

Chadema Waliungwa mkono na jamii iliyoona dhahiri kulikuwa na tatizo katika kesi na kwamba kama jamii tukae na kuangalia tena mifumo yetu kupitia KATIBA MPYA.

Kuachiwa huru kwa M/Kiti Mbowe ilikuwa kama 'kachumbari' katika mlo mtamu wa kudai katiba.
Kwa namna tofauti kabisa hamasa ilififia masaa machache baada ya M/kiti kuelekea Ikulu

Kulikuwa na bumbuwazi, nini kimetokea ghafla. Taarifa ya pamoja ya Mbowe na Rais SSH hakikusaidia hali

Tatizo halikuwa Rais kasema nini. Tunafahamu Rais alisema nini akiwa na BBC , katika mkutano wa vyama na DW ya ujerumani.Tunajua Mkuu wa Jeshi la Polisi alisema nini kama chombo cha serikali na DPP aliendesha vipi kesi vipi kama sehemu ya serikali

Kinachowasumbua WanaChadema ni kauli ya Mbowe. Kwanza, alipotoka magereza aliomba muda wa kukutana na Familia na ndugu wakiwemo pia ndugu wa ''Chadema'

Ilieleweka kwa kuzingatia mengi yaliyotokea akiwa Magereza ikiwemo taarifa za kupotelewa na ndugu jamaa na marafiki. M/Kiti akapewa fursa hiyo

Ghafla jioni kaonekana akiwa na kutoa kauli za kumpongeza Rais kwa kujali na uwepo wa haki

Tukio hilo limeleta uchechefu mkubwa ndani ya Chadema na kuleta faraja ndani ya CCM

CCM wana haki ya kufurahia, mwenendo wa kesi ulichafua sana taswira yao hasa kwa vijana , wasomi na akina Mama. Kitendo cha kupiga picha ilikuwa 'mahali pa kutokea''

Katika hili CCM na Serikali walichanga karata zao vizuri sana, walielewa kumpa Mh Mbowe kuelewa mazingira ya nje pengine angekuwa na mtazamo tofauti hata kama angekwenda Ikulu siku 1, 2 au 3 baadaye. CCM na Serikali yake walielewa moto wa Chadema ungefunika na harakati zingepata nguvu mpya, na hivyo kutafuta namna ya kumtuliza M/Kiti Mbowe.

Kwa Chadema, uchechefu si kuonana na Mh Rais ni haraka ya kuonana naye.

Kwamba, kwa miezi kadhaa ilijulikana hakuna kesi na kwamba serikali ilikuwa na uwezo wa kuliondoa tatizo si kusbiri shinikizo na kisha kuchukua ''point' za mezani kama ilivyotokea

Hoja za Wanachadema ni je, Mwenyekiti alikuwa na muda wa kutafakari?
Je, aliongea na viongozi wenzake kutafuta ushauri?
Ni kwanini hakuongea na Wanachama, akaridhia 'kuongea' na upande wa pili wa kesi yake.

Kisaikolojia, kinachowachafua baadhi ya Wanachadema ni kejeli na kauli za maudhi kutoka kwa mahasimu wao wa CCM. Mwenezi wa CCM anasema kitendo cha Mbowe ni siasa za kiustarabu! Kinyume cha ustaarabu ni ushenzi kwa maana hiyo.

Wapo CCM wanaosema kitendo hicho kimesaidia kupunguza joto la kudai katiba mpya na wengine kukejeli magereza imeleta 'nidhamu' na kila maneno yenye raha au karaha

Angalizo
Tunasema baadhi ya Wanachadema kwa kuzingatia ukweli kuwa wapo '' wanaojifanya' ni Chadema kwa lengo la kuleta mtafaruku, na wapo WanaChadema wa kweli wenye madai ya uchechefu

Kumekuwa na taharuki na shinikizo la kutaka M/Kiti Mbowe afafanue nini kilitokea Ikulu !

Mwenyekiti akachukua maamuzi ya kuzungumzia suala hilo siku 3 baada ya kutoka gerezani.
Uamuzi unaonyesha shinikizo na taharuki ndani ya Chama chake

Mwenyekiti ahutubia Taifa, bandiko linalofuata
 
Kesi ya Ugaidi-Mh Mbowe III

Mh TL makamu M/Kiti Chadema alikutana na Rais SSH ubelegeji.
Baada ya mkutano TL alitoa taarifa ya kwamba aliomba mkutano nini wamejadili
Kulizuka mtafaruku kwanini Mh TL alieleza maongezi kati yake na Mh Rais.

Ni kweli katika mazingira ya kawaida hilo lisingetokea.
Katika mazingira yetu baada ya miaka 6 hatua hiyo ilikuwa sahihi.

TL alielewa kuna ''spin' za habari ambazo zingeleta mtafaruku ndani ya chama.
Kwamba, yangezushwa yanayohusu maongezi na hatakuwa na fursa ya kueleza

Mh TL alifanya jambo zuri katika siasa, kwamba, alitumia fursa na timing katika tukio

Wasioitakia Chadema mema hawakuwa na hoja wala hawakuweza kufanya ''spin'

Mh Mbowe alitoa taarifa ya pamoja na Mh Rais akieleza mambo mawili, kumshukuru kwa kujali na kutamani haki itamalaki. Kwamba haki ni zao amani. Hakueleza mengine !!

Siku 3 baadaye akahudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Hotuba ilikuwa ya Taifa na kueleza muktadha mzima wa kutoka na kikao na Rais

Hotuba ilikuwa na mambo yafuatayo
1. Kueleza shukurani kwa niaba ya wenzake kwa Jamii kwa michango ya hali na mali.

2. Akaeleza kuhusu katiba na kusema ''Katiba si agenda ya Mbowe ni agenda ya Chadema''

3. Kaeleza utata wa mkutano na Rais, kasema kabla ya kwenda magereza aliomba kukutana na Mh Rais. M/kiti alimaanisha kwenda kwakwe ni kufuatia mwito wa mwaka 1 uliopita

M/kiti hakueleza nini walichongelea. Katika 'utetezi' alikiri kama inabidi achukue maamuzi magumu. Hili la kwenda Ikulu ni mojawapo

Tofauti na namba 2 ,alikwenda Ikulu kwa maamuzi magumu, pengine si agenda ya Chama
Swali, iweje basi kuna nyakati anakuwa kiongozi katika mazingira magumu na nyakati nyingine anakuwa kiongozi wa agenda ya wanachama kama katiba ?

Hotuba yake haiku address utata uliopo bali kuwapa ''wasioitakia mema' Chadema na baadhi ya Wanachadema jambo la kusema. Kwamba, M/kiti amewekewa ' kufuli'

Makamu TL amesikika akisema M/Kiti atakutana na kamati kuu kujadili walichojadili Ikulu.
Ni utaratibu tu wa kurekebisha tatizo (damage control) wakikwepa kukubali uwepo wake.

Ikiwa Mbowe anafahamu umuhimu wa Kamati kuu, kulikuwa na ugumu gani wa kuita kamati kuu kwa njia ya mtandao apate ridhaa na msimamo kabla ya kwenda Ikulu ?

Laiti Mbowe angefanya mawasiliano kwanza isingelitokea tatizo, kwamba, alikwenda kwa baraka za Chama, hakufanya hivyo!! alichukua maamuzi magumu peke yake.
Ugumu wa maamuzi ndio unaoleta sintofahamu ndani ya Chadema

Kuna kila sababu ya kuamini ''Wabaya wa Chadema'wame '' capitalize'' sintofahamu hii ya Mwenyekiti Mbowe kiasi cha kuathiri kampeni nyingine kama ''join the chain'

Mbowe akitoka magereza alikuwa na kila 'excuse' ya kutokwenda haraka.
Alikuwa na sababu za kuwasiliana na wenzake katika chama kwanza!

Hoja si kukutana na Mh Rais, kukutana na Rais kujenga mazingira mazuri ya kutangamana ni jambo la heri sana na lipongezwe.

Hoja ni uharaka wa kukutana naye hata kabla ya kusema ahsante kwa waliompigania.

Hoja ni kuchukua maamuzi mwenyewe, yeye si chama kama livyosema na hawezi kuchagua lini ni ni Mwenyekiti wa kubeba agenda kama katiba (rejea# 2 ) na lini ni Mbowe wa maamuzi magumu. Mwenyekiti ni taswira ya chama na busara lazima imuongoze.

Inaweza kuwa si tatizo ndani ya Chadema, lakini turufu aliyowapa 'wabaya wa Chadema ni kubwa'' na wanaitumia vyema iwe ndani au nje ya chama chake.

M/Kiti amejifunga, kila sentensi yake itaangaliwa kwa jicho kali, haifai na haikupaswa kutokea

Tusemezane
 
Nguruvi, nilidhani ni mimi peke yangu niliepata ukakasi wa Mbowe kuonana na SSH kwa uharaka wa ajabu.

Niseme tu Mbowe alikosea sana, na SSH amejipatia point nyingi mno.
Na kama ulivyosema tatizo lipo kwenye uharaka. Wengi tuliugua baada ya Mbowe kuwekwa ndani, tukazidiwa SSH aliposema Mbowe ni gaidi, na ni kama tulikuwa ICU kwa jinsi kesi jaji alivyokuwa anaendesha kesi.

Kwa waliougua, Mbowe alipaswa aongee na waliougua ili wapone. Alipaswa atembee angalau mikoa yote kuwashukuru watu wa kawaida waliompigania, na hapo hapo automatically to keep in touch with those who joined the chain. Alipaswa hata kuazisha group la whatsup na wote waliojoin the chain na kuwahutubia. Nk, nk, nk

Alipaswa kufanya ziara magereza kuwaona na kuwapa moyo waliofungwa miaka mingi au vifungo vya maisha kisa tu ni wanachama wa CHADEMA.

Kimsingi kesi hii ilimpa Mbowe na CHADEMA faida nyingi kuliko hasara, but nikama amezipiga teke na Zimemwagikia kwenye kapu la SSH
 
Back
Top Bottom