Kesi ya Saileth Vithlani wa kashfa ya Rada

Status
Not open for further replies.
Huyu jamaa wakimleta Bongo si watam-Balali haraka haraka?

Utatu wewe una mawazo kama mimi, huyu wanaweza kabisa 'kumbalali' huko huko UK kabla hata hajakanyaga Bongo. Na hapo ndipo itakuwa mwisho wa kesi ya rada.
 
Jamani mlio karibu na wahusika huko UK muwaambia wamhoji haraka kabla hajabalaliwa.
 

Where is Vithlani? Still in UK or already in Tanzania? Sirikali iko kimyaaaaa haitaki kutufahamisha nini kinaendelea kuhusu fisadi huyu.
 
Where is Vithlani? Still in UK or already in Tanzania? Sirikali iko kimyaaaaa haitaki kutufahamisha nini kinaendelea kuhusu fisadi huyu.
.
Wajameni hawa PCCB hawana lolote. Vithlani japo anatafutwa lakini hana kesi yoyote ya maana.
Hata hii kesi ya kina Mramba, Mgonja na Yona, serikali itapigwa chini.
Ile habari ya this day na kulikoni kuhusu kukamatwa kwa Vithlani ni uzushi tuu kama uzushi wa kukamatwa kwa Mzee wa zeutamu.
Kisheria Vithlani amefanya biashara safi. Kapendekeza bei, serikali ikakubali. John Cheyo akazama kwenye mtandao, akapata bei halisi, akaitisha press conference kupinga, serikali ikaziba masikio, sasa yameibuliwa na SFO ndipo serikali kupitia PCCB inajidai eti inajali!.
Aminini msiamini, mgao haukuishia kwa mzee wa vijisenti, ulipanda mpaka juu darini. Kwa akili ya kawaida, haiwezekani mtuu huyo huyo alambe deal zote hizo yeye mwenyewe na washirika wake, Rada/Ndege ya rais, Helcopter za jeshI, magari ya jeshi na deal nene la silaha za kivita (ila hii ni siri).
Kesi anayotafutiwa Vithlani sio kesi, kusema uwongo chini ya kiapo ni kifungo cha kuanzia mwezi mmoja na kisizidi mwaka mmoja.
 
Wadau, this is for your information. Ripoti juu ya sakata la rada inayoonyesha jinsi Rashid na Chenge walivyohusika. Jamani, hivi ni kipi kinaendelea mbona iko wazi kabisa kuwa hawa jamaa wana kesi ya kujibu? Au ndo kama alivyosema IGP Mwema kuwa mafisadi ni vigumu kuwakamata vinginevyo nchi italipuka
 
Inashangaza kwa ushahidi wote huu serikali nasubiri nini kuwafungulia mashtaka akina chenge na rashid
 
Kulindana ndio jadi ya Mtanzania wakati wengine wanaumia...
 

Asanta sana mkuu, ngoja niipitie.
 
mafisadi watafikishwa mahakamani pindi tu uongozi wa kulindana utakapong'olewa madarakani,otherwise danganya toto tutaendelea kuisikia kila siku
 
aisee asante mkuu

italipuka?mkuu wa polisi anasema ivo?
basi kitu ni kimoja tu,ipo siku hii dhurma ya kulindana itafika mwisho
ngoja utawala mpya siku uingie,au kiongozi makini

watajuta kutufanya waTz taahira!!
 
Ni mpaka CCM itoke madarakani au iwe na wabunge wachache (hata kama itakuwa na Rais) ndipo watanzania tutaanza kuona uozo huu ukichukuliwa hatua. Wakati fulani nilisema tunamuihitaji kiongozi kama Mrema (wa wakati ule) ili kwanza watuhumiwa wote wawekwe ndani!
 
Mkamatwa na ngozi si ndio mwizi wa ng'ombe? ... Vipi mpaka leo wapo? - Mrisho Mpoto
 
...Au ndo kama alivyosema IGP Mwema kuwa mafisadi ni vigumu kuwakamata vinginevyo nchi italipuka

unakumbuka ile hadithi ya sungura aliyekimbizwa na mbwa? kila mbwa alivyokaribia kumkamata sungura, yeye alimrushia mfupa. kwa kifupi hao watu hawakula peke yao.
 
unakumbuka ile hadithi ya sungura aliyekimbizwa na mbwa? kila mbwa alivyokaribia kumkamata sungura, yeye alimrushia mfupa. kwa kifupi hao watu hawakula peke yao.

Sheria itachukua mkondo wake tu, iwe ni mwaka huu au baada ya miaka kenda.. Ushahidi/ukweli tunao na kamwe hawataweza kutunyang'anya.
 
Hii issue ipo open since then......Ila hili linchi letu sijui lina nini tu???? Ila am still holding more pains in veins and the end of all these is soon or later....How soon is ths soon???? yet to know...........................
 
of coz ni chain ndefu na mwishowa mchezo unajikuta hata wale wenye mandate ya kuwashtaki nao wamo kwenye chain. Ila kuna kauli moja-tunafanya uchunguzi-hii kauli ina maana nyingi saana na ni pana kwa ujumla. Uchunguzi unaweza hata kubadili ukweli nayo ni sehemu ya uchunguzi wa kina
 
Jamani watanzania naomba kupitia bunge letu tukufu tumzawadie kitu chochote yule mama wa kiingereza (ex MP) jina lake limenitoka aliyeripua scandal nzima ilohusu rada iliyouziwa serikali ya TZ na kampuni ya BAE systems. Kama si mama huyo leo hii hizo pesa zinazotakiwa kurejeshwa nchini zisingepatikana. Ili kuheshimu na kupongeza kazi aliyoifanya mama huyu nafikiri hatuna budi kuonyesha kuwa tunathamini kazi aliyoifanya.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…