Kesi ya Sabaya na Mbowe ni makutano

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Habari watanzania, watanzania wapenda amani.

Leo Jtatu nimeona nisiwache wanyonge hivi ni bora nitie neno kidogo kwenye hili Sakata la Mbowe sambamba na Sabaya. Maneno yapo mengi ya kusema lakini maneno bora nayoyaona ni haya “ HISTORY REPEAT ITSELF UNTIL LEARNED”. Msingi wa kuchukua msemo huo wa kithungu ni baada ya kufwatilia kwa yaliyojiri katika kesi moja kubwa sana hapo zamani mji wa GALILAYA ambako Pilato kama gavana na mtu mwenye mamlaka katika eneo hilo alilitewa mbele yake bwana mmoja akihutumiwa makosa kadhaa moja ya kosa lilikuwa ni kujifanya mfalme wa wayahudi. Hili shitaka la kujifanya mfalme huyu bwana alisingiziwa na watesi wake ambao ni makuhani na walimsingizia ili ahukumiwe kusubishwa msalabani. Pilato alikuwa na mashaka juu ya mastaka hayo na alikuwa na lengo la kumwachia huru bwana yule, hivyo katika mipango yake kukwepa damu ya yesu mikononi mwake akataka kumwachia kutokana na utaratibu wa kumwachia mfungwa mmoja kabla ya sikukuu, akamleta bwana mmoja, jambazi, muuwaji aliyekuwa akijulikana kama Jesus Barbabas na akawauliza wale washitumu kati ya hawa watu wawili nimwachie nani, wale makuhani wakasema mwachie Barbabas msulubishe huyo mwingine. Mwisho pilato akatoa hukumu na yule bwana akasulubishwa na haukuwa mwisho wake kwani mpaka leo watu wanataja na kusifu jina lake JESUS wa galilaya, mwokozi wa wanyonge.

Ukifwatilia mlolongo wa matukio mpaka bwana Kristu kusulibiwa utaona ni visa vinavyofanana na yanayojiri mahakami kwetu kwa sasa upande mmoja yupo Mbowe, mtu safi na upande mwingine yupo Sabaya, mtu mbaya. Kama nilivyosema hapo mwanzo history repeat itself, kwa kufananisha naona Mbowe ni kama Yesu mtenda haki, Sabaya kama Barbabas, hakimu ni kama Pilato, na watanzania ndio kama makuhani. Kwa hizi kesi mbili bado hukumu hazijatoka ndio maana kwenye kichwa cha huu uzi nimesema hizi kesi ni kama junction/makutano ambako maamuzi yake yata athiri kwa namna moja ama nyingine vizazi na vizazi huko miaka ya mbele ijao. Ukitizama kesi iliyomhusu yesu kristo mwendelezo wake tunaufahamu ya kwamba wale makuhani wenye hila mbovu walifanikiwa kushawishi hukumu ya kifo kwa Kristo na ndipo maandiko yakatimia yesu akapata ushindi mkubwa mpaka leo watu tunajifunza Maisha yake.

Basi namaomba watanzania tuungane Pamoja na mimi katika kupanga matukio ya hizi kesi ya Mbowe na Sabaya ili kuyafanyisha na yale yaliyojiri katika kesi ya yesu Kristo. Kufanikiwa kufanya hivyo kutaleta neema sana katika nchi yetu kama Yesu Kristo alivyoleta neema hapa duniani. Kwa mtizamo huo wa kupanga matukio itabidi Mbowe akamatwe na ugaidi na Sabaya aachiwe huru! Mipango ya kufanikisha ili jambo la Mbowe kufungwa na Sabaya kuachiwa huru itabidi watanzania wote wenye mapenzi mema na hii nchi bila kujali ni CHADEMA ama CCM kushiriki kuhakikisha mpango huu unakamilika, mwongozo wenyewe ni kama ifuatavyo.

Mosi. Inapokuwa kesi ya Mbowe inasikilizwa inabidi twendeni kwa wingi mahakamani tukipiga mayowe “MFUNGE MFUNGE” “MNYONGE MNYONGE MNYONGE” kwa kufanya hivyo kutamshawishi hakimu kutoa hukumu kali kama Pilato alivyofanya hapo kale.

Mbili. Inapokuwa kesi ya Sabaya twendeni pia nje ya mahakama kesi inaposoma kupiga makele kuonyeshwa ya kuwa tunampenda sana Sabaya na aachiwe huru maneo ya kusema tuseme “ MWACHEE MWACHEE” hivyo hakimu akisikia atashawishika na kumwachia Sabaya

Pia ili hili jambo kufanikisha tunahitaji wanachama wa CHADEMA wa ndani kabisa kufikisha huu mpango kwa mwenyekiti wao na hivyo kumpa hii script atakapokuwa akihojiwa na hakimu ili aweze kuhukumiwa.

Hakimu akimwuliza. “ je wewe ni GAIDI hapa nchini Tanzania”

Mweshimiwa mbowe anapaswa amjibu hivi hakimu “ wewe wasema” alafu anauchuna kimya kama hana habari vile, kufanya hivyo kutamwaga nyongo za hakimu na hakimu atahukumu chap chap. CHADEMA BAVICHA msiniangushe kwa hili Tafadhali kwani hamna namna nyingine ya kushida hii nchi kutoka kwa hawa watesi wetu.

Basi ile siku Mbowe ananyongwa mbona ardhi itatetemeka na sijui nani ambaye atawasafisha damu hiyo kwa wale wote waliohusika. Ila kwa wale wenye mapenzi mema na nchi wataimba na kuendeleza yale mwenyekiti alikuwa akihimiza, watasambaa Tanzania nzima kuelezea jinsi gani jamaa Mbowe alivyokuwa jasiri. Anaweza akawatokea baathi kuwapa mwangaza kisha ataondoka mazima hapo mbeleni watanzania wote watakuwa chadema na watamsifu na kujifunza Maisha ya Mbowe na kutafakari yale yote ambayo aliwahi kusema. Kwani Mungu aliyemlinda Tundu Lisu ndio huyo huyo atakuwa na Mbowe katika kuongoza Maisha yake mwanadamu hana la kufanya dhidi yake.
 
Mkuu, kwa nia njema tu naomba kujua unajisikiaje kuona uzi wako una miezi miwili hapa jamvini na hauna hata reply moja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom