Kesi ya Ole Sabaya ni kiashiria cha chuki na udhaifu mkubwa iliyopo ndani CCM tofauti na CHADEMA

Unajaribu kutuaminisha kesi za Sabaya inasukumwa zaidi na chuki za kisiasa dhidi yake.?

Au unamaanisha Ccm imemtosa Sabaya na kama wangekuwa na umoja huenda wangemtetea?
Jamaa anasema kama ni makosa mbona wengi tu ndani ya CCM wamekosa ila wanatamba mtaani? kwa nini awe Sabaya tu. ?
 
Jamaa anasema kama ni makosa mbona wengi tu ndani ya CCM wamekosa ila wanatamba mtaani? kwa nini awe Sabaya tu. ?
Hili pia linafikirisha, maana hata hao waliopiga dili huko Escrow na kwingineko ni majambazi tu.

Hii dunia ina double standards nyingi.
 
Alishawahi kuitwa kwenye kamati ya maadili ya CCM,nini maana ya hiyo kamati..mimi nitaamini vipi?
Kwa hiyo wewe unataka uaminishwe ndio ukubali kwamba Sabaya alikuwa jambazi?

Sabaya amepelekwa mahakamani ili kuthubitisha uhalali wa uhalifu wake, hiyo kamati ya maadili ya CCM sio mahakama kusema kuwa wangemkuta na hatia ya ukosefu wa maadili angehukumiwa kifungo.

Hivyo kama ulikuwa na maslahi na maisha ya bwana mdogo Sabaya alivyokuwa uraiani tafuta namna nyingine ya kuishi subiri na hii hukumu pia ipite uje kulalamika huku.

Yeye , Makonda na baba yao mwenda zake hawakuwa na roho za ubinadamu hivyo hawastahiki kuangaliwa kwa jicho la kibinadamu.
 
Jamaa anasema kama ni makosa mbona wengi tu ndani ya CCM wamekosa ila wanatamba mtaani? kwa nini awe Sabaya tu. ?
Kama anao ushahidi wa kutosha kuendesha kesi dhidi ya hao anowatuhumu/anaowahisi , anayo haki/wajibu wa kwenda mahakamani kufungua mashitaka.
 
Jamaa anasema kama ni makosa mbona wengi tu ndani ya CCM wamekosa ila wanatamba mtaani? kwa nini awe Sabaya tu. ?
Tajiri tanzanite, anashindwa kuainisha makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na makosa ya jinai.

Mengi katika makosa ya matumizi mabaya ya ofisi ( richmond, meremeta, nk) adhabu zake si lazima zifikishwe mahakamani bali mhusika aweza kuwajibishwa kwa mjibu wa sheria za kazi yake, mfano kuwajibika wenyewe, kufutwa kazi, kulipa faiani, onyo, karipio nk...

Hata hivyo katika kundi la makosa ya matumizi mabaya ya ofisi hujitokeza kwa uwazi makosa ya jinai ( rushwa, uhujumu uchumi, ujambazi, wizi, nk) hapa ndipo mhusika hufikishwa mahakamani.

Hapa hauwezi kulinganisha bila kuainisha aina ya kosa katika matumizi mabaya ya ofisi. Mfano kiongozi/ mtumishi anaweza kutumia nafasi yake kwa kuajiri kiupendeleo, huyu si lazima apelekwe mahakamani, adhabu yake ni kupokonywa madaraka.
 
Kama sio msongo wa mawazo, basi una mtindio wa ubongo…. hiyo kenge inapaswa kuongezewa miaka gerezani.
 
Alishawahi kuitwa kwenye kamati ya maadili ya CCM,nini maana ya hiyo kamati..mimi nitaamini vipi?
Unatia aibu mkuu kwa utetezi wa kitoto.

Kuna watu hawana maskio wamekatwa na Sabaya, wengine walipigiluwa misumari kama Yesu msalabani na wengine hawana meno na hizo kesi bado hazijafunguliwa.

Zikiisha kesi za Arusha atashitakiwa tena Kilimanjaro...kaa kwa kutulia mambo bado
 
Back
Top Bottom