Kesi ya Ole Sabaya ni kiashiria cha chuki na udhaifu mkubwa iliyopo ndani CCM tofauti na CHADEMA

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,070
3,705
Hapo vip!!

Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia tuhuma zilizo tengeneza hii kesi ya Sabaya ila nimeonea kama sio tuhuma nzito kuzidi tuhuma zote ambazo tumeshawahi kuzisikia kwa viongozi mbalimbali ndani ya nchi hii, ila kwa maoni yangu kama kweli serikali imeamua kuwashughulikia viongozi wanaotumia madaraka vibaya basi isingeishia kwa Sabaya tu, ningetarajia kuona viongozi wengi wakiburuzwa mbele ya mahakama...kuanzia skendo za Richmond, Escrow, Meremeta n.k

Ila kinachoonekana ni chuki iliyopo baina ya viongozi wenyewe dhidi ya wengine...huku anayemtuhumu mwingine in fact wala sio msafi sana ukimlinganisha na anayemtuhumu ni aibu.

Lakini zaidi na zaidi katika Chama cha Chadema kama kiongozi wao yeyote, au mwanaharakati wao akituhumiwa au akishtakiwa mahakamani iwe kwa tuhuma za ukweli au za uongo hawataki kujua hilo...wataweka tofauti zao pembeni na kuhakikisha wanazunguka kila kona kumtetea mtu wao.

Ila kwa CCM naona kama ni tofauti kidogo, namini Sabaya angekuwa ni mtu wa Chadema, harakati zingefanyika za kugeuza maneno hata kwa gharama yeyote ili kuaminisha Dunia ya kwamba Sabaya anaonewa... ila huku pengine ni tofauti kabisa, kama ulikuwa ndani ya CCM na ukapotoka katika kutekeleza majukumu ya uongozi na yakatolewa maelekezo ya chuki dhidi yako na kiongozi fulani mwenye chuki dhidi yako, basi utaachwa kama mkiwa ushambuliwe na mbwa mwitu wenye hasira kali juu yako na juu ya chama chako.

Binafsi sipingani na hatua ya serikali kuwawajibisha viongozi wanaotumia madaraka vibaya ila bado sijashawishika na hatua hii kwa sababu naona ina hila ndani yake...na kama ni kweli Serikali inadhamira ya dhati kabisa basi Jamhuri ifunguwe kesi kwa viongozi wote wa CCM waliwahi kutuhumiwa kwa kutumia madara vibaya kwa ufisadi na kadhalika...

Na declare ya kwamba mimi siyo mwanachama yeyote wa kisiasa ila natamani nione ule umoja na mshikamano wa CCM wa miaka ya nyuma ukichukua nafasi.

Binafsi CCM naona ndio chama iliyokizi vigezo vya kuitwa chama cha siasa kwa sababu ni chama ambayo haina mwenyewe.
 
Toka nchi hii imepata uhuru wake, ni kiongozi mwenye wadhifa wa RC, DC, aliyewahi kufanya ujambazi kama wa sabaya!!?kuhusu kutumia madaraka vibaya kwa viongozi hayo yapo sana, lakini ya sabaya hapana, ule ulikuwa ni ujambazi.

Kwani watu si walianza kupiga kelele wakati jiwe akiwa hai, lakini alifanya nini zaidi ya kuzidi kumpa kichwa?!!

Kuhusu chadema sio kwamba wao kila mwanachama wao anayeingia matatizoni watamtetea, tu, wewe kabake/ua mtu live ushahidi uko wazi uone kama kuna atakaye kutetea.

Kwa taarifa yako baada ya wiki mbili tena sabaya anachezea mvua nyingine tena!!
 
Alishawahi kuitwa kwenye kamati ya maadili ya CCM,nini maana ya hiyo kamati..mimi nitaamini vipi?
Alishakili alikua anatumwa na magufuli document Hana zinazoonyesha kutumwa lakini alishawahi tamka anatumia makonda style akasahau makonda ni mkuu wa mkoa anauhalali popote kuzunguka isipokua kufanya wizi lakini makonda hajawahi kwenda morogoro kukusanya Kodi
 
Alishakili alikua anatumwa na magufuli document Hana zinazoonyesha kutumwa lakini alishawahi tamka anatumia makonda style akasahau makonda ni mkuu wa mkoa anauhalali popote kuzunguka isipokua kufanya wizi lakini makonda hajawahi kwenda morogoro kukusanya Kodi
Kipindi hicho kulikuwa hakuna mahakama Tanzania,kwanini hakuburuzwa kama alikuwa anajiamulia yeye pasipo kupewa maelekezo?
 
Me nadhani hapo tatizo sio chama ila tatizo linaanzia kwenye katiba yetu na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Ukiangalia RC au DC ni viongozi wa umma kwaiyo inatakiwa waanze kuwajibishwa ndani ya serikali huko kwenye chama ni kutokana na udhaifu wa kikatiba kumpa raisi madaraka makubwa ya uteuzi ambapo sasa anateua machawa wake tu wengine hawana hata sifu za kimaadili kuwa viongozi zaidi ni vijana na makada wa chama chake
 
Back
Top Bottom