Kesi ya Ole Sabaya ni kiashiria cha chuki na udhaifu mkubwa iliyopo ndani CCM tofauti na CHADEMA

Hapo vip!!

Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia tuhuma zilizo tengeneza hii kesi ya Sabaya ila nimeonea kama sio tuhuma nzito kuzidi tuhuma zote ambazo tumeshawahi kuzisikia kwa viongozi mbalimbali ndani ya nchi hii, ila kwa maoni yangu kama kweli serikali imeamua kuwashughulikia viongozi wanaotumia madaraka vibaya basi isingeishia kwa Sabaya tu, ningetarajia kuona viongozi wengi wakiburuzwa mbele ya mahakama...kuanzia skendo za Richmond, Escrow, Meremeta n.k

Ila kinachoonekana ni chuki iliyopo baina ya viongozi wenyewe dhidi ya wengine...huku anayemtuhumu mwingine in fact wala sio msafi sana ukimlinganisha na anayemtuhumu ni aibu.

Lakini zaidi na zaidi katika Chama cha Chadema kama kiongozi wao yeyote, au mwanaharakati wao akituhumiwa au akishtakiwa mahakamani iwe kwa tuhuma za ukweli au za uongo hawataki kujua hilo...wataweka tofauti zao pembeni na kuhakikisha wanazunguka kila kona kumtetea mtu wao.

Ila kwa CCM naona kama ni tofauti kidogo, namini Sabaya angekuwa ni mtu wa Chadema, harakati zingefanyika za kugeuza maneno hata kwa gharama yeyote ili kuaminisha Dunia ya kwamba Sabaya anaonewa... ila huku pengine ni tofauti kabisa, kama ulikuwa ndani ya CCM na ukapotoka katika kutekeleza majukumu ya uongozi na yakatolewa maelekezo ya chuki dhidi yako na kiongozi fulani mwenye chuki dhidi yako, basi utaachwa kama mkiwa ushambuliwe na mbwa mwitu wenye hasira kali juu yako na juu ya chama chako.

Binafsi sipingani na hatua ya serikali kuwawajibisha viongozi wanaotumia madaraka vibaya ila bado sijashawishika na hatua hii kwa sababu naona ina hila ndani yake...na kama ni kweli Serikali inadhamira ya dhati kabisa basi Jamhuri ifunguwe kesi kwa viongozi wote wa CCM waliwahi kutuhumiwa kwa kutumia madara vibaya kwa ufisadi na kadhalika...

Na declare ya kwamba mimi siyo mwanachama yeyote wa kisiasa ila natamani nione ule umoja na mshikamano wa CCM wa miaka ya nyuma ukichukua nafasi.

Binafsi CCM naona ndio chama iliyokizi vigezo vya kuitwa chama cha siasa kwa sababu ni chama ambayo haina mwenyewe.
Wewe ni sabaya na ni sukuma gang.... Utajibeba na ushetani wenu mama kaokoka mwenzenu
 
Akina Sabaya wako wengi sana.

Mwingine anagombana na akina GSM huko regent!
Chawa wengi walipora mali za Wananchi wenzetu hadharani.Makonda hakuwa na raslimali hizo kabla ya kuteuliwa kuwa dc na baadaye rc.
Hivi vyeo vya utumishi wa kuteuliwa vimetumika kuwaumiza Watanzania wengi sana.
Tukipata Katiba mpya tunavifuta na kuokoa raslimali nyingi za Taifa letu.
 
Ukitetea uovu unajiweka kwenye nafasi gani wewe mwenyewe?
naamini kwamba kwa anayetetea uovu anayo sababu yake binafsi ikiwemo kwamba ni pamoja na kwamba alikuwa anafaidika yeye mwenyewe binafsi kupitia uovu ambao anajaribu kuutetea
Kwa mtu mwenye imani ya kimungu huwezi mtetea mouvu anayeadhibiwa kwa sababu ya uovu alioufanya na tena na unatetea kwa kutoa sababu ambazo ni hafifu mno kwamba kwa sababu waovu wengine unaowafahamu wewe hawajaadhibiwa basi na yeye huyu asiadhibiwe

acha sabaya avune alichokipanda kwa wakati ule na sasa ni wakati wa yeye kuvuna na wengine nao watavuna kwa wakati wao ila usisahau kwamba hata wezi wanaoiba siyo wote huwa wanakamatwa kwa wakati mmoja ila kila anayekamatwa huwajibika kwa wakati wake

Hivyo nakushauri ukae kimya ama ueleze wewe nini alichosingiziwa kama utapewa nafasi ya kufanya hivyo.
sasa hawa wezi walionekana kwenye riport ya CAJ..wapelekws mahakamani..kama mama alikuwa alikuwa anapambana na wezi na majambazi ndani ya serikali.
 
Back
Top Bottom