GE2025 Kesi ya Mpina kuzuiwa kugombea Urais Kupitia ACT inaendelea leo Septemba 8, 2025 Saa 8 Mchana Mahakama Kuu Dodoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
TAARIFA KWA UMMAKESI YA LUHAGA MPINA KUENDELEA SAA 8-00 MCHANA MAHAKAMA KUU DODOMA.#TaifaLaWote#.jpg
Kesi ya Luhaga Joelson Mpina dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume Huru ya Uchaguzi ya kuzuiliwa kuwa Mgombea Urais Kupitia ACT Wazalendo, itaendelea Leo Saa 8 mchana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Chama cha ACT kimesema Waandishi wa Habari wanakaribishwa Kuhudhuria.

============================

Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma, leo Jumatatu, Septemba 8, 2025 inahitimisha usikilizaji shauri la kuenguliwa kwa mgombea urais aliyeteuliwa na Chama cha ACT-Wazalendo kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29.

Awali Mahakama hiyo ilielekeza shauri hilo lisikilizwe kwa njia ya maandishi na mawakili wa pande zote waliwawasilisha hoja zao kwa tarehe walizopangiwa.

Hata hivyo mahakama hiyo, inahitimisha usikilizaji wa shauri hilo leo kwa njia ya mdomo, ambapo mawakili wa pande zote watafika mahakamani kwa ajili ya ufafanuzi wa baadhi ya hoja zao za maandishi.

‎Shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa wa ACT-Wazalendo na mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Luhaga Mpina; dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

‎Chama hicho kilichukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wa Mpina kuomba kuteuliwa na INEC kuwa mgombea urais wa chama hicho, na wa INEC kumzuia kurejesha fomu yake ya kuomba uteuzi aliyokabidhiwa awali kuijaza.

‎Katika shauri hilo namba 21692 la mwaka 2025 lililofunguliwa chini ya hati ya dharura sana, chama hicho pamoja na mambo mengine kinapinga uamuzi wa INEC kumuengua mgombea wao huyo katika orodha ya wagombea wa vyama mbalimbali walioomba uteuzi wake.
 
Kwanini Zirto Cabwe hataki kugombea hiyo nafasi na hata yule mama aliyetakiwa kugombea naye amepigwa chini.
 
hahaha wakati zito huuyo bungeni, wajinga ndiyo waliwao na muslims ...
 
Leo kesi mbili za kisiasa zinagonga vichwa vya habari, kesi ya mpina haina impact kulinganisha na kesi ya lissu, ya mpina inaonekana ni zuga tu
 
Kesi ya Luhaga Joelson Mpina dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume Huru ya Uchaguzi ya kuzuiliwa kuwa Mgombea Urais Kupitia ACT Wazalendo, itaendelea Leo Saa 8 mchana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Chama cha ACT kimesema Waandishi wa Habari wanakaribishwa Kuhudhuria.

============================

Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma, leo Jumatatu, Septemba 8, 2025 inahitimisha usikilizaji shauri la kuenguliwa kwa mgombea urais aliyeteuliwa na Chama cha ACT-Wazalendo kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika Oktoba 29.

Awali Mahakama hiyo ilielekeza shauri hilo lisikilizwe kwa njia ya maandishi na mawakili wa pande zote waliwawasilisha hoja zao kwa tarehe walizopangiwa.

Hata hivyo mahakama hiyo, inahitimisha usikilizaji wa shauri hilo leo kwa njia ya mdomo, ambapo mawakili wa pande zote watafika mahakamani kwa ajili ya ufafanuzi wa baadhi ya hoja zao za maandishi.

‎Shauri hilo limefunguliwa na Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa wa ACT-Wazalendo na mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Luhaga Mpina; dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

‎Chama hicho kilichukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wa Mpina kuomba kuteuliwa na INEC kuwa mgombea urais wa chama hicho, na wa INEC kumzuia kurejesha fomu yake ya kuomba uteuzi aliyokabidhiwa awali kuijaza.

‎Katika shauri hilo namba 21692 la mwaka 2025 lililofunguliwa chini ya hati ya dharura sana, chama hicho pamoja na mambo mengine kinapinga uamuzi wa INEC kumuengua mgombea wao huyo katika orodha ya wagombea wa vyama mbalimbali walioomba uteuzi wake.

..Samia amehakikisha hana mpinzani.

..wakati Mpina amekwama mahakamani, Samia anachanja mbuga akipiga kampeni.
 
Back
Top Bottom