Kesi ya Mfanyabiashara Salehe Alamri kumiliki silaha kinyume na sheria yapigwa kalenda hadi September 28, 2021

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria inayomkabili mfanyabiashara,Salehe Salim Alamri na wenzake imehairishwa jana katika mahakama ya hakimu mkazi wilayani Babati mkoani Manyara .

Kesi hiyo nambari 11 ya mwaka 2020 imehairishwa Jana na hakimu wa mahakama hiyo,Kimario hadi September 28 mwaka huu baada ya upande wa jamhuri kueleza kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Katika kesi hiyo Mfanyabiashara huyo anadaiwa mnamo Julai 26 mwaka 2019 akiwa katika eneo la Makame Kijenge jijini Arusha alikutwa akimiliki silaha aina ya Riffle CAR 22 No. 00104516 kinyume na sheria.

Pia mfanyabiashara huyo siku hiyo hiyo alikutwa na silaha nyingine aina ya Shotgun yenye nambari 00104513 mali ya HSK Safaris Ltd aliyokuwa akiimiliki bila leseni wala kibali cha umiliki kutoka mamlaka husika.

Mbali na mfanyabiashara huyo mtuhumiwa mwingine,Gerald Joseh Ole Kashiro anashtakiwa kwa kosa la kushindwa kutunza silaha sehemu salama kinyume na sheria nambari 59(1)(a) na sheria nambari 61 ya sera ya udhibiti wa silaha nambari 2 ya mwaka 2015.

Katika shitaka hilo Ole Kashiro anadaiwa mnamo Febuari 20 mwaka 2020 akiwa katika pori ya hifadhi ya akiba ya Simanjiro ndani ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara alishindwa kuhifadhi sehemu salama silaha aina ya Rifle 300mm No.A757677 na nyingine aina ya Shotogun 12bore No.T.0611018 na kishindwa kuzihifadhi sehemu salama hali iliyopelekea kuangukia mikononi mwa mtu asiyekuwa na uhalali kisheria.

Itakumbukwa ya kwamba mbali na mashtaka anayokabiliwa Ole Kashiro lakini pia anatumikia kifungo cha miaka 30 katika gereza la mkoa Manyara kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali katika kesi ya uhujumu uchumi nambari 21 ya mwaka 2019 hukumu iliyosomwa na hakimu Jumaa Mwambago.

WAFANYA KIKAO CHOONI,

Katika hali isiyo ya kawaida mahakamani hapo mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa Ole Kashiro anayetumikia kifungo cha miaka 30 katika la mkoa wa Manyara alionekana akifanya kikao cha siri pembeni ya choo cha mahakama hiyo na mfanyabiashara huyo tukio lililowaacha watu midomo wazi.

Katika kikao hicho Ole Kashiro alikuwa na Alamri pamoja na askari wa magereza ambaye hakutambulika jina lake Mara moja ambapo haijajulikana walikuwa wakijadili mambo gani jambo huku mazingira ya eneo walilokuwa wamesimama yaliibua hali ya mshangao.

Katika tukio hilo watu hao walionekana wakiteta kwa muda wa takribani dakika 20 huku askari magereza akiwasimamia jambo ambalo liliubua maswali mengi mahakamani hapo na kisha baadae mfungwa huyo alipelekwa katika mahabusu iliyopo mahakamani hapo kabla ya kurejeshwa magereza.

Mwisho.

Pichani chini ni mfanyabiashara anayetuhumiwa kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume na sheria,Salehe Alamri akifanya maongezi na Gerald Ole Kashiro anayetumikia kifungo cha miaka 30 katika gereza la mkoa wa Manyara kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali katika kesi ya uhujumu uchumi nambari 21 ya mwaka 2019 pembeni ya choo cha mahakama hiyo Jana,aliyesimama katikati ni askari magereza.

Mwisho.

IMG_20210826_122421_108.jpeg
IMG-20210826-WA0013.jpeg
IMG-20210826-WA0012.jpeg
 
Back
Top Bottom