antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 51,283
- 133,887
The rights of every man are diminished when the rights of one man are threatened.Hapa chini ni nukuu halisi kutokea kwa baba Askofu Lusekelo:
View attachment 2052368
Kauli yake inaakisi kauli za maaskofu na masheikh wengine wengi wakiwamo kina:
"Sheikh Ponda, Dr. Shoo, Niwemugizi, Mwamakula, Dr. Bagonza, na wengi wengine."
Mwangwi kama huo unasikika kutokea kwa manguli kama kina Prof. Shivji, Lwaitama, Ulimwengu, Warioba nk.
Kwa hakika ni furaha kuu mbinguni na nchini, sauti nzito kama hizi zinaposikika.
Haipo shaka kuwa tuko katika njia sahihi.
Kwa hakika ni suala la muda tu, kwani inafahamika Mola hajawahi kuwaacha waja wake.
Eeh mola wetu ukawape ujasiri zaidi watumishi wako hawa kuweza kutufikisha kunako taifa la ahadi.
Taifa lenye utamalaki wa haki, uhuru usawa na demokrasia.
Eeh Mola wetu, ukatusikie.
John F. Kennedy