Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Hiyo affirdavity imeshamaliza hiyo kesi hakuna kesi ya kujibu tena hapo kama amesafishwa na BWM kwisha...tusubiri JK nae atasemaje akiwa waziri wa BWM je atamkaanga na kumkana boss wake wakati huo?sio rahisi...Mahalu out
 
Hiyo affirdavity imeshamaliza hiyo kesi hakuna kesi ya kujibu tena hapo kama amesafishwa na BWM kwisha...tusubiri JK nae atasemaje akiwa waziri wa BWM je atamkaanga na kumkana boss wake wakati huo?sio rahisi...Mahalu out

from the begining the DPP knew that he had a strong case at hand, just as he thought so during Zombe's case. The defence councel will have to fight to the end to win this case, that's why it was ruled that, the defendant had a case to answer.

From the legal point of view, whether JK testifies in person or by affidavit it weighs very little, what matters is what he testifies about, and if there is a proof beyond reasonable doubt linking the defendant with the malicious practice while in office at Rome.

Wishing the Republic all the best to win this case, and if it turns otherwise, then a heavy burden to our public coffers in terms of civil proceedings in favour of the defendant.
 
Hii fani ya sheria ngumu sana! Nimesoma maelezo yanayotajwa kuwa ni affidavit ya Mkapa in defense of Mahalu, na sijaona popote ambapo Mkapa anasema Mahalu hakutenda kosa hilo aliloshtakiwa, sasa najiuliza ni utetezi huu?

Shahidi (Mkapa) amerudia yote yanayojulikana tayari kwenye kesi hii, na hajagusa chochote kuhusu wizi unaodaiwa kufanyika wa Euro milioni 2.

Nashangaa kwa nini mawakili wa utetezi hawajataka aitwe mahakamani wamfanyie mahojiano kidogo. Anyway, sorry, sina ujuzi kwenye fani hii, niacheni tu nishangae!
 
Je aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje anaweza kuitwa kutoa ushahidi mahakamani (for the prosecution or defence)? Hii kesi naweza kuona itakavyoisha.. itakuwa ni null prosequi na DPP!
Kama Mawakili wanaomtetea Mahalu wataona kuna umuhimu wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hana budi kufanya hivyo.
 
Hiyo affirdavity imeshamaliza hiyo kesi hakuna kesi ya kujibu tena hapo kama amesafishwa na BWM kwisha...tusubiri JK nae atasemaje akiwa waziri wa BWM je atamkaanga na kumkana boss wake wakati huo?sio rahisi...Mahalu out

And the guy is out! Kwanza inasemekana pesa zenyewe zilikusanywa kwa ajili ya kampeni ya kumuweka Kikwete madarakani, sasa hapa unategemea nini?
 
Hapa ndo sielewi

Yaani ni ngumu sana kumeza hii dadangu. Jamaa atadai fidia na huyu dada (Grace) alikuwa analipwa nusu mshahara kwa kipindi chote cha kesi yao. Naye itabidi wamlipe malimbikizo yote na kama alistahili kupanda cheo hapo katikatika sijuwi inakuwaje, wataalamu wa sheria watuambie.
 
Yaani ni ngumu sana kumeza hii dadangu. Jamaa atadai fidia na huyu dada (Grace) alikuwa analipwa nusu mshahara kwa kipindi chote cha kesi yao. Naye itabidi wamlipe malimbikizo yote na kama alistahili kupanda cheo hapo katikatika sijuwi inakuwaje, wataalamu wa sheria watuambie.

Hivi huu mchezo wa mara kwa mara WANASHERIA wa serikali kupeleka kesi mahakamani bila ushahidi wa kutosha utaisha lini?

Kwani tumeshachoshwa nao kuanzia IPTL, RICHMOND, KESI YA ZOMBE na nyingine ambazo nimezisahau pamoja na hii nayo ya Mahalu. Na gharama ya kuendesha hizo kesi ni nani analipia?
 
Hivi huu mchezo wa mara kwa mara WANASHERIA wa serikali kupeleka kesi mahakamani bila ushahidi wa kutosha utaisha lini? Kwani tumeshachoshwa nao kuanzia IPTL,RICHMOND,KESI YA ZOMBE na nyingine ambazo nimezisahau pamoja na hii nayo ya Mahalu. Na gharama ya kuendesha hizo kesi ni nani analipia?

Mkuu hakuna haki mahakamani kama inavyofikiriwa. Suala la ushahidi wa kutosha is very relative term na mahakimu hutumia hicho kigezo as a loophole ya kutoa maamuzi kutokana pengine na maelekezo waliyopewa na wakubwa wao au baada ya kula mlungula.

Hizi kesi zote ulizozitaja hapa vigogo wa serikali kuu wanahusika hivyo nashawishika kusema kuwa maamuzi hayakuwa ya haki bali kulinda uovu wa viongozi wetu maana wanahusika katika kesi hizo.
 
Kweli iko----Kazi!!! Did Public become overly Judgemental in this case??...... Did Court of Law Justice prevail???
 
same old story, pesa za watanzania zinaibiwa na hakuna anayechukuliwa hatua, kufikishwa mahakamani ndio style ya kumaliza mambo kiujanja ujanja.

So good country, iba peleka kesi mahakamani, itapigwa danadana weee, zikifika danadana 100 inaibuka issue nyingine wanasema hakuna ushahidi then kimya, watanzania tunaibiwa na siku zinakwenda wezi wanaendelea kupeta.
 
Naleo ndo hukumu imetolewa,Mahalu na Grace hawana hatia...Kweli kuna haja ya kuwa na sheria au tutumie hisia tu?
 
Mengi, This Day wamjibu Mahalu

  • Wasisitiza si mwaminifu, pia alidanganya
  • Waeleza alivyoweka fedha akaunti tofauti
  • Wasema kavuliwa ubalozi, ilibainika Dar
na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI Mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi, waandishi na wahariri wa Gazeti la This Day na Kulikoni, wamemjibu aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, na kusisitiza madai dhidi yake yaliyoandikwa na magazeti hayo.

Madai hayo ni kumhusisha Mahalu na ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, iliyopo 185 Via Cortina d Ampezzo, jijini Roma, ambapo wanaeleza kwamba, bei iliyokubaliwa awali ni tofauti na fedha zilizotolewa.

Katika majibu yao ya maandishi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na Wakili Deogratias Ringia mwishoni mwa wiki iliyopita, walisema kwamba makubaliano ya ununuzi wa jengo hilo yalikuwa Euro 1,032,913.80, lakini fedha zinazodaiwa kulipwa ni Euro 3,098,741.40.

Wanaeleza kwamba, Euro 1,032,913.80 ziliwekwa katika akaunti ya Ceres SRL, kwa mujibu wa makubaliano yalivyokuwa Oktoba, 2002, wakati fedha nyingine, Euro 2,065,827.60, zilipelekwa kwenye akaunti nyingine, ya Monaco Soc Ceres SRL, asasi ambayo haikuwa mshirika katika makubaliano ya mauzo ya Oktoba mosi, 2002. Ringia alisema walalamikiwa wataegemea nyaraka hizo.

Walalamikiwa waliosaini majibu yao, licha ya Mengi ni Furaha Thonya, Mbaraka Islam, Simon Ileta, Kiondo Mshana na Agapitus Nguma. Wameeleza kwamba, malipo ya ziada ya Euro 2,065,827.60 hayakuambatanishwa na maandishi ya makubaliano ya mauzo, kati ya Ceres SRL wala Monaco Societata a Responsabilita (Monaco Soc Ceres SRL), katika akaunti ambako fedha hizo inaelezwa zilipelekwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wanaeleza kwamba, zaidi ya hapo, maagizo yanayodaiwa yalitolewa na Ceres SRL, kwamba fedha zilipwe kwenye akaunti hiyo nyingine, hayakuonyeshwa kwenye hati ya madai ya Mahalu iliyowasilishwa Mahakama Kuu.

Katika barua zake tofauti kwa Serikali ya TanzaniaAvvocato Pasqual Giorgio, alionya juu hatari ya kuwa na mkataba wa mauziano, unaoonyesha bei ndogo, wakati stakabadhi zinaonyesha kiasi kikubwa zaidi cha fedha, na ilishuhudiwa hivyo kwa barua yake kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje iliyoandikwa Milan Mei 5, 2004, wanaeleza walalamikiwa hao.

Kadhalika, wameeleza kwamba, kutokana na udanganyifu huo, ofisi ya Balozi wa Tanzania iliyopo Roma, pamoja na makazi yake, yaliingiliwa kwa nguvu na kukaguliwa na watekeleza sheria wa Italia. Kwamba suala hilo lilichunguzwa na taasisi zenye dhamana hiyo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB).

Japokuwa ripoti za uchunguzi huo hazijawekwa hadharani, mlalamikaji (Mahalu) alivuliwa hadhi ya kidiplomasia na kutakiwa kurudi nyumbani Tanzania, na alipowasili, mlalamikaji hakupitia VIP ambako kwa kawaida hutumiwa na watu mashuhuri, mabalozi wakiwamo. Nakala za picha za kuwasili kwa mlalamikaji zinaambatanishwa, wanaendelea kueleza walalamikiwa hao.

Mengi na wenzake wanazidi kueleza kwamba, baada ya kuwasili kwake nchini, alitoa taarifa kwa wapelelezi, na pia kwa vyombo vya habari, alinukuliwa na hajapata kukanusha, kwamba kulikuwapo na makubaliano ya Euro 1,032,913.80 tu. Mahalu amewafungulia kesi walalami
 
Back
Top Bottom