Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 299
- 58
Mengi, This Day wamjibu Mahalu, Wasisitiza si mwaminifu, pia alidanganya.
Waeleza alivyoweka fedha akaunti tofauti. Wasema kavuliwa ubalozi, ilibainika Dar na Mwandishi Wetu.
MWENYEKITI Mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi, waandishi na wahariri wa Gazeti la This Day na Kulikoni, wamemjibu aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, na kusisitiza madai dhidi yake yaliyoandikwa na magazeti hayo.
Madai hayo ni kumhusisha Mahalu na ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, iliyopo 185 Via Cortina d' Ampezzo, jijini Roma, ambapo wanaeleza kwamba, bei iliyokubaliwa awali ni tofauti na fedha zilizotolewa.
Katika majibu yao ya maandishi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na Wakili Deogratias Ringia mwishoni mwa wiki iliyopita, walisema kwamba makubaliano ya ununuzi wa jengo hilo yalikuwa Euro 1,032,913.80, lakini fedha zinazodaiwa kulipwa ni Euro 3,098,741.40.
Wanaeleza kwamba, Euro 1,032,913.80 ziliwekwa katika akaunti ya Ceres SRL, kwa mujibu wa makubaliano yalivyokuwa Oktoba, 2002, wakati fedha nyingine, Euro 2,065,827.60, zilipelekwa kwenye akaunti nyingine, ya Monaco Soc Ceres SRL, asasi ambayo haikuwa mshirika katika makubaliano ya mauzo ya Oktoba mosi, 2002. Ringia alisema walalamikiwa wataegemea nyaraka hizo.
Walalamikiwa waliosaini majibu yao, licha ya Mengi ni Furaha Thonya, Mbaraka Islam, Simon Ileta, Kiondo Mshana na Agapitus Nguma. Wameeleza kwamba, malipo ya ziada ya Euro 2,065,827.60 hayakuambatanishwa na maandishi ya makubaliano ya mauzo, kati ya Ceres SRL wala Monaco Societata a Responsabilita (Monaco Soc Ceres SRL), katika akaunti ambako fedha hizo inaelezwa zilipelekwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanaeleza kwamba, zaidi ya hapo, maagizo yanayodaiwa yalitolewa na Ceres SRL, kwamba fedha zilipwe kwenye akaunti hiyo nyingine, hayakuonyeshwa kwenye hati ya madai ya Mahalu iliyowasilishwa Mahakama Kuu.
"Katika barua zake tofauti kwa Serikali ya Tanzania…Avvocato Pasqual Giorgio, alionya juu hatari ya kuwa na mkataba wa mauziano, unaoonyesha bei ndogo, wakati stakabadhi zinaonyesha kiasi kikubwa zaidi cha fedha, na ilishuhudiwa hivyo kwa barua yake kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje iliyoandikwa Milan Mei 5, 2004," wanaeleza walalamikiwa hao.
Kadhalika, wameeleza kwamba, kutokana na udanganyifu huo, ofisi ya Balozi wa Tanzania iliyopo Roma, pamoja na makazi yake, yaliingiliwa kwa nguvu na kukaguliwa na watekeleza sheria wa Italia. Kwamba suala hilo lilichunguzwa na taasisi zenye dhamana hiyo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB).
"Japokuwa ripoti za uchunguzi huo hazijawekwa hadharani, mlalamikaji (Mahalu) alivuliwa hadhi ya kidiplomasia… na kutakiwa kurudi nyumbani Tanzania, na alipowasili, mlalamikaji hakupitia VIP… ambako kwa kawaida hutumiwa na watu mashuhuri, mabalozi wakiwamo. Nakala za picha za kuwasili kwa mlalamikaji zinaambatanishwa," wanaendelea kueleza walalamikiwa hao.
Mengi na wenzake wanazidi kueleza kwamba, baada ya kuwasili kwake nchini, alitoa taarifa kwa wapelelezi, na pia kwa vyombo vya habari, alinukuliwa na hajapata kukanusha, kwamba kulikuwapo na makubaliano ya Euro 1,032,913.80 tu. Mahalu amewafungulia kesi walalamikiwa hao, kutokana na habari walizoandika na kuchapisha, zikimhusisha na kashfa ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia.