Kesi ya Lema: Shahidi amtaja Edward Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Lema: Shahidi amtaja Edward Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Dk. Batilda Burian


  Shahidi wa pili upande wa ulalamikaji, katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), Agness Gideon Mollel, ameieleza mahakama kuwa aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, alidhalilishwa na Lema kwa kuambiwa ana mimba ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, na hafai kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa madai wananchi watakuwa wameliuza kwa Lowassa.

  Aidha, aliiambia mahakma hiyo kuwa alimsikia Lema akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kuwa, Dk. Burian alikuwa ameolewa Zanzibar na akipata ubunge ataifunga Safina Redio na kuufungua msikiti.

  Alitoa madai hayo mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabiel Rwakibarila, anayesikiliza kesi hiyo iliyofunguliwa na watu watatu, ambao ni Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo.

  Mahojiano kati ya shahidi na wakili upande wa walalamikaji, Alute Mugwai, yalikuwa kama ifuatavyo:

  Wakili: Wewe unaishi mtaa gani?
  Shahidi: Mtaa wa Roman Katoliki.
  Wakili: Huo mtaa una mwenyekiti wa mtaa?Shahidi: Ndiyo ambaye ni mimi.

  Wakili: Wewe una elimu gani?
  Shahidi: Elimu ya msingi.

  Wakili: Umemaliza mwaka gani?
  Shahidi: 1983.

  Wakili: Wewe ulihudhuria mikutano mingapi ya kampeni?
  Shahidi: Nilihudhuria mikutano mitatu ya CCM, Chadema na TLP.

  Wakili: Huo mkutano wa Chadema ulifanyika lini na wapi?
  Shahidi: Ulifanyika Septemba Mosi eneo la Bigsister, Kata ya Olorieni.

  Wakili: Ulianza saa ngapi?
  Shahidi: Ulianza saa kumi jioni.

  Wakili: Unaweza kueleza alichosema Lema katika mkutano huo?
  Shahidi: Ndiyo, nilimsikia Lema akisema msimchague Dk. Batilda sababu ana mimba ya Lowassa na ameolewa na Mzanzibari, hivyo akichaguliwa mtaliuza jimbo kwa Lowassa na akiwa mbunge atafunga Redio Safina na atafungua msikiti.

  Wakili: Huyo Lowasa ni nani?
  Shahidi: Huyo Lowassa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli na alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu.

  Wakili: Baada ya kusikiliza maneno hayo ulifanya nini?
  Shahidi: Niliamua kuondoka.

  Wakili: Sasa Mahakama ikithibitisha maneno haya yalisemwa na Lema,
  unataka Mahakama ikufanyie nini?
  Shahidi: Nataka avuliwe ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini na atulipe gharama za kesi hii.

  Baada ya mahojiano hayo ndipo alipoanza mahojino mengine na wakili wa upande wa mlalamikiwa, Method Kimomogolo na sehemu ya mahojiano yalikuwa kama ifutavyo:

  Wakili: Hivi unakumbuka uliweka sahihi yako katika hati ya mashitaka ulipofungua kesi hii wewe na wenzako?
  Shahidi: Ndiyo.

  Wakili: Uliyosema hapa na katika hati ya mashitka mbona yanatofautiana, katika hati ya mashitaka sehemu uliyosaini wewe inasema ulimsikia Lema akisema asichaguliwe Dk. Batilda sababu ni
  mwanamke na hafai kuwa kiongozi na ukadai aliyasema hayo eneo la
  Fantastiki huko Olomatejoo kata ya Erelai?
  Shahidi: Siyo kweli sikusema hivyo.

  Wakili: Angalia haya maneno na sahihi hii siyo yako?
  Shahidi: Ndiyo.

  Wakili: Hapa mahakamani ni lazima useme moja ukubali moja tu, nakuuliza
  tena hii hati ni yako au umeyakataa uliyobambikiziwa? Na ni kweli uliyoshuhudia ni ya Olomatejoo au Bigsister?
  Shahidi: Nimeshuhudia ya Bigsister Kata ya Olorieni.

  Hapo Jaji aliingilia kati na kuhoji kama ifuatavyo:
  Jaji: Ulishuhudia wapi?
  Shahidi: Bigsister kata ya Olorieni.

  Jaji: Hakuongea chochote kuhusu eneo la Fantastic Olomatejoo?
  Shahidi: Hapana.

  Wakili Kimomogolo aliendelea na mahojiano kama ifuatavyo:

  Wakili: Akija mtu akasema ulihudhuria mkutano Septemba 22 mwaka juzi saa 10.00 jioni eneo la Fantasitick Elerai atakuwa mwongo? Na mwongo Mkubwa?
  Shahidi: Hata sifahamu eneo hilo.

  Wakili: Wewe unafahamu Redio Safina ilipo na siyo ile ya kuambiwa?
  Shahidi: Ndiyo na nilishasali pale.
  Wakili: Hufahamu Redio Safina ipo Kaloleni na siyo Olasiti?
  Shahidi: Mi najua Olasiti tu.

  Wakili: Je, katika huo mkutano uliomsikia Lema akisema Dk. Burian ana mimba ya Lowassa na maeneo yote hayo ulikuwa na tepu ya kunasa hayo maneno?
  Shahidi: Hapana sikuwa nayo.

  Wakili: Ulikuwa na kalamu ya kuandika na kuweka kumbukumbu ya yale yaliyosemwa?
  Shahidi: Sikuwa nayo.

  Wakili: Je, ulishawahi kumuuliza Dk. Batilda kwanini hajafungua kesi au
  aliwahi kukueleza sababu ya kutofungua kesi? Wakati yeye aliwahi kuwa Waziri na hivyo kama ulimweleza amedhalilishwa angekimbilia mahakamani kwa nini hakufanya hivyo?
  Shahidi: Hakuwahi kunieleza.

  Wakili: Sasa wewe kama mama lishe na tena darasa la saba, ukaamua kufungua
  kesi je, wewe binafsi uliguswaje hayo maneno?

  Shahidi: Yalinigusa kijinsia, kidini na kikabila.
  Wakili: Je, ulishawahi kuona au kusomewa maelezo ya Lema ya kujibu malalamiko yenu?
  Shahidi: Nilisomewa tu.

  Wakili: Wewe huo ujasiri unaupata wapi wakati wewe mama lishe na Waziri akaogopa kufungua kesi hii?
  Shahidi: Natetea haki zangu za kimsingi.

  Kesi hiyo inayovutia hisia za watu na kujaza umati wa watu mahakamani hapo, inaendelea na utoaji wa ushahidi upande wa walalamikaji leo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I think this case should go private kama hizi ndio excuses Batilda anatumia kwenye kesi... tu huwezi kupata mimba bila kutiana au kupandikiza mbegu, this is not right!! edward and Batilda both have families, can we imagine the pain cause by these ushahidis??
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  HIvi kwanini Batilda mwenyewe hakufungua kesi? Inawezekana ni kweli hakudhalilishwa? maana kama anayedaiwa kudhalilishwa hajalalamika mahali popote hawa wengine wanajuaje kuwa amedhalilishwa?
   
 4. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii kesi kwa mwenendo huu nafikiri ccm wanapoteza muda wao kama ilivyotokea kwa Slaa walipomfungulia kesi 2010
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Wastage of the scarce govt resources! Kuna kesi nyingi za msingi na mahakimu hakuna! Sasa kama mama lishe anakana maelezo yake ya msingi, what is that?
   
 6. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kesi gani hii!..****** mtupu.
   
 7. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mama lishe amehongwa huyoo sio buree, maana batilda mwenyewe mbona hakufungua io kesii??? i smell smthing fishy here!
   
 8. M

  Makfuhi Senior Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwani huyu mama alijuaje Batilda hakuwa na hiyo mimba ya lowasa?. Pia ni kweli Batilda ameolewa Zanzibar; kashfa iko wapi
   
 9. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Mpangilio mbaya wa matumizi ya mali ya umma (Time + Resources)
   
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hawa wanaolalamika huwa nawafananisha na wale watu wanaopiga kelele pale wanapomwona Mbwa amekalia Mkia wake, wakidhani Mbwa anaumia. Kumbe kukalia mkia ni moja ya starehe za Mbwa. Kama angekuwa anaumia angesimama kwani ni yeye mwenyewe ndiye aliyeukalia. Hawa watu ni Wanafki! Njaa Mwanakharam!

   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  upumbavu mtupu, hata hao mahakimu wanaosikiliza hii kesi wanapoteza muda wao
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Patamu hapo hata kama lema atashinda lakini ni vema wakati mwigine kuchagua maneno mazuri ya kusema kwenye kampeni ili wakati mwingine hali na usumbufu kama huu usijitokeze tena.
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hao ndio mashaidi gani?hii kesi imepikwa na dhamira kuu ni kumvua ubunge Lema,lakini hakimu atakua na kazi kubwa sana kutimiza dhamira ya waliopika kesi,maana hawakujipanga kabisa!ushaidi gani unaotolewa mahakamani huo?hizi njaa kweli kazi!
   
 14. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wape pole njaa zitawaua na waelekeze wakalime kupunguza njaa.
   
 15. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hao watu wamelipwa na Batilda ili wakamsemee? How come atukanwe mwingne, akashtaki mwingne tena mamalishe std 5? Tanzania hatujafikia huo ustaarabu na utash huo hapo...therez smthng behind the scene! Sasa jamani....mwe! Nimekosa hata cha kumalizia sentensi kwa kweli! Smthng very fishy is taking place....pale!
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Watu wanasukumwa kwa njaa zao kuja mahakamani kutoa ushahidi usio na maana, mashahidi wa namana hii wametumwa kwa lengo la kuyumbisha mbunge wetu asiwe makini kwenye majukumu yake ya ubunge!!!!!

   
 17. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hivi hawa waliofungua kesi wana tofauti na wale Wakristo walikuwa Bonde la Msimbazi wakitaka kusafiri bure kwenda kuhubiri nje ya Nchi?? Nimewasahau dhehebu lao.Imani Mbovu inayonuka...
   
 18. n

  nketi JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbu batilda anawafuasi wengi sana wanaomuonea hadi mamalishe kaamua kufungua kesi badala yake?!!!!!!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Mimi hata sielewi kinachoendelea huko Arusha, hata nikisoma kilichoandikwa hapa natoka mtupu. Mara namsoma huyo Agness Gideon Mollel kama shahidi wa kesi, halafu ghafla anabadilika na kuwa mshitaka aliyefungua kesi..darasa la saba sijui hiyo elimu ndio inaweza fungua kesi au ndio kujua zaidi haki yake.

  Halafu utangulizi unaonyesha ni kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), sasa sielewi ni nani anayeweza kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo zaidi ya Batilda mwenyewe..Mwenye kuelewa zadi kinachoendelea atujuze maana vitu kibao vinajichanganya hapa.
   
 20. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hivi hii ndio kesi ninayosikia kuwa Lema anapoteza ubunge??
  Au kuna nyingine??
  Kama ni hii, basi nasubiri kweli kuona anapopotezea.
  Labda kwa tusiojua sheria tunaweza kusema hvyo
   
Loading...