Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 15, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Namshukuru sana Maringo na wenzake kuona kiini kikuu cha umwagaji damu na uminyaji wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu wa 31 Okt 2010 kwa kufungua kesi ya kikatiba.

  Source: Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa

  Exuper Kachenje

  UCHAGUZI mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu unaweza kuingia mushkeli baada ya mkazi wa Dar es Salaam, Denis Maringo kufungua kesi ya kikatiba akihoji sheria inayozuia matokeo ya rais kupingwa baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi (Nec). Katika kesi hiyo ya madai namba 86 ya mwaka 2010 iliyofunguliwa juzi,

  Maringo anataka mahakama itoe ufafanuzi wa mambo hayo kabla ya kufanyika uchaguzi huo. Maringo pia anadai kuwa Rais Jakaya Kikwete alivunja katiba kwa kulivunja Bunge kabla ya kumalizika muda wake wa miaka mitano. Kwa mujibu wa Maringo, Bunge la Tisa la Jamhuri la Muungano wa Tanzania lililoingia madarakani mwezi Desemba mwaka 2005, lilipaswa kuvunjwa Desemba 5 mwaka huu badala ya Julai 17 kama alivyofanya rais.

  "Tunaitaka Mahakama itamke kuwa kifungu 41(7) cha katiba kinapingana na kifungu namba 13(6)(a) kinachohusu mgawanyo wa madaraka na uhuru wa mahakama kwa kueleza kuwa matokeo ya urais baada ya kutangazwa na Nec hayawezi kupingwa," inasema sehemu ya madai hayo. "Kitendo cha rais kulivunja Bunge tarehe 17 Julai ni kinyume na kifungu namba 65(1) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano ambacho kinaeleza kuwa kipindi cha muda wa Bunge ni miaka mitano," imesema sehemu ya hati hiyo.

  "Kifungu cha 46A cha katiba kimetamka bayana kuwa rais hatalivunja Bunge wakati akijua kuwa mwenyewe (rais) bado yupo madarakani kwa lengo la kuleta uwiano wa madaraka." Maringo amefungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Nec akiwa ni Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura.

  Katika kesi hiyo, anashirikiana na Kituo cha Haki na Demokrasia (CJD). Mbali na madai hayo ya awali, walalamikaji wametaka wabunge kurejesha fedha za walipa kodi walizopewa kwa ajili ya mafao yao, wakidai kuwa hawastahili kulipwa kwa kuwa hawakulitumikia Bunge kwa muda uliotakiwa. Madai mengine yaliyotolewa na walalamikaji hao ni pamoja na kupinga umri wa mgombea urais kuwa miaka 40. Walisema Mahakama inapaswa kuirekebisha sheria hiyo kwa kuwa ni ya kibaguzi.

  Walalamikaji hao pia wameiomba Mahakama kuondoa zuio liliolowekwa na baadhi ya vyama vya siasa kwa wagombea wake kushiriki midahalo ya uchaguzi kwenye vyombo vya habari wakisema hatua hiyo inawanyima wagombea hao fursa ya kujieleza; na wapigakura haki ya kujua sera za wagombea wanaopaswa kuwachagua.

  Madai mengine yaliyoelezwa kwenye hati hiyo ni kupinga mipaka ya kijiografia ya majimbo ya uchaguzi na upigaji kura iliyowekwa na Nec kwa maelezo kuwa yataleta matokeo yasiyo ya haki kwa wapigakura.Walalamikaji wametaka pia Nec itafsiri sheria za uchaguzi kwa lugha ya Kiswahili kuwawezesha wapigakura wote kuzifahamu na kujua haki zao kabla ya kufanya uamuzi.

  "Sheria inayomtaka mgombea kujua kuzumgumza Kiswahili tu ni mbovu kwani sheria zote huandikwa kwa lugha ya Kiingereza ingawa mijadala bungeni na mambo mengine ya serikali hufanyika kwa Kiingereza," anasema Maringo katika hati hiyo.

  Chanzo: Mwananchi
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ni kesi nzuri lakini mahakama haikawii kusema ni ya kisiasa na hivyo ipelekwe bungeni.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Utaona sasa mahakama haitatoa hukumu hadi uchaguzi upite. Nawashauri wasifanye hivyo .
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimeisikia muda huu hiyo taarifa redion. Itaweza kusaidia
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Good... make use of the "means" at your disposal to get rid of "them"
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  dalili za ukomavu wa kisheria, swali je mahakama zitapokeaje kesi za namna hii?

  My take is:hii kesi itakwisha mwaka 2020 mahakama ni slow sana kwenye kesi za namna hii.
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwa vyovyote vile ni mwanzo mzuri. hata kama NEC itatangaza matokeo ambayo siyo sahihi na halali angalau wanajua kitakachofuata. pia kata kama mahakama ikikataa kuisikiliza basi itafanyiwa kazi baadaye kwa ajili ya chaguzi zinazofuata
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,061
  Likes Received: 3,984
  Trophy Points: 280
  safii, nilitaka kushangaa wanasheria woote hawaoni walakini na hiyo sheria beberu ati matokeo ya NEC hayawezi kuingiliwa kati na mahakama! This country is going to dogs
   
 10. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Mwanzo mzuri kaka..... heko zako
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  well...lets await and see!
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Good beginning,tutafika tuu
   
 13. M

  Mundu JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wataichakachua tu hii kesi, kama walivyofanya kwenye ile kesi ya Mtikila inayohusu "mgombea Binafsi". Wasomi wetu (majaji) wanajali zaidi maslahi yao. Badala ya kusimamia haki na ukweli, wataamua kujikomba kwa viongozi waliowachagua. Utadhani walichaguliwa pasi na sifa!!

  Ni hatua nzuri, lakini itakuwa yale yale tuliyoyazoea na tuliyopata kuyaona na kuyasikia.
   
 14. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Ndugu maringo tunashukuru kwa kupinga sheria za kidhalimu. Iko siku mambo yatakuwa sawa.
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  I very happy on this matter!sasa tunaelekea kule ambapo nikuwa napaota kwa muda mrefu,ni vema sasa watanzania tuamke na kujua haki zetu!
   
 16. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mtikila wapi hiyooo??? Anyway,ni nzuri, lakini mizigo iliyopo pale judiciary,haitaenda popote hii kesi...
   
 17. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanaharakati wengine mko wapiiiiii...

  Onesheni solidarity ktk hili.... Shambulia huyu Adui wa Haki (aka AMANI)

  BIG UP MAN!!
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Huwa nabaki hoi na separation of power ya Tanzania;kesi ya Mtikila aliyofungua kutaka mgombea binafsi lkn majority opinion chini ya Jaji Mkuu Ramadhan wakasema wanaliachia Bunge kwenye issues zozote zinazopelekea kutamka kuwa Kipengele fulani ndani ya Katiba kimevunja katiba!

  Lkn mahakama hiyo hiyo juzi imesema kwa kauli moja tena bila woga kwenye kesi ya Prof Mahalu kuwa kipengele husika ndani ya katiba kinavunja katiba yetu;wala Bunge halikuhusishwa kwenye uamuzi wao labda kwa sababu ni kesi mbili tofauti!

  Si vyema kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani lkn hisia zangu zimekwisha nipa jibu kesi hii itakuaje!
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  MODS, Samahani, unganisheni hii thread.
   
 20. Z

  Zhu Senior Member

  #20
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is this blog for great thinkers or emotional thinker. I can see that all you look like you are under a certain age.
  You mostly argue emotionaly rather than criticaly.
   
Loading...