OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,208
- 103,785
Sehemu ya mahojiano ya Wakili Msomi Peter Kibatala na Mkuu wa upelelezi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, SSP Gerald Ngichi kuhusu kesi nambari 112 ya Mwaka 2018 inayowahusu Freeman Mbowe na wenzake.
KIBATALA: Umesema Freeman Mbowe aliondolewa kwenye Mkutano na walinzi wake?
SSP Ngichi: Ndio
KIBATALA: Unawajua walinzi wa Mbowe?
SSP Ngichi: Siwafahamu.
KIBATALA: Sasa uliwezaje kuwatambua kuwa ni walinzi wake?
SSP Ngichi: Walikuwa wakimsaidia
KIBATALA: Kwahiyo kila anayemsaidia Mbowe ni mlinzi wake?
SSP Ngichi: Kimya.
KIBATALA: Mbowe alisema hatupaswi kuona kawaida wenzetu kunyongwa hadi kuuawa. Je unajua alikua anamaanisha nini?
SSP Ngichi: Hapana
KIBATALA: Kwahiyo Mbowe yupo sahihi?
SSP Ngichi: kimya
KIBATALA: Umesema Mbowe alisema kuwa haiwezekani wanaume wazima kama sisi tugeuzwe mandondocha. Je kuna tatizo gani kwenye maneno hayo?
SSP Ngichi: Huo ni uchochezi
KIBATALA: Wewe ni mwanaume au mwanamke?
SSP Ngichi: Mwanaume?
KIBATALA: Je uko tayari kugeuzwa ndondocha?
SSP Ngichi: Hapana
KIBATALA: Kwahiyo Mbowe yupo sahihi?
SSP Ngichi: Kimya
KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Jacob Zuma alilazimishwa kujiuzulu. Je ni kweli au si kweli?
SSP Ngichi: Sifahamu
KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Mugabe aling'olewa madarakani. Je ni kweli Mugabe aling'olewa au hakung'olewa?
SSP Ngichi: Sijui
KIBATALA: Unawezaje kufungua mashtaka kwa mambo ambayo hata wewe hujui?
SSP Ngichi: Sifuatilii vyombo vya habari.
KIBATALA: Unadai Mbowe alisema Rais Magufuli ni Mwepesi kama Karatasi?
SSP Ngichi: Ndio
KIBATALA: Maneno hayo yana shida gani?
SSP Ngichi: Magufuli sio mwepesi kama karatasi
KIBATALA: Wewe unaufahamu uzito wa Magufuli?
SSP Ngichi: Magufuli yupi?
KIBATALA: Magufuli aliyeandikwa kwenye hati ya Mashtaka
SSP Ngichi: Simjui
KIBATALA: Kwahiyo kwenye hati ya mashtaka mmeandika watu msiowafahamu?
SSP Ngichi: Aulizwe askari aliyeandika hiyo hati
KIBATALA: Kama wewe humfahamu kwanini unakataa kuwa si mwepesi kama karatasi?