Kesi ya Dr Slaa yaanza kunoga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Dr Slaa yaanza kunoga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigMan, Jul 12, 2012.

 1. B

  BigMan JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  KESI YA KUPINGA NDOA YA DK.SLAA YAANZA KUNOGA


  Na Happiness Katabazi


  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,imemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Dk.Willbrod Slaa na mchumba wake Josephine Mushumbusi ambao ni wadaiwa katika kesi ya kupinga wasifunge ndoa Julai 21 , wawasilishe utetezi wao kwa njia ya maandishi Julai 30 mwaka huu.


  Hivi karibuni mke wa Dk.Slaa, Rose Kamili nee Sukum anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo alifungua kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 dhidi ya wadaiwa hao akiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia wadaiwa hao wasifunge ndoa inayokusudiwa kufungwa Julai 21 mwaka hu,kwasababu yeye bado ni mke halali wa Dk.Slaa na jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa.


  Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Laurance Kaduri ambapo alisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba
  anawataka wadaiwa wawasilishe utetezi wao kwa njia ya maandishi Julai 30 na mlalamikaji awasilishe hoja zake kama inaona inafaa Agosti 7 na kwamba Agosti 14 mwaka huu, kesi hiyo itakuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa.Hata hivyo mlalamikaji wala waidaiwa ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Mutakyamilwa Philemoni hawakuwepo mahakamani.


  Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya masuala ya ndoa,. Rose anaiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwaajili ya kupatanishwa. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dk.Slaa bado ni wanandoa.


  Dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk.Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.


  Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum(Chadema) huyo anadai mdaiwa wa pili(Josephine) alimshawishi mumewe(Dk.Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.


  “Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile,ndoa
  hiyo ihesabike kuwa ni batili.


  Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dk.Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia. Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili(Josephine) amlipe fidia ya shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake na kuongeza kwa kuimba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.


  Chanzo;gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Julai 13 mwaka 2012
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani wewe ndo mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima? Mbona umetangulia kuandika habari ya gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa tar 13.7.2012 kabla ya muda muafaka? Tafadhali tupe source nyingine tofauti na Tanzania Daima!
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe mbea, hata kama habari itakuwa ya ukweli lakini wewe ni mbea. Habari ya gazeti la ijumaa mbona unaitoa alhamisi? Au wewe ni mhariri wa gazeti hilo?
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Dah hi zengwe sijui kama Dr.Slaa atalivuka kiulaini
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani hii habari imeletwa hapa tarehe ngapi hata useme hayo?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tukisema yule jamaa ni mzinzi na kakaa anafanya zinaa tu, watu hawataki kukubali. Hii nchi sijui inaelekea wapi? au ndio "Nchi ya Ahadi"?
   
 7. g

  gnsulwa Senior Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilishasema kabla kuwa mgombea urais kwa ticket ya CDM 2015 ni Mbowe na si Slaa. Tayari cdm (Mbowe) wameshaanza kumtengenezea zengwe
   
 8. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi sioni haja ya kutaka kujua chanzo cha habari na wala hakuna haja ya kumtuhumu mleta mada, tujikite zaidi katika kuchangia mada iliyo mbele yetu.

  Jamani mimi bado sijaelewa kwanini huyu mzee Dr. Slaa amekiuka kabisa miiko na maadili ya kanisa Katoliki, kiasi kwamba ukiambiwa kuwa aliwahi kuwa Padri wa Kanisa Katoliki wala huwezi kuamini kwani haya anayoyatenda hayafanani hata kidogo maisha yake ya kiroho kama alivyokuwa miaka ya nyuma.

  Hivi amewezaje kumpanda mwanamke ambaye si mke wake mpaka akampa mimba na kumzalisha, halafu leo ndio akumbuke kuwa alitakiwa aoe, kwani hapo mwanzo hakulijua hilo? sasa leo anaumbuka vikwazo kila kona, sijui watoto wake wanajifunza nini?
   
 9. A

  Alhabaad Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hapo hajawa Amiri Jeshi Mkuu!!!
   
 10. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,954
  Likes Received: 1,772
  Trophy Points: 280
  Hakunaga kitu dr anafanya kwa bahati mbaya na hajawahi kukwama mahali popote..na hapo ndipo hata ccm huwa wanachoka na huyu mzee..hili swala ni dogo sana kwake.. yeye yuko bize na kupigania taifa letu..hayo mengine ni vijimambo tu..msioong ee sana..tegeni macho na masikio ndio mtajua how bright is he..!!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na ufuska lakini vile vile katika madai haya I smell rat:


  - dai la kwanza linavuruga maana ya madai mengine yote. hajui kuwa kesi zote chini ya family law huanza na usuluhishi nje ya mahakama?


  -dai la pili, anataka mahakama itamke kuwa ameolewa bila kuonyesha hati ya ndoa. Hajui kuwa mahakama inahitaji ushaidi wa ndoa kupitia sheria ya ndoa ya Tanzania. Nyumba ndogo kwa Tanzania haijawa ndoa kisheria ingwa Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alijitahidi kuwasaidia nyumba ndogo wawe wanatunzwa na wenzi wao.

  -dai la tatu, analazimisha mahakama iwafungishe ndoa yeye na dr slaa. Sidhani kama kuna sheria ya namna hiyo.

  -dai la nne halina nguvu yoyote kutokana na dai la pili na la tatu.

  nadhani mama huyu hakushauriwa vizuri kuhusu kesi hii.
   
 12. m

  manucho JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Akioa inawahusu nini ktk maisha yenu? Huyo anayedai amdai yeye this's personal business
   
 13. m

  manucho JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mama huyu anyedai hajui anataka nini
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii issue ndogo "isipokuwa Slaa busara ndogo sana"

  Mbowe for presidency 2015
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kesi ya kwanza iliishia wapi na hii mnayoileta leo inatofautiana na ile ya kwanza? Kabla ya kubuni hii kesi mlishaangalia kisheria vinginevyo msijeonekana kuzoea usanii badala ya mfumo wa kisheria.
   
 16. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kuwa Padre haimaanishi akiacha upadre basi ataendelea kuwa mkatoliki coz anaweza acha kabisa ukatoliki na kuwa mpagani na ndoa zake akafunga kiserikali. Na ndoa zote za serikali zinatambua kuwa mwanaume anaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini pia ndoa yaweza vunjika kwa talaka. Kwa hiyo sioni kosa hapa kwa Dr Slaa, afu pia huwezi jua kwanini aliacha upadre yawezekana aliacha coz mafundisho yake hakuyaamini. Sasa kutoamini mafundisho ya kanisa unalosali tayari ni vigumu sana kukaa ndani ya imani ambayo uhalali wake unamashaka nao. Wapo wengi sana wameacha na wamekuwa wapagani au wamehama madhehebu na dini pia. Tusiwe wepesi wa kuhukumu bali tuwe wepesi wakufanya utafiti kuhusu ukweli wa mambo, tuache ushabiki. I stand to be corrected
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,789
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kumnyooshea kidole mwenzio jiangalie wewe mwenyewe! wewe sio mzinzi? toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio! Mimi cjui kama ulikuwa na mwanamke mkashindwana ndani ya nyumba ukaaamua kutua mzigo ukaoa mwingine ni uzinzi! Tena aliweka hadharani na anataka kufunga ndoa takatifu huo uzinzi unaozungumzia ni upi? Uzinzi ni kama angeendelea na kuwa na wote wawili na tena kwa kificho. Na mwisho elewa kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu wote tumepungukiwa na utukufu wa mungu! Usikhukumu usije ukahukumiwa! na kipimo kile unachompimia jirani yako ndicho hichohicho utapimiwa siku ya hukumu! usingozwe na motives za kisiasa ukamkosea mungu wako siku ya mwisho ukalia na kusaga meno!!
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mama yake ridhwani yuko wapi? Kama alikufa nini kilimuua? Wakina jack zoka?
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kichuguu shkamoo...nimeopenda kweli analysis yako mwanana
  .asante sana
   
 20. Kipaji Halisi

  Kipaji Halisi JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 2,263
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Dr slaa kama ndesapesa ktk masuala ya mahusiano, wote wameacha wake zao wa awali,na wote wana wanawake wa nje tena kutoka kagera

  Ndesapesa ndio mkali yeye kahonga ghorofa mbili mtaa wa chwaku pale regent
   
Loading...