Baada ya watu kujadili hukumu ya kesi ya jamuhuri dhidi Mh. Lissu, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Mendeleo nimeona nami niiangalie kesi kwa jicho la mtu wa kawaida, ambaye si mwanasheria na namna hukumu inavyoathiri twasira ya mahakama kwa jamii.
1 .Iwapo kosa alilokutwa nalo mh. Lissu baada ya mlalamikaji ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kushindwa kuthibitisha kosa la uhaini, lingekuwa si la kufirika bali kuonekana moja kwa moja mfano kubaka, wizi au kupokea rushwa, kusingetokea malamiko kwamba lisu kaonewa. Ila kitendo cha mahakama kuu kutafuta kosa la kufikirika- Uchochezi ambao athari yake haikuonekana wakati mtuhumiwa anatamka na kudai kwamba waliochochewa walichocheka oktoba 2026 inasababisha watu wawe na mashaka na uadilifu wa mahakimu wetu, na mhimili wa mahakama kwa ujumla.
Aidha kauli ngapi zilishatolewa na CCM zenye elements za uchochezi mf hakutakuwa na nywinywi wala nywinywi, tutashinda kwa bao la mkono, ushindi ni lazima nk hazikuadhibiwa kisheria?
2. Kwa vile mtuhumiwa alikuwa ameshawekwa jela kwa siku zaizi ya 500 kwa kosa ambalo hakulifanya, unawezaje kumfunga miaka 4 kwa kosa dogo wakati ulisha muadhibu kwa kosa ambalo hakulifanya? Haki yake umeizingatia? Mimi naomba nieleze kusikitishwa kwangu na namna ambayo mahakama zetu zimegeuka kuwa nyenzo ya chama tawala kufanya siasa. Siasa chafu, zisizolitakia mema taifa letu. Ni hayo tu kwa leo.