Mkuu, ndio hutoi habari za blah blah lakini heading ya post yako ina mislead.....ilitakiwa iwe kama swali Re: Babu Seya na wanae kutoka jela? otherwise kwa namna ulivyopost you have already made a conclusion......Mimi sitoi habari za blaa blaa, nyie subilini tu,
Naona Bi.Lyamuya alikosea kuwa hukumu sawa sawa, alitakiwa awahukumu kunyongwa washenzi hawa...ingelikuwa hadithi saivi...wakenda appeal wanaweza wakapunguziwa miaka ua wakatoka...na uhuni walioufanya kwa visichana vile ni mkubwa na wakishenzi...aaaagh!
Sikusema kuwa hawana haki ya kukata rufani...lakini hata kama watashinda rufani hiyo haina maana kuwa na si lazima iwe hivyo, kuwa hawakufanya unyama ule...nafikiri kama sijakosea kuna memba hapa alituletea taarifa za kumbukumbu ya kesi ile na memba wengi wamesoma na wakakubali kuwa jamaa hawajaonewa wala hawajasingiziwa, ushahidi ulikuwa wazi na usio chembe ya shaka...na ndo maana hata mahakama kuu ika upheld uamuzi wa mahakama ya awali...na kwa kadiri nijuavyo, watakachofanya waheshimiwa majaji wa rufani ni kutazama kumbukumbu ya kesi tu na si kusikiliza kesi upya...na zaidi kwa kuwa wanapinga kutiwa hatiani...itatazamwa wapi maelezo ya kesi na sheria imekosewa...mpaka wakata rufani wakajihisi kuwa wametiwa hatiana isivyohalali...tusubiri lakini mpaka sasa tunahaki kuwaita...wahalifu, wabakaji...ndivyo mahakama za awali zilivyoamuwa na itabaki hivyo mpka mahakam ya juu ione vinginevyo.Kaka kukata Rufaa ni haki yao, na kama wakifanikiwa kutoka watakuwa wametoka kwa maamuzi ya mahakama na siyo kwa sababu wamependelewa, kwani ni wangapi wamefungwa kwa makosa ya kusingiziwa na jamii leo inawahesabu kuwa ni wahalifu wakubwa sana duniani? Punguza hasira, ingawa ni kweli kitendo hicho kinaumiza lakini vita subira nao watimize haki yao ya kukata rufaa. Isipokuwa kama nawe unaoushahidi endelea kuwashutumu na kuwaitwa waninii vileeee! Loo siwezi kurudia kutamka
Kuna uhusiano gani kati ya hao uliowataja na raisi..??nguza v nkik na wanawe wa wapi baba mama kaka dada mjomba shangazi bibi babu shemeji
Mmh nashindwa kuelewa jamani kama walishapelekwa congo wale tuliowaona wakiimba na kucheza pale ukonga ni akina nani?
Hii inasikitisha sana na mara nyingi nikisoma hii taarifa ya Nguza Family natokwa na imani na viongozi wa nchi hii. Kwa kuwa sijui ukweli halisi wa hili, nadhani wako wenye data. wasiwasi wangu ni kwanini kesi hii ilendeshwa chemba sana.
Kama ni harakati za kuamsha ari ya kuwezesha rufaa ya Nguza nadhani ikianzia hapa JF naiamini JF ni wanaharakati wenye uhakika na kile wanachofanya.
Hapana ... hawakupakaziwa ... hawa watu walicheza mkanda wa mambo hayo na watoto .. mkanda ukauzwa nje ya nchi .. some foreign ambassodor to tanzania had gone back home on an errand ... akaufuma huu mkanda ambayo aliletewa akaambia see what is happening in Tanzania ... the ambassodor who knew the culprits came back to TZ ... called top officials and showed them the mkada ... luckily the guys were easily identified ... and the only thing to do was to pin them down ...wakatumia hizo mbinu as wale watoto waliyowachezea wasingepatikana .. this is why hii kesi no one could tamper with with it as there was recorded evidence ....
They are paying for their sins
Sina hakika kama issue ya Mzee Nguza Viking na wanae iliwahi kukatwa hapa, by then ilipokuwa hot nilikua sija join JF. Kwanza kabisa lazima niseme kwamba sifagilii kabisa vitendo vichafu vya aina yoyote ile kwa watoto na kama kweli walifanya hayo wanayotuhumiwa kufanya- they deserve to rot in jail.
Wikiend hii nilibahatika kukutana na mtu ambaye alitoa ushahidi kwenye hii kesi (Mwanamuziki na rafiki wa karibu wa Papii) na my feelings kwamba hawa jamaa walikua stitched up zimezidi kukua.Baadhi ya mambo aliyoniambia ni pamoja na kwamba baadhi ya tarehe na saa ambazo Papii anatuhumiwa kushiriki kwenye huo ufirauni- hakuwepo kabisa jijini Dar na hata pale alipokuwepo Dar, alikua yuko jukwaani akifanya kile anachopenda kufanya.Jambo jingine la kushangaza pia ni usiri mkubwa wa jinsi ambavyo kesi hiyo iliendeshwa, na chanzo changu cha habari kinaamini kwamba kwa sababu hii ushahidi mkubwa na wa maana umetiwa kapuni.Hadi leo huyu jamaa anamtembelea Papii gerezani na anasema huwa anagoma kula kwa siku kadhaa na kushinda akilia tu, anatamani afe kuliko kuendelea kuishi na machungu ya uonevu aliofanyiwa yeye pamoja na nduguze.
Nimesikia mengi kuhusu hii kesi- ambalo ni common kwa wengi ni kwamba Mzee Nguza aliingia anga fulani za Waziri mmoja wa serekali ya sasa na waziri huyo aliahidi kumkomesha- yeye pamoja na familia yake.Kuna baadhi wanasema sio Waziri ni Balozi fulani. Kwa jinsi nionavyo mimi, inawezekana labda watoto wakafanya kitu kama hiki peke yao bila baba yao and the vice versa is possible.Lakini kweli inaingia akilini kwa mzee mzima wa kiafrika kufanya huo upuuzi mbele ya wanae huku wakipokezana tena kwa kitoto kidogo?
Rumours zimekua nyingi kwenye hii kesi - kuna yeyote anayeujua ukweli wa hii kesi? I understand kwamba hawa jamaa walikata rufaa na ikatupwa, is there any other way anyone can help them?
Nje ya mada kidogo, Bluray uko wapi mkuu?
Kuna sehemu kwenye hiyo attached doc wameandika:
voire dire examination
Lakini siamini kama ilitakiwa kuonekana hivyo, sio voir dire examination?
Well, ni ndefu sana (35 pages) lakini ni muhimu kuisoma kujua undani wa kesi yenyewe
Haya maandishi ya wanasheria usihangaike kusoma yoooooooote, nimesome vipengele kadhaa na kupata kujua kuwa nini wamelenga... Wanazunguuuuka kufanya reference za kesi za miaka hiyo mfano ukurasa wa 4 mpaka 14 nadhani ni reference za kesi tu, unaachana nazo... Pia kuna errors kadhaa ambazo zinatakiwa kurekebishwa, uzuri ni kuwa Tanzania mtu akiandika 'gay' badala ya 'guy' hata mahakamani wanajifanya wamemwelewa kuwa alitaka kuandika 'guy' kakosea kidogo.mie nimeprint nitasoma home ni ndefu sana
kulikuwa na rumours kuwa ni mganga wa kienyeji ndio alitoa hayo masharti kwa babu seya na familia yake kuharibu watoto. Ni kweli ni rahisi kuwaza kuwa kwa mwafrika kufanya kitendo kama hicho kwa kushirikiana na watoto wake sio rahisi lakini kwa upande mwingine, kwa mwafrika kuamini maagizo ya mganga wa kienyeji ni rahisi kuliko kuamini ushauri wa daktari.
Amini usiamini waganga wa kienyeji wakitoa (kama mkwara)tamko leo kua kila aziniye atakufa baada ya siku saba, UKIMWI utakuwa ndio kwa heri.