Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 363
Sina hakika kama issue ya Mzee Nguza Viking na wanae iliwahi kukatwa hapa, by then ilipokuwa hot nilikua sija join JF.
Kwanza kabisa lazima niseme kwamba sifagilii kabisa vitendo vichafu vya aina yoyote ile kwa watoto na kama kweli walifanya hayo wanayotuhumiwa kufanya- they deserve to rot in jail.
Wikiend hii nilibahatika kukutana na mtu ambaye alitoa ushahidi kwenye hii kesi (Mwanamuziki na rafiki wa karibu wa Papii) na my feelings kwamba hawa jamaa walikuwa stitched up zimezidi kukua.
Baadhi ya mambo aliyoniambia ni pamoja na kwamba baadhi ya tarehe na saa ambazo Papii anatuhumiwa kushiriki kwenye huo ufirauni- hakuwepo kabisa jijini Dar na hata pale alipokuwepo Dar, alikuwa yuko jukwaani akifanya kile anachopenda kufanya.
Jambo jingine la kushangaza pia ni usiri mkubwa wa jinsi ambavyo kesi hiyo iliendeshwa, na chanzo changu cha habari kinaamini kwamba kwa sababu hii ushahidi mkubwa na wa maana umetiwa kapuni. Hadi leo huyu jamaa anamtembelea Papii gerezani na anasema huwa anagoma kula kwa siku kadhaa na kushinda akilia tu, anatamani afe kuliko kuendelea kuishi na machungu ya uonevu aliofanyiwa yeye pamoja na nduguze.
Nimesikia mengi kuhusu hii kesi- ambalo ni common kwa wengi ni kwamba Mzee Nguza aliingia anga fulani za Waziri mmoja wa serekali ya sasa na waziri huyo aliahidi kumkomesha- yeye pamoja na familia yake. Kuna baadhi wanasema sio Waziri ni Balozi fulani.
Kwa jinsi nionavyo mimi, inawezekana labda watoto wakafanya kitu kama hiki peke yao bila baba yao and the vice versa is possible. Lakini kweli inaingia akilini kwa mzee mzima wa kiafrika kufanya huo upuuzi mbele ya wanae huku wakipokezana tena kwa kitoto kidogo?
Rumours zimekuwa nyingi kwenye hii kesi - kuna yeyote anayeujua ukweli wa hii kesi? I understand kwamba hawa jamaa walikata rufaa na ikatupwa, is there any other way anyone can help them?
=====
Kuhusu hukumu, soma Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu
UPDATE:
Hatimaye waachiliwa kwa msamaha wa Rais. Habari zaidi soma...
Breaking News: - Mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na Mwanaye Johnson Nguza (Papii Kocha), watoka jela kwa msamaha wa Rais Magufuli